Mkuu tukubaliane na ukweli huu japo ni mchungu, Yanga sasa hivi hali ya uchumi ni mbaya mno:Twite, Niyonzima wagoma... Yanga - Global Publishers
WACHEZAJI wa kigeni wa Yanga wametangaza mgomo mkali kwenye timu hiyo, kutokana na uongozi wa timu hiyo kushindwa kumlipia kodi ya nyumba, beki Mbuyu Twite.
Twite, ambaye ni raia wa Rwanda, amekuwa akidaiwa kodi ya nyumba anayokaa Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kwa mwezi anatakiwa kulipa shilingi 600,000, lakini uongozi wa timu hiyo ambao kwa mujibu wa mkataba wake ndiyo unatakiwa kumlipia, umekuwa ukimzungusha.
Beki huyo kisiki alianza mgomo wa kutotokea mazoezini kuanzia juzi Jumatatu na viongozi wa timu hiyo wamekuwa wakitupiana mpira kulizungumzia suala hilo.
Championi ambalo jana lilitinga kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika katika Uwanja wa Loyola jijini Dar es Salaam, lilishangaa kuona kiungo mahiri wa timu hiyo, Haruna Niyonzima naye akikosekana kwenye mazoezi hayo, lakini lilipouliza kwa uongozi, bado halikupata jibu sahihi.
Chanzo cha ndani cha uhakika ambacho kilizungumza na gazeti hili jana, kilisema kuwa kiungo huyo naye amejiunga kwenye mgomo na Mnyarwanda mwenzake, huku Didier Kavumbagu raia wa Burundi na Hamis Kiiza nao wakitajwa kuungana nao siku zijazo.
"Amewaambia anaumwa, kawadanganya, yupo sawa tu, sema hafurahishwi na jinsi viongozi wa klabu wanavyompa ahadi ambazo kwake anaona kama ni dharau," kilisema chanzo chetu.
"Mimi nimezungumza naye leo (juzi asubuhi), ameniambia kuwa hana tatizo lakini hili suala lake la nyumba anaona kama ghasia kutoka kwa mwenye nyumba, ambapo kila siku wanamuona anaamka na kwenda mazoezini huku kodi akishindwa kulipa, hivyo amekasirika sana.
"Unajua hapa sasa wanachofanya viongozi ni kumweka kocha (Ernie Brandts) katika wakati mgumu, anawakosa wachezaji kama hao katika mazoezi anawezaje kuandaa timu tayari kwa mechi na ratiba inaonyesha Yanga ina michezo migumu hivi karibuni?
"Timu ina wachezaji wengi lakini lazima tukubali Yanga ikiwakosa hao inaweza kuwa katika wakati mgumu kwenye mechi zake na hapo ikitokea timu ikafungwa viongozi watamgeukia kocha na kuwa wakali wakati wao ndiyo wanaomkwamisha.
"Hivi sasa Mbuyu na Huruna wameonyesha kutokukubaliana na hili kwa kujiweka kando lakini wakati wowote usishangae kusikia kuwa hata Kiiza na Kavumbagu nao wakiungana na wenzao, kwa nilivyofuatilia nimeambiwa kuwa kwa upande wa Haruna kodi yake inaisha leo (jana), sasa sijui itakuwaje."
Mkuu tukubaliane na ukweli huu japo ni mchungu, Yanga sasa hivi hali ya uchumi ni mbaya mno:
1. Wanadaiwa zaidi ya 100M na wale Mapro wawili waliofungua madai FIFA na mpaka sasa hivi hawajalipwa.
2. Nsajigwa na mwenzake wanaidai yanga zaidi ya milioni 15 baada ya kukatiza mikataba yao lakini Yanga wako hoi wanasubiri makato ya milangoni ndiyo walipe.
3. Hivi karibuni walijishebedua kukwamishwa ujenzi wa uwanja wao na serikali kumbe wanadeni la kodi ya ardhi lisilopungua milioni 100 ambalo halijalipwa toka miaka ya 90.
4. Funga kazi ni hii hapa, wamemshawishi mtoto wa watu limbukeni Mrisho Ngassa kusaini timu mbili huku wakijua ni mali halali ya Simba SC laki wakimpa moyo watakuwa nayeye mpaka mwisho hata kwa kuirubuni TFF ili tu Simba igonge mwamba, lakini mwisho wa siku kutokana na ukata mkali wa pesa Ngassa amejikuta yuko peke yake.
Amejikuta akilipa mwenyewe faini ya 45M bila kusaidiwa na timu ya Yanga na bado anatakiwa kuitumikia kwa miaka 2. Pole sana Ngassa, lakini endelea kuonesha mapenzi ya dhati hata wakati huu mgumu wa kutembeza bakuli kuchangiwa. Likifika kwangu nitakuchangia japo buku usipofika nitakuwekea kwenye akaunti yako (01J2095037800) uliyoinadi kwenye Mwana Spoti.
Mkuu ahsante kwa kunikumbusha majina ya hao Maproo.Msemaji na Mwesiga wanadai 115
Ndlovu na Marash wanadai 106, kila kona madeni