Zain yauzwa India

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,850
Kampuni ya simu za mkononi ya Bharti Airtel Limited (“Bharti”) kutoka India, imenunua rasmi kampuni ya simu za mokono ya Zain inayoendesha shughuli zake katika nchi 15 za Afrika, ikiwemo Zain Tanzania, kwa gharama ya Dola za Marekani bilioni 10.7 (takribani Sh. trilioni 14.4).
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti, Sunil Bharti Mittal, alitangaza kufikiwa kwa makubaliano hayo na kwamba serikali za nchi 15 za Afrika ambako Zain ilikuwa inaendesha shughuli zake wameafiki ununuzi huo.
“Tumefurahi kukamilisha makubaliano haya kwa ajili ya India na Bharti. Tunapenda kuzishukuru kwa dhati serikali za nchi zote 15 pamoja na serikali ya India kwa kutuunga mkono katika hatua hii muhimu. Na hii itakuza zaidi uhusiano wa kihistoria baina ya India na Afrika katika masuala ya kiuchumi na kijamii na kupelekea kuboresha ushirikiano kati ya Kusini na Kusini,” alisema Mittal.
Mwenyekiti huyo alisema Bharti imedhamiria kuchangia kukua kwa mawasiliano ya simu katika bara la Afrika kwa kusambaza huduma ndani ya nchi hizo na kutoa huduma zenye bei nafuu ambazo zinawagusa watu wa kawaida.
“Tunawaahidi wateja wetu wa Afrika mambo kabambe na bidhaa na huduma kadhaa zenye ubunifu wa hali ya juu,” alisema.
Hata hivyo katika ununuzi huo, wafanyakazi wapatao 6,500 wa Zain katika nchi hizo hawatapoteza ajira, kwani wataendelea na ajaira zao chini ya kampuni hiyo mpya.
Naye Mwenyekiti, Zain, Asaad Al-Banwan, aliishukuru Bharti kwa kufanikiwa kununua Zain na aliitakia mafanikio mema katika kuendeleza kukua kwa mawasiliano ya simu barani Afrika.
Nchi ambazo Bharti imenunua shughuli zake ni Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Sierra Leone, Tanzania, Uganda, na Zambia.
Hii ni mara ya tatu Zain Tanzania inauzwa kwa wabia mbalimbali, kampuni ambayo ilianza kwa jina la Celtel chini ya uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakati huo ikiongozwa na MSI/Detecon, waliokuwa wamenunua hisa asilimia 35 za TTCL chini ya mkataba uliosainiwa Februari 21, 2001.
MSI/Detecon waliokuwa wamenunua hisa hizo kwa Dola za Marekani milioni 120, walilipia nusu ya fedha hizo na kukabilidhiwa uendeshaji wa kampuni hiyo na albaki ya Dola milioni wangelipa baada ya kuyafanyia ukaguzi mahesabu ya TTCL. Hata hivyo baadaye kiasi kilicgokuja kulipwa kilikuwa ni chini ya Dola milioni nane baada ya mvutano mrefu wa kisheria na kuamuliwa kumalizana nje ya mahakama.
Baadaye Celtel ambayo serikali ya Tanzania ni mbia, hisa zake zilinunuliwa na kampuni ya Celtel International ikimilikiwa na bilionea mwenye asili ya Sudan, Mohamed Ibarahim, ambaye siku hizi anaendesha utoaji wa tuzo nono na maarufu ya Dola za Marekani milioni tano kwa wakuu wa nchi za Afrika wastaafu ambao walizingatia utawala bora wakiwa madarakani.
Miongoni mwa wakuu wa nchi waliokwisha kushinda tuzo hiyo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano na yule wa Botswana, Festus Morae. Mwaka jana Tuzo hiyo haikutolewa kutokana na walioshindania kutotimiza vigezo vya utawala bora.
Celtel International nayo iliuzwa kwa Zain ya Uarabuni, miaka miwili iliyopita baada ya kuiendesha kama Zain International Afrika ikabadilishwa kuwa Zain mwaka 2008 na sasa imeuzwa kwa Bharti.
CHANZO: NIPASHE
 
Nina swali ? are they going to change the name.?
 
Kamchezo kalikuwa katamu sana haka,toka zamani wanajua tulipigwa hivi bunge huwa linafanya kazi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…