Yuko wapi Lucas Seleli?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,273
Lucas Seleli alikuwa mmoja wa wajumbe wa tume iliyochunguza kashfa ya Richmond chini ya uenyekiti wa Dr. Harrison Mwakyembe. Ripoti ya tume ile ndiyo iliyopelekea Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu ingaw mjadala ulipopamba moto Mwakyrmbe akadokea kuwa kuna siri nyingine walizificha ili kuiokoa serikali isiporomoke yote. Baada ya pale mwenyekiti wao akanusurika kifo kw ugonjwa usiojulikana mpaka leo. Rafiki yake Sitta akatangaza kuwa m/kiti alipigwa sumu. Mgonjwa mwenyewe akaahidi kuweka wazi wabaya wake. La ajbu Seleli akatoswa hata kugombea ubunge kupitia CCM. wenzake walioonekana bado ni vidomo domo wakapewa vyeo. Mwakyembe kapewa uwaziri wa uchukuzi, Sitta akaundiwa wizara isiyokuwa na tija yoyote kwasababu tayari wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ipo. Yule mama Stella Manyanya licha ya kuukwaa tena ubunge wa dezo wa viti maalumu akaongezewa na ukuu wa mkoa wa Rukwa.

Nina muulizia Seleli kwasababu wenzake wote waliokosa ubunge kupitia CCM ktk ngazi ya kupitishwa na chama au uchaguzi wenyewe wamepewa vyeo vya ukuu wa wilaya, mkoa, ubalozi kuwekwa kwenye mabodi mbali mbali. Seleli sijamsikia. Alikosa nini? au hakuonesha ushrikiano katika kuficha ile siri? Maana mwenzake Mwki pamoja na kupiga makelele sana baada ya kuchungulia kaburi alipopewa uwaziri kawa mpole kama malaika. Ama kweli :"If you can't fight them, join them!" Ndaga na maloli pijo Mwaki!
 
 
yuko wapi mpendazoe. simwoni maandamano chadema.

alijidanganya sana mpendazoe.
 
hata nami nilikuwa najiuliza huyu mtaalam wa Kilimo yu wapi au ndo anapasua mapori nzega kukamilisha mbiu ya Kilimo Kwanza
 
mmmmh watakuja wenye majibu sahihi sasa
 
Aligombea tena ubunge nzega lakini akawa wa 2 kwenye kura za maoni,hapa tatizo siyo involvement yake kwenye kashfa ya richmond bali wananchi walimtosa
 
miezi kadhaa iliyopita Lucas Selelii nilikuwa namuona kwenye tv akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya mazingira ya Ngorongoro conservation area authority.
 
Aligombea tena ubunge nzega lakini akawa wa 2 kwenye kura za maoni,hapa tatizo siyo involvement yake kwenye kashfa ya richmond bali wananchi walimtosa

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Nzega, utakubaliana na mimi kuwa tatizo halikuwa wananchi kumtosa Bw. Seleli. Huu ulikuwa ni mwendelezo wa siasa za visasi na chuki ndani ya ccm ili kuhakikisha kuwa jamaa harudi tena mjengoni. Katika hao, kwanza ni kundi la EL, RA, AC na washirika wao waliotumia mamilioni ya fedha kwenye kura za maoni kuhakikisha bashe anachukua jimbo. Walifanikiwa kwa hatua ya kura za maoni, lakini CC ikasema bashe sio raia. Kwa akili ya kawaida yoyote kabisa option iliyokuwepo ni ama kuchukua mshindi wa 2 (ambaye alikuwa Seleli) au kama hakupishana sana kura na mshindi wa 3, basi wangeweza kurudia uchaguzi kwa mshindi wa 2 na wa 3. Katika kudhihirisha kuwa Seleli alikuwa haitakiwi sio tu na kundi la EL, bali pia na CC, wakaamua kuteua mgombea aliyeshika nafasi ya tatu, dr. Kigwangawala.

Kwa kifupi Bw. Seleli bado ni mtu anayekubalika kwa wapiga kura wa Nzega, lakini hatakiwi na ccm. Changamoto aliyo nayo ni ama kufanya maamuzi magumu ya kuhama chama au akubali kuwa kwa kuendelea kubaki ccm huu ndio mwisho wake kwenye ulingo wa siasa za Nzega na Tz kwa ujumla.
 
  1. Huyu Lucas Lumambo Selelii katika uchaguzi Mkuu 2010 katika kura za maoni CCM ilikuwa hivi: wakwanza alikuwa Husein Bashe,Lucas Selelii alishika namba mbili na DR Kigwangalla alikuwa wa tatu.
  2. Mtakumbuka katika uchaguzi ule Bashe aliwekewa pingamizi la kuwa yeye siyo raia.Kwamaana hiyo ilitakiwa achukuliwa Mtu wa pili ambaye alikuwa Lucas Selelii,lakini mizengwe ikafanyika wakamwambia kuwa Hana mvuto kwa wapiga kura Ili asirudi tena Bungeni wakamtosa, ndipo akachukuliwa DR Hamis Kigwangalla.
  3. Kwa sasa yupo tu na mishe mishe zake bado anajipanga.ila bado yeye ni ccm damu japo ccm walisha muona kuwa kapoteza mvuto kwao
 
Bashe alimpiga na kitu chenye Ncha kali kichwani hadi leo yuko hoi analima Nyanya Nzega
 
yuko wapi mpendazoe. simwoni maandamano chadema.

alijidanganya sana mpendazoe.

Mpendazoe alidanganywa na Sitta, Mwakyembe na NApe. Wakamwambia ajitambulishe na CCJ wakati wao wakiisaliti CCM na NApe akiiba siri za CCM. Ndiyo maana alikuwa akijinasibu kuwa wako vigogo wangejiunga CCJ. Hakuja wenzake ni ma-opportunist. Walipobandikwa vyeo wakafyata na siri zao. Sam six kamaliza bunge kihuni baada ya kuahidiwa uspika. Wakati ulipofika akakosa sifa. Kwa hiyo hata Lembeli alitoswa. Wajanja ni mawaziri hata kama hauna tija kama wa Afrika Mashariki.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…