Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Kampeni chafu, kibaguzi na za kujenga chuki nahofu zinatiririka kila siku. Bhati mbaya sana lugha hizi zinazotoka kwenye chombo cha serikali ZBC kila kukicha na vipindi hivi viko chini ya wa watu teule mabingwa wa fitinakutoka chama maarufu kinacho hubiri upendo na amani. Mawaidha wanayoyatoa yanahatarisha utengemano wa watu waZanzibar kama hatua muafaka haitachukuliwa. Kipindi hiki kiinaongozwa na kiongozi wa juu wa ZBC na wanasiasa wa msimu wsiokuwa namvuto au walioanguka kwenye chaguzi zilizopita!
Mbinu hizi za Ministry of love hutumika wakati mambo yanapoonekana kuwa magumu kisiasa upande wao chama hiki kongwe. Nakumbuka wizara hii ilitumika kumpaka matope Dr, Salim alipokuwa anawania kuchaguliwa na chama kugombania Urais wa Jamhuri ya Tanzania na kumwambia kuwa yeye si mzanzibari..
Matunda ya ndoa za nguvu zilizoanzishwa na mzee KARUME,kwa lengo la kuondoa ubaguzi leo limekuwa ndio kichecheo kikubwa cha kuwagawa watu. Tulitarajia nini muhadimu akioa muhindi kinachozaliwa kitakuwa kama Seif Iddi?
Hivi leo tukiuwambia mzimu wa Sheikh Thabit Kombo mtoto wake kuitwa chotara na hivyo hana haki Zanzibar utatusamehe? Mjukuu wa mzee Karume muasisi wa ndoa za nguvu Fatma Karume ni chotara na hana haki ya kuzungumzia kitu nchi yake lakini akina Bulebo ndio wanayohaki atajisikiaje?. Leo mtoto wa Memba wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi, Brigadier Yussuf Himid mwanawe ni chotara kungekalika?
Vipindi vya aina hii vyenye viashiria vya chuki, fitina na uhasama visipewe nafasi kwenye chombo cha walipa kodi