Labda wana wakomoa Simba
Mkuu wanashangaa bure Wapare kuuza mbuzi ili ashinde kesi ya kuku kumbe na huku Jangwani wapo Wapare wa Kizaramo na Kihindi.Sasa wote hao wanini?Alafu ukute pesa iliyowasajili hao strikers wote ni mara mbili ya pesa ya ubingwa wa vodacom!
hapo ndipo ninaamini yanayosemwa na wachambuzi wa soka kwamba yanga ni sehemu ya kuulia vipaji. Walioshituka walikimbia mapema sasa hivi wanachukua zawadi y awachezaji bora wakiwa na timu zinazojua kukuza vipaji na wanazidi kuonekana na kung'ara kimataifa.
Acha wakaue soka lao huko wakiridhika na vihela mbuzi vya kuchukulia machangu sunsiro na corner bar.
Kwa kweli hili la javu kwenda yanga hata mm sijapendezwa nalo, ingawa ameenda timu ninayoipenda, ki mtazamo javu alikuwa anaweza kucheza vizuri zaidi kma angeendelea kucheza timu isiyo kuwa na lundo la mafoward wala presha, kma alipotoka mtibwa.
Pia dhana ya kuwa had uchezee yanga au simba ww ndio mchezaji, inawaponza wengi, hata kama kivutio ni maslai ila waangalie badae watakuwa wapi, isije kuwa msimu mmoja tu unaonekana hufai, wajifunze kwa wachezaji wengine kwa kilichowatokea baada ya kukimbilia timu hizo.