ZANZIBAR NI YA MWANZO. !! JE NINI KIMEISIBU ZANZIBAR ??

Hashim bin Faustin

Senior Member
Jan 30, 2017
177
216
ZANZIBAR NI YA MWANZO

katika mwaka 1884 Sultan wa zanzibar Sayyid said walitiliana mkataba wa kibiashara na Marekani

wakati huo Zanzibar ilikuwa ni Nchi ya mwanzo kutumia Nishati ya umemr katika nchi za Afrika Mashariki

ambapo Zanzibar ilikuwa inazalisha Umeme wake kupitia kinu cha Taa ambacho kilipatikana kwa mahusiano ya Zanzibar na marekani

Uingereza ilikuwa bado inatumia Gesi,kinu cha Taa hicho ambacho kilikuwa eneo la Malindi kiliiwezesha Zanzibar kutokuwa tegemezi katika Nishani hiyo

pia ikawa ndio chachu ya Nchi za Bara kupata umeme mpaka Nchi za Afrika ya kati kama vile Kongo

Bwana Abdurahman Babu akiandika utangulizi kuhusu yaliyopita katika mapinduzi ya zanzibar ndani ya kitabu kiitwacho

'SIKU 100 ZA KUUNDWA MUUNGANO WA TANZANIA UHASIDI WA MAREKANI KWA MAPINDUZI YA ZANZIBAR"

Babu anazungumzia maendeleo ya zanzibar siku za mwanzo ikishirikiana na marekani

"Wamarekani walijenga kinu cha lifti ya kwanza ya umeme katika Afrika mashariki

pia Marekani iliiwezesha Zanzibar kufaidi kuwa na Taa za Barabarani mapema mno kuliko hata london

ambayo london wakati huo bado inatumia Taa za Gesi"

si hivyo tu bali kutoka zanzibar mitambo ya simu iliyosambazwa kutoka Aden kwenda London Uingereza kuja Zanzibar

kadhalika Mitambo hiyo ilitoka Zanzibar kwenda Bagamoyo

leo utaona athar za hayo hapo tunapopaita 'Welesi' ilikuwa Mitambo ya 'Wireless"

iliyokuwa ikisafirisha mawasiliano kutoka Unguja kwenda Bagamoyo,Rwanda,Barundi,Uganda mpaka Koñgo

kadhalika kutoka Unguja kwenda Aden mpaka Uingereza

ndio tunasema Zanzibar ni ya Mwanzo kutandaza waya za simu "Wireless"


na ikawa ndio ya mwanzo kutumia Lift ya Umeme katika Ghorofa la Baytul Ajaaib

Ni vijana wangapi leo hii wanaojua kwamba Mji wa Zanzibar ulikuwa wa mwanzo kuwasha Taa za umeme Barabarani na Mitaani zikiitwa 'Taa za Stimu' kabla ya London na New york?

Aliyekuwa Balozi wa Marekani Nchi, wakati anamaliza muda wake


Bwana Mark Green, wakati akitoa khutuba yake ya kuaga alisema

"Meli za Marekani zilikuwa zikitia Nanga katika Bandari ya Zanzibar kuja kununua Mafuta ya Nyangumi kwa ajili ya kwenda kuwashia Taa zao za Barabarani wakati Zanzibar inatumia Umeme.

Swali la kujiuliza haya yote yamekwenda wapi na kwa nini Zanzibar hivi sasa inashindwa kujitegemea na kuzalisha umeme wake kuliko kutegemea Nishati hiyo Tanzania Bara?

leo Zanzibar inategemea kampuni kibao za Simu zenye makao yake makuu Tanzania Bara

nini kimeisibu Zanzibar ishindwe kusimama kwa miguu yake.
 
Hii makala baada ya muda mfupi tu itakuwa ni ya kichochezi...

Nadhani kuna mashindano ya TZ vs Kenya, Dar vs Nairobi jukwaa fulani, sasa kabla hamjamalizana na utengano utakaotokana na mashindano hayo, sasa tumeshahamia ndani.

JK wakwanza alisema "dhambi ya kubaguana haiishi, ni kama kula nyama ya mtu"

Kila la kheri Tan & Zan
 
mkuu ccm ni hatari, hebu angalia wanavyowaharibu wasomi kama maprofesa, angalia lipumba na wengine wengi tu, ndiyo itakuwa wazanzibari?
 
Mkwepa kodi,

CCM inaharibuje usomi wa mtu? Nadhani kuna tofauti ya usomi na kujitambua, wakidhani wameharibiwa na CCM, basi ujue wana vyeti na hawajitambui. Na hivyo vyeti una haki ya kuvitilia shaka.
 
Back
Top Bottom