Yesu alisema msinililie bali lilieni nafsi zenu,je na sisi tumuombe mtu au tujiombee wenyewe?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa wasimlilie yeye bali walilie nafsi zao. Je, huoni kuwa hata sisi yatupasa kuliombea Taifa hili kuliko kumuombea mtu mmoja?

Binafsi sioni umuhimu wa kumuombea mtu kwani hata waliopita kabla yake waliombewa kuanzia Makanisani,Misikitina na mpaka Bungeni lakini waliyoyafanya kila mtu anajua.

Ni bora tukaombea wagonjwa na wenye shida tutapata thawabu kwa mungu kuliko kuombea wanasiasa.

Nawashauri sana tuyakumbuke maneno ya Yesu hasa katika kipindi hiki.
 
hata wimbo wa Taifa una kasoro hii hii , urekebishwe haraka , tulipaswa kuishia kwenye Mungu ibariki Tanzania tu , Ile " wabariki viongozi wake " haikuwa sahihi , kila mtu ajiombee mwenyewe , haiwezekani Mungu kuwabariki watu wababe , dhulumati au walevi , haiwezekani .
 
Halafu wanapoongopa na kufanya ubabe wao wanasahau kabisa, wanasahau pia kwamba waliapa kwa bible Na Quran, sio sahihi hata kidogo Na wajiombee wenyewe
 
Nasikitika kukwambia kwamba.... Huna unacho kijua hata juu ya huyo Yesu uliemnukuu....ni bora ungekaa kimya tu mkuu kuliko kidhalilisha imani yako kiasi hiki
 
Hayo mapepo ya uongo,wizi,dhulma,ulaghai tutayatoa kwa kumwomba Mungu...inategemea unavyoomba kwa Mungu.
Kuomba sio gharama, tuombe viongozi wachafu waanguke na watetezi wetu wasimame imara tuliinue taifa pamoja.
 
Halafu wanapoongopa na kufanya ubabe wao wanasahau kabisa, wanasahau pia kwamba waliapa kwa bible Na Quran, sio sahihi hata kidogo Na wajiombee wenyewe
kuna mlemavu mmoja akitoa maoni yake kwenye tume ya warioba alipendeza maneno ya kuwaombea viongozi kwenye wimbo wa Taifa yaondolewe , huwezi kuwaombea wapagani ; hii ni hatari sana !
 
2Nyakati 7:14 Ikiwa watu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha kuomba na kutubu na kuziacha njia zao mbaya, nitasikia kutoka juu mbinguni na kuwasamehe uovu wao na kuiponya nchi yao.

Kuna mstari unasema waheshimuni wenye mamlaka maana wamewekwa na Mungu.

Kuna sehemu inaeleza zamani wakati wana wa israel walikengeuka na kukataa uongozi uliokuwepo na kuamua kuweka viongozi wao-hao viongozi wao wakaanza kuwanyanyasa na kuwatesa ila Mungu alikaa kimya kwasababu walitaka wenyewe.

Mchango wangu:
1. Kutokana na maelezo hapo juu, ni wajibu wa wananchi kuomba na kutubu kwa ajili ya taifa lao ili mambo yaende ikiwa ni pamoja na kuombea viongozi.

2. Tunaposhindwa kusimama kwenye nafasi zetu kuombea taifa na viongozi, rushwa, mateso, na uovu tunauona sio kwamba Mungu haoni, anaona ila anaamua kuacha na kukaa kimya.

3. Maombi ya kuombea taifa ni zaidi ya kuita mashehe na wachungaji wafanye show off ya kuomba.

Ni mtazamo!!
 
Yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa wasimlilie yeye bali walilie nafsi zao. Je huoni kuwa hata sisi yatupasa kuliombea Taifa hili kuliko kumuombea mtu mwingine?

Binafsi sioni umuhimu wa kumuombea mtu kwani hata waliopita kabla yake waliombewa kuanzia Makanisa,Misikitina na mpaka Bungeni lakini waliyoyafanya kila mtu anajua.

Ni bora tukaombea wagonjwa na wenye shida tutapata thawabu kwa mungu kuliko kuombea wanasiasa.

Nawashauri sana tuyakumbuke maneno ya Yesu hasa katika kipindi hiki.
Uliweza kumwombea Lowasa tu!
Alipopigwa chini ukaona maombi hayajibiwi! JIPU SUGU WEWE
 
Nasikitika kukwambia kwamba.... Huna unacho kijua hata juu ya huyo Yesu uliemnukuu....ni bora ungekaa kimya tu mkuu kuliko kidhalilisha imani yako kiasi hiki
ndugu kiongozi huna haja ya kutoa mapovu , tumekubaliana nchi nzima hatutaombea mtu , jiombeeni wenyewe na escrow zenu , hii hoja ni ya kisiasa na bwana yesu hapa amenukuliwa kama mtu maarufu tu , usigeuze hoja hii kuwa ya kidini , mambo ya akina mazinge hukohuko.
 
Sorry blaza,Yesu sio "mtu maarufu" mngemnukuu gwajima tungeelewa. Hatuwezi kuacha mtu atumie jina la Yesu kusimamia jambo la kuongopa lenye hisia za chuki
 
Theolojia ni somo linalosomewa kwa zaidi ya miaka mitano, ulichokiandika hakifanani kabisa na mtu anayeijua theolojia. Yesu aliposema msininilie mimi alimaanisha mifumo ya kimaisha ya dunia hii imezama katika kutafuta kinachokwenda tumboni badala ya kutafuta haki kwa wote. Dunia ambayo Yesu alikuwa anaiongelea ni ile ambayo yeye kwa uwezo wake aliipa chakula kwa muujiza lakini bado ikafanya mipango ya kumuua, dunia isiyokuwa na upendo wala shukrani.

JPM anaposema aombewe anamaanisha kwamba anataka kupambana na hao wasiokuwa na upendo wala shukrani, watu ambao wanaihujumu nchi yao halafu wanataka kutumikiwa. Watu ambao wanapitisha mafuta bure pale bandarini, halafu wakifanya kosa wanahonga kila idara na hawafungwi. Yesu aliongelea watu wasio na huruma, wenye kusahau upesi juu ya neema zote za Mungu kwa sababu tu ya vyeo vyao vya kidunia. JPM anaomba tumuombee kwa sababu kupambana na mifumo michafu inayoamini katika mbingu iliyopo duniani ambayo maisha yake ni mafupi, sio kazi ndogo, kuvunja mirija ya kinyama sio shughuli nyepesi.

Jitahidi usome sana theolojia kabla hujaanzisha mada za kisiasa zinazojenga hoja kupitia mafundisho yanayotoka kwenye vitabu vitakatifu.
 
Unateua watuhumiwa wa Escrow,unateua watu waliodhihaki afya za wengine(hata mungu hapendi),n.k,alafu unataka eti tukuombee!!
 
Yoyote yule asiye na dhambi kati yenu na awe wa kwanza kumrushia jiwe huyu mwanamke, Baada ya kuyasema hayo Yesu akainama na kuchora mchangani, aliposimama na kutazama juu hakuna kati ya wale wanaume aliyekuwa amebaki mahali pale...akamgeukia mwanamke na kumwambia nenda zako....
 
sasa ni wapi aliposema tuombee wadhulumaji na wababe ?
 
Back
Top Bottom