Yusuph Manji awekwa chini ya ulinzi siku 20, aiomba mahakama iingilie kati

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa mujibu wa sheria.

Manji yuko kwenye matibabu Hospitali ya Aga Khan jiji hapa akiwa chini ya ulinzi baada ya kuachiwa kwa dhamana.

Februari 20 mwaka huu, alipelekwa ofisi ya Uhamiaji mkoa na kuhojiwa kwa madai ya kuingia nchini kinyume cha sheria.

Katika kesi hiyo wajibu maombi hayo ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo aliyefungua kesi ya maombi hayo, anataka Mahakama iagize maofisa uhamiaji na polisi kumfikisha mahakamani ili iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kuagiza aachiwe.

Katika hati ya maombi hayo, Ndusyepo anadai kuwa alimtembelea mteja wake hospitali ya Aga Khan Februari 17 mwaka huu na kukuta maofisa wa Uhamiaji wakimsubiri mteja wake wampeleke kwa ofisa Uhamiaji wa mkoa kwa mahojiano dhidi ya tuhuma kuwa siyo raia wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Ndusyepo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited na Diwani wa Mbagala Kuu, Amedai kuwa alitoa maelezo kwa maofisa Uhamiaji na alirudishwa Aga Khan ambako yupo chini ya ulinzi hadi leo.

Chanzo: Mwananchi

pic%2Bmanji.jpg
 
kama Manji sio raia wa Tanzania, aliwezaje kupata nafasi za uongozi alizokuwa nazo?

kuna watu pia wakuchukuliwa hatua hapa, na pia inonekana watanzania hatuko salama kama mtu ambaye sio raia anaweza kupenya na kuwa na hizo nyadhifa...
 
Nimeshangaa wanasema sio raia wa Tanzania
Inasemekana (tetesi) anamiliki passport ya nchi nyingine. Na huenda alikuwa ameificha nyumbani na walipopekuwa wakaikuta. Sheria za Tanzania zinasema huwezi kuwa na uraia wa nchi mbili na unapokuwa na uraia wa nchi nyingine basi ule wa Tanzania automatically unakuwa umefutika. Tuseme kwa mfano ni kweli anamiliki passport ya nchi nyingine na alikuwa anaficha, sidhani kama kuna namna serikali ingeweza kujua!
 
Katka ili kuna uonevu mtanzania halisi ni yupi?nataka niwe waz sio uchochezi ebu tumuulize rais wetu baba yake na babu yake alizikwa wap?kama ni tanzania au la?tujiulize mhaya au msukuma mtanzania ni yupi?manji n raia mm nasema hivo hanijui simjui ila kama tunataka kuwa salama tuache visasi,haiwezekan tuishi kwa visasi ndugu haiwezekan ccm ya maguful ndo bora kuliko ccm zilizopita sawa?
 
Wakili wa Yusuph Manji amesema mteja wake yuko chini ya ulinzi kwa siku 20 na ameiomba mahakama kuilazimisha uhamiaji na polisi imfikishe mahakamani.
=====

Kwa ufupi
Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa mujibu wa sheria.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa mujibu wa sheria.

Manji yuko kwenye matibabu Hospitali ya Aga Khan jiji hapa akiwa chini ya ulinzi baada ya kuachiwa kwa dhamana. Februari 20 mwaka huu, alipelekwa ofisi ya Uhamiaji mkoa na kuhojiwa kwa madai ya kuingia nchini kinyume cha sheria.

Katika kesi hiyo wajibu maombi hayo ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo aliyefungua kesi ya maombi hayo, anataka Mahakama iagize maofisa uhamiaji na polisi kumfikisha mahakamani ili iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kuagiza aachiwe.

Katika hati ya maombi hayo, Ndusyepo anadai kuwa alimtembelea mteja wake hospitali ya Aga Khan Februari 17 mwaka huu na kukuta maofisa wa Uhamiaji wakimsubiri mteja wake wampeleke kwa ofisa Uhamiaji wa mkoa kwa mahojiano dhidi ya tuhuma kuwa siyo raia wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Ndusyepo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited na Diwani wa Mbagala Kuu, Amedai kuwa alitoa maelezo kwa maofisa Uhamiaji na alirudishwa Aga Khan ambako yupo chini ya ulinzi hadi leo.

CHANZO: Mwananchi
 
Back
Top Bottom