Yupi anafaa kati ya hawa

BABU KIZEE

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2013
Posts
452
Reaction score
72
Wakuu napata mtiani mgumu kutoa maamuzi hawa maduu wananichanganya sana ,niko kwenye mchakato wa kutaka kuoa mwanamke yupi anafaa kati ya hawa WATATU.

WA KWANZA; kabila ni mzigua ni mwanamke aliyetulia hana mapepe mnaweza kupanga kitu akakuelewa lakini baadaye akabadilika, usipomtafta kwenye simu hakutafti , ni mfanya biashara, elimu yake fomu four, msafi sana , ni mweupe na mrefu. Ana malingo sana,

WA PILI: kabila msukuma,mwelevu ,msema ukweli, mtulivu,elimu yake fomu four,msafi,rangi maji ya kunde na msafi sana. anajua kujali. Mpenda zawadi sana, hana kazi yoyote.

WATATU; NI msambaa mtu wa Tanga ,mfupi mweupe ,mpenda starehe sana,ana matumizi makubwa bila kujali kipato changu, ni mchangamfu kupita kiasi, anajua kucare, anapenda pesa kupita maelezo , ukimwahidi kitu lazima aking'ang'anie., mpenda matanuzi, mfanya biashara na mtaftaji sana.
 
jambo moja la msingi 6x6 je?
 
Umeshawapasha habari kua wako watatu? Ukiwataarifu utakua umepata akufaaye/
 
Hiv unaweza kupenda watu 3 kwa pamoja?

lazma kuna ambae moyo wako ume base zaid! So fuata moyo wako.

over!
 
wape huu mtihani atakaeshinda ndo anafaa.

@
MTIHANI KWA MADUU
1.rais wa tz ni kikwe..... a)ta b)te c)ti d)to e)tu
2,mlima mrefu afrika ni kilima...ro a)nja b)nje c) nji d)njo e)nju
3.sitoi penzi bila pe... a)sa b)se c)si d)so e)su.
 
Ukitoa cfa za ktandan bac utapata majib sahih zaid...so kawachunguz vzur then urud tena
 
mbombo ngafu, wewe mwenyewe unajua yupi unamkubali zaidi sema tuu unataka faaida ya bure hapa JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…