Yuko wapi Baraka Harrison Mpenja (Sauti ya Radi) mtangazaji kiongozi wa kabumbu Azam Media?

Jones Clean

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
393
678
Habari wajumbe.

Ni muda Sasa sijamsikia mtangazaji maarufu wa kabumbu wa Azam Media, Baraka Harrison Mpenja a.k.a Sauti ya Radi ambae mechi zote kubwa mara nyingi huwa anakaa nyuma ya kipaza sauti. Ila kwa siku za hivi karibuni gurudumu hili limekuwa likiongozwa na Gharib Mzinga (Kilwa Finest) pamoja na Ayoub Hinjo. Je nini kimempata huyu Sauti ya Radi? Au na yeye ameitwa kamati ya nidhamu kama Cleotas Chota Chama kutoka kule Unyamani?

Merry Christmas kwa wote tunaposubiri kuzaliwa kwa mwokozi wetu.
 
Kuna siku sijui Twitter aliuliziwa hivihivi.Mwananzengo mmoja akaandika Hivi,Nanukuu."Karibu katika uwanja wa Benjamin Mkapa ,Hali ni shwari kabisa.Jiji la Mama na Mama anaupiga mwingi."Mwisho wa kunukuu.

Hayo ni maneno yake kwenye mechi moja Hivi.Sasa pengine maboss wake wameona anafiti zaidi kwenye siasa zaidi ya kwenye chombo Chao.
 
Back
Top Bottom