Yanga lazima ishinde mechi zote za nyumbani Kombe la Shirikisho

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
YangaMtibwa.jpg

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, wataanza kibarua kizito Ijumaa ijayo Juni 17, 2016 wakati watakapokuwa ugenini nchini Algeria kukabiliana na klabu ya MO Bejaia katika mchezo wa Kundi A la Kombe la Shirikisho.

Yanga, ambayo pia imetwaa Kombe la Shirikisho Tanzania, iko katika nafasi nzuri ya kufanya vyema kwenye mashindano hayo ikiwa kasi yake iliyokuwa nayo tangu kuanza kwa msimu haitavurugwa na mwenendo wa uchaguzi ndani ya klabu hiyo.

Ingawa imepangwa na timu ngumu kama hiyo ya Algeria pamoja na mabingwa mara tano wa Afrika, TP Mazembe na Medeama ya Ghana, lakini Yanga bado inayo nafasi kubwa ya kufanya vizuri ikiwa utulivu utakuwepo klabuni pamoja na umakini kwa kikosi hicho.

Soma zaidi hapa => http://www.fikrapevu.com/yanga-lazima-ishinde-mechi-zote-za-nyumbani-kombe-la-shirikisho/
 
Sina hakika na hilo hasa kwa Algeria na TP Mazembe, hizo timu hatari hazijui neno ugenini. Wahenga walisema Simba hana poli geni.
 
Back
Top Bottom