kwa habari zilizonifikia hivi punde ni kuwa timu ya Yanga inatarajia kukata dhidi ya mchezo wao na Azamu uliochezwa leo kwenye uwanja wa taifa na Azam Fc kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa mawili ya Yanga.kwa mujibu wa taarifa hyo Yanga watakata rufaa kwani MTANGAJI aliyekuwa akitangaza mpira huo alitangaza goli la mwisho la Azam kuwa ni yanga ndio wamefunga badala ya kutamka Azam ndio waliofunga,kwa mantiki hiyo wanahisi ni hujuma wamefanyiwa na wanaadhimia kuwasilisha rufani yao TFF ili mechi hiyo ichezwe upya.
aka2030 said:Hawa jamaa wanaupendeleo sana leo uwanja wa taifa walikuwa wanashoot mechi ya yanga na azam huku wakiionyesha kwenye big screen. Cha ajabu magoli yote yanga waliokuwa wakifunga jamaa hawakuwa wanayarewwind kwenye big screen kwa style hii inamaana itakuwa inawabeba tu azam
Na sababu nyingine hii hapa:
sababu nyingine ni ubovu uliokithiri wa uwanja wa taifa na mawingu kuzuia jua hivyo kuwapa Azam kivuli
Sababu nyingine kwanini bao lifungwe kwenye muda wa nyoongeza.
Nasikia wamesema mchakato wa katiba unawachanganya wachezaji ao wanaomba ligi iahirishwe
kigogo umetisha aisee...nimecheka usikuu mpaka bac
Baraza la wazee mbona kimya??????sababu nyingine ni ubovu uliokithiri wa uwanja wa taifa na mawingu kuzuia jua hivyo kuwapa Azam kivuli
Wazee waliongea baada ya mechi ya Mbeya City wakasema: "Sisi wanatuona hatujasoma na hawataki kuongea nasi na huyo mkenya wanamwona anajua basi anajua maana huko alikotoka kaendeleza vilabu vingi vina maendeleo basi anajua lakini sisi wazee tunasema mpira una mambo yake ya asili na inabidi yaheshimiwe, huyo mkenya si wanasema anajua basi anajua" nilimsikia mzee mmoja wa Yanga anaongea magic fm, safari hii hakuwa mzee Akilimali.Baraza la wazee mbona kimya??????