Kwanza kabisa naomba nijulikane sipo upande wowote wa kisiasa, Ila naomba nimwelezee pole pole kidogo kulingana na upeo wangu mdogo
Pole pole ni MTU wa kupiga kazi kimya kimya hasa kwa siku za hivi karibuni hasa baada ya kupata UDC Ubungo, alikuwa anapenda kufanya mambo kimya kimya pasipo kutumia Media kama Madereva , ilifikia kipindi jamaa alikuwa anapiga kazi hadi SAA Tano usiku pale aneo lake la kazi kwa kusimama muda wote huku akisikiza na kusolve kero za watu bila kujali ukada,
Kiukweli Mimi nilikuwa namfuatilia kwa karibu sana na hata alivyotoka pale wananchi wa Ubungo walisikitika sana kwa jinsi jamaa alivyojitoa. Kwa Mara ya kwanza toka nizaliwe ndo niliona kazi ya Mkuu wa wilaya kwa jinsi jamaa alivyokuwa anafanya kazi yake, nikawa najiuliza hii ndo kazi ya mkuu wa wilaya au jamaa kapililiza majukumu yake.
Kulingana na haya Nina amini kule aliko Ajenda ya kupiga kazi kimya kimya inaendelea na Matokeo yanaweza kuonekana kwa jinsi wao wanavyojitasmin,
Hivyo kuwa Mwenezi kwa upande wake inawezekana anaendesha kwa jinsi anavyoona na jopo lake la Uongozi, Tuchukulie hata CDM, kwa wale ambao hawafuatilii sasa karibu mwenezi sizani kama anawika sana kiasi kwamba hata mtoto wa Primary anamjua huyu ni mwenezi wa CDM