Yanga FC msijidanganye ' Kiufundi ' bado hamna uwezo wa Kuifunga Simba SC katika ' Derby ' ya tarehe 30, Septemba 2018

Endeleeni kujipa moyo kwa Kigezo cha kushinda mechi zenu Nne ( 4 ) mfululizo za Ligi ila ukweli upo na utabaki pale pale kwamba ' Kiufundi ' kabisa na hapa naweka ' Mahaba ' yangu ya Usimba kando / pembeni kwamba bado Yanga SC haina Kikosi imara cha kuweza Kucheza na Simba SC.

Tena ni vyema mkawa tu wapole kwani kuna uwezekano mkapata Kipigo ambacho kitaumizeni sana na hamtoamini. Na mnachokosea na nimewashangaa mno mnashangilia John Boko kutokuwepo kwakuwa alipata Kadi Nyekundu jana wakati mnasahau kwamba kuna Watu wengine wapo ' bench ' ambao muda wowote wanaweza wakabadili matokeo na bado Simba SC ikashinda.

Kama kuna eneo ambalo Yanga SC ipo vizuri ni Ushambuliaji tu ila kama kuna eneo ambalo Yanga SC ipo vibaya na ambalo ndilo litawaumizeni hiyo tarehe 30, Septemba 2018 basi ni eneo lenu la Ulinzi na kidogo katika ' midfield ' yenu.

Endapo Simba SC siku hiyo pale mbele atasimama Medie Kagere na Emanuel Okwi huku katikati wakiwepo ' Injini ' zinazoelewana za Simba SC Jonas Mkude, Maulid Dilunga na James Kotei halafu pembeni wakawekwa ' Viberenge ' akina Shiza Kichuya na Mohamed Ibrahim naziona Goli za haraka za Simba SC na pia nina uhakika kunaweza pia kukawa na Kadi za Njano kadhaa na hata Nyekundu kwakuwa najua hawa Wachezaji tajwa hapa watawasumbua mno Mabeki na Viungo wa Yanga SC hadi itapelekea wapo ' Kupaniki ' na kupoteza mechi.

Naiheshimu sana Yanga SC na kama Mwanamichezo napenda pia Kuipongeza kwani kidogo sasa inaanza kurudi vizuri katika mstari na kuna kila dalili kwamba kama Yanga SC itaendelea hivi na kumuamini Kocha wao na hamasa ikazidishwa basi huko mbeleni itakuwa ni ' mshindani ' mzuri katika Ligi ila kwa sasa ' msijidanganye ' bado ' Kiufundi ' hampo vizuri na bahati mbaya ni kwamba mnaibuka washindi dhidi ya Timu ambazo zenyewe pia hazipo vizuri ' Kiuchumi ' na zina matatizo ya Kiutendaji.

Bado naiona Simba SC kuibuka mshindi tena wa Goli zaidi ya mbili ( 2 ) hiyo tarehe 30, Septemba 2018.

Nawasilisha.
Mechi zote za hivi karibuni Simba wakiwa wanatumia viungo watano bado kiungo mmoja tu wa yanga aliweza kuwalaza na viatu, Papii Kabamba Shishimbi akitajwa mchezaji bora wa mechi. Kwaiyo sehemu ya kiungo Simba ata wawe watano kama ilivyo sasa bado Shishimbi atawafunika.

Hatari ninayo iona kwasasa Yanga wanakasi kubwa wakiwa wana shambulia na Simba wana wachezaji wenye umli mkubwa hasa katikati ya difensi na ilo ndilo eneo ambalo Yanga watalishambulia. Tusubiri tuone itakavyokua.
 
Mikia kucheza na Yanga wanaona kama wanacheza na USM Alger kwenye CAF Championship mpaka wanaomba mechi kuhairishwa wajiandae....TFF mjitathimini sana
 
Eti mkuu kuna ukweli wowote kuhusu hilo suala?

Hizi ndo timu ambazo hazijafungwa hatrick mpaka sasa
1)SIMBA
2)AZAM
3)JK TANZANIA
4)MBEYA CITY
5)PRISON
6)ALLIANCE
7)MTIBWA
8)KAGERA
9)LIPULI
10)KMC
11)AFICA LYON
12)STAND UNITED
13BIASHARA
14)SINGIDA
15)MBAO
16)NDANDA
17)RUVU SHOOTING
18)MWADUI
19)COSTAL UNION

KM TIMU YAKO HAUION HAPO MUULIZE ALEX KITENGE


Hizo ndio timu zenye mataja ya VPL chini ya 27.

Ukiona timu yako haipo ujuo ina mataji zaidi ya 27.
 
Mind game ni nini na mbinu ya mchezo ni nini. Kama utatumia mind game kwenye mchezo hiyo itakuwa part ya mbinu ya mchezo.
Simba huwa anamfunga yanga kwa mind game zaidi na si mbinu za kimchezo...MANARA SASA ANAUMWA..NANI ATAONGEA TRASH TALK...?
 
Back
Top Bottom