Habari wakuu,
Leo Rais Magufuli ni mgeni Rasmi kwenye kilele cha mbio za uhuru. Pia leo ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kinachoendelea sasa ni dua na sala kutoka kwenye Sheikh na Askofu, kuwa nami...
======
Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wote walishawasili na kuimbwa wimbo wa Taifa.
Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki shughuli hii, mwaka jana nilimuomba Rais Shein aniwakilishe Simiyu.
Watanzania tunafaa kujiuliza kwanini tunamkumbuka Mwalimu Nyerere, nijuavyo siku hii iliamuliwa kuwa siku ya kitaifa ili kujikumbusha mchango mkubwa na usiosahaulika wa mwalimu Nyerere.
Nimuona ni jambo jema kumzungumzia kidogo Mwalimu Nyerere, historia ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ilikuwa ni ndefu. Kwanza alikuwa mzalendo, TANU iliongoza harakati za kutafuta Uhuru nae alikuwa kiongozi.
Umbali wa kutoka Pugu mpaka ofisi za TAA, kwenda na kurudi ilikuwa kilomita 46 na alitumia fedha zake kusafiri na wakati mwingine kulazimika kutembea, tujiulize leo viongozi wangapi wanaweza kujitolea kiasi hiko.
Alipoambiwa kuchagua kati ya kazi na TANU, aliamua kuchagua TANU. Nna uhakika maisha yalikuwa magumu, wasomi wa kiwango chake wakati huo walikuwa wakihitajika sana, watanzania wangapi wangeweza kujitoa hivyo? Viongozi wangapi kwa kufanya kazi kwenye makampuni ya kigeni, wanatusaliti?
Yeye na familia yake waliishi maisha ya kawaida sana, hawakujilimbikizia mali. Kuna mifano mingi ya viongozi wa zama zake hata sasa.....
Mwalimu Nyerere hakukubaliana na wafanyakazi waliotaka kuongezewa mishahara, alifanya mfano kwa kujipunguzia mshahara wake. Je sisi tuko tayari kuacha mishahara hewa? Je! Mishahara tunayopata tuumeifanyia kazi? Je! Tuko tayari nasi kujipunguzia au kuacha kuishinikiza serikali kuongeza mishahara na marupurupu yetu ili kuwezesha kuboresha huduma za jamii kwa manufaa ya watanzania na hasa watanzania wote?
Ninasema hivyo, simaanishi kuwa mishahara isiongezwe, La Hasha! Ninachotaka kusema ni kwamba, kabla ya kudai nyongeza ya mishahara, ni lazima kwanza kufahamu uwezo wa serikali. Lakini pia tutambua kwamba kuna watanzania wenzetu wengi wanaohitaji kuboreshewa huduma
Tuna mifano inayoishi kwa hapa Zanzibar, baada ya Shein kushika madaraka, mishahara ya kima cha chini imepandishwa 150,000 mpaka 300,000 lakini na sisi kule Bara, baada ya kuchukua hatua za kupunguza watumishi hewa pamoja na watumishi ambao hawakutakiwa serikalini na kuanza kujisafisha sisi wenyewe.
Tumeshafanya uchambuzi kwa watumishi 59,967 watarekebishiwa mishahara yao na promotion zao karibu bilioni 159 zitaanza kutolewa kuanzia mwezi unaokuja lakini tusingefanya uchambuzi, tungelipa bilioni 89 kwa watumishi hewa.