Zaidi ya Ng'ombe 700 wamekamatwa ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti


Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
5,629
Likes
6,195
Points
280
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
5,629 6,195 280
Zaidi ya Ng’ombe 700 mali ya wafugaji watano wa kijiji cha Mwauchumu kata ya Gillya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wamekamatwa na askari wa wanyamapori wa hifadhi ya taifa ya Serengeti (SENAPA) kwa madai ya kuingia ndani ya hifadhi hiyo kinyume cha sheria ya hifadhi za taifa sura 282 ya mwaka 2002, jambo ambalo limesababisha baadhi ya ndama kufa kutokana na kushindwa kunyonya.

Ng’ombe hao 765 ni mali ya wafugaji watano wa kijiji cha Mwauchumu ambao ni Shima Masunga, Mang’welela Marini, Tahalama Ntunga, Samson Yuma na Johnson Makeja wamekamatwa usiku wa juni 6 majira ya saa sita usiku asubuhi na askari wa wanyamapori wa hifadhi ya taifa ya Serengeti katika eneo la upande wa magharibi mwa hifadhi hiyo, ambapo kila Ng’ombe anatakiwa kulipiwa faini ya shilingi elfu 50, hatua ambayo imelalamikiwa na baadhi ya wafugaji.

Alais Melawi ni mwanasheria wa chama cha wafugaji kanda ya kaskazini amesema kutokana na Ng’ombe hao kushikiliwa kwa siku nne na kusababisha mateso kwa mifugo hiyo, ikiwemo kukosa malisho na maji ameiomba serikali kupitia kwa waziri wa maliasili na utalii Prof. Jumanne Maghembe kuiagiza SENAPA kuiachilia mifugo hiyo kabla haijaleta mgogoro huku pia akikosoa kiwango kikubwa cha faini kilichoamriwa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa Serengeti.

Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Serengeti William Mwakilema amethibitisha kukamatwa kwa mifugo hiyo.


Chanzo: ITV
 
mkunyegere

mkunyegere

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2013
Messages
441
Likes
52
Points
45
mkunyegere

mkunyegere

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2013
441 52 45
Sheria lazima ichukue mkondo wake
 

Forum statistics

Threads 1,236,522
Members 475,174
Posts 29,260,682