Yaliyotokea Loliondo sasa Monduli

Yaliyotokea Loliondo sasa Monduli

olee

Member
Joined
Nov 24, 2011
Posts
97
Reaction score
23
Loliondo, Mvomero, Kiteto, sasa Monduli

Hofuimetanda katika baadhi ya watu wa kata ya sepeko wilayani Monduli. Hakunaanayejua nini kitatokea. Wala hakuna anayejua ataenda wapi. Hii ni baada yakuambiwa sehemu mnayoishi ni mali asili na saa yoyote mnaweza kupewa notice. Sasawamekua na mgogoro katika nafsi zao, baina yao, na viongozi, na serikali.

Mgogoro hutokea pale pande mbili au zaidi yambili ikihasimiana ikiwa kila upande inafikiri ndo yupo sahihi. Kila upande ikihisihaki yake inapokonywa. Kushindana katika hali kama hii mgogoro hutokea. Naisipopata mwafaka mapigano ya umwagaji damu yaweza kutokea.

Nchiyetu tofauti kama hizi yamekua mengi sana. Migogoro haya yamekua yakihusianishakutofautiana kwenye rasilimali hasa ya ardhi. Migogoro haya yamekua yakitokeabaina ya watu binafisi, jamii Fulani na jamii nyingine ambayo mara nyingiwakulima na wafugaji au jamii Fulani na serikali au mwekezaji. Chanzo yamigogoro haya yamekua ikisababishwa kugombania mipaka au mara nyingine eneozima bila kujali mpaka ikiwa kila upande inahisi ana haki ya kumiliki.

Mifanoni mingi tu, Loliondo wameingiakwenye mgogoro mzito sana na mwekezaji ambaye alikua natetewa na serikali. Watuwalipoteza maisha baada ya kuuwawa na asikari wanaomtii mwekezaji na wenginekupoteza mali kwani maboma yao yalichomwa moto. Na hata kupoteza mifugo yaowakati wa mgogoro.

Mfanomwingine ni ya Kilosa na Kitetoambayo hawa wamefanana. Migogoro yao imetokea baina ya wakulima na wafugaji. Nahapa wengi wamepoteza maisha na mali. Kila mmoja anadai ndo mwenye haki katikasehemu tajwa.

Nihivi majuzi tu wananchi wa sehemu ya Monduli katika kata ya sepeko wameingia katika mgogoro ambao hawajawahikuifikiria. Wamejikuta wakiambiwa sehemu mnayoishi na kufanyia shughuli zenusiyo mali yenu. Ni sehemu ya hifadhi (mali asili). Hawa wananchi wakapigwa nabutwaa.

Taarifawanazozipata ni kwamba kuna siku mnatangaziwa notice ya kuondoka. Khaaa!,wanauliza tumeishi hapa sasa kwa zaidi ya miaka 40. Wanaambiwa Serikalihaitambi hilo ni kwamba sheria ya mwaka 1974 inaosha hili ni sehemu ya maliasili. Zaidi wakaambiwa ukubwa wa eneo unaohitajika ni ekari hekta 3,600.Katika eneo tajwa, wananchi maelfu wanaishi ndani yake.

Hawawananchi wanapewa notice bila kupewa sehemu mbadala ya kwenda. Hawa wananchiwameishi hapo kwa miaka 40. Kuna watu wamezaliwa hapo na kuzeeka hapo. Hawajuipa kwenda, cha kufanya hata pa kujitetea hamna.

Ndiyosheria zipo lakini wenye kutekeleza hizi sheria walikuwa wapi kwa miaka 40sasa, hawa wananchi waligawiwa maeneo husika na serikali zao za vijiji. Uongoziwa hizi vijiji ni halali kabisa na walikua wanawasiliana na serikali yahalimashari ya wilaya.

Sasaeti leo baraza la madiwani wamepitisha azimio, kwamba hawa wananchi wapo kwenyehifadhi. Hawa wapiga kura wenu waendewapi? Kweli tunasikia kuna fidia, ni ya kuifanyia nini?Mtuanapoishi kwa miaka 40 sasa anayo mashamba, makazi ya kudumu na rasilimalimengine mengi yasiyo hamishika. Ghafula bin fuu unamwambia tunakupa notice yakuondoka. Hakuna makubaliano ya kueleweshana ya nini kifanyike. Bali nikuambiwanotice inatolewa.

Kwahali kama hii, kwa usumbufu kama huu, mgogoro utaepukikaje? Hawa watu nimchanganyiko wa wakulima na wafugaji. Kuna watu wana mashamba makubwa sana.Afadhali ya wafugaji wanaweza kuhama na mifugo yao. Je wakulima kama mtu alikuwana zaidi ye ekari 50 atapata wapi huko anakohamishiwa au anakohamia aridhi kubwakiwango hiyo ambayo ni tayari kwa kulima.

Nahisiserikali inatengeneza mgogoro kama wa Loliondomaana inasemekana kuna mwekezaji. Bila kujali madhara itakayotokea kwa wananchina hata usumbufu watakao pata wao kama serikali.
karibuni kwa mjadala!!!

ahsanteni
 
Mkuu nipo Arusha kikazi kwa wiki hii na bahati nzuri nipo wilayani Monduli, nimejaribu kufuatilia Uzi wako na baadae kutafuta wahusika, Hakuna hata mmoja anayejua hili, kwa sasa nipo hapa sepeko maarufu kwa jina Meserani au Duka mbovu ambayo ndiyo kaka ya Sepeko, wananchi wanasema hawana taarifa kama hiyo na viongozi (watendaji na Madiwani wanasema hawajui. Je notice hiyo umeiona wapi?
Njoo na taarifa iliyonyooka yenye vyanzo sahihi. Unaposema ni eneo la maliasili unamaana gani? ni kwa ajili ya misitu au wanyama? kwa kifupi eneo hili lilikuwa na mashamba makubwa ya NaFCO na upande mwingine ni eneo la jeshi ambalo kwa miaka mingi wananchi wanekuwa wakitumia kwa kilimo kwa sharti la kutopanda mazao ya muda mrefu, wananchi waliruhusiwa kupanda mazao ya chakula ya muda mfupi kama mahindi na maharage
Hebu funguka kama unataarifa za ndani zaidi
 
bosi cjabuni hii habari na kimsingi haihusianai na huko meserani...ni sehemu ya misitu upande wa juu wa kijiji cha lashaine/orkeeswa, lendiknya, orkaria na huko monduli juu. leo tunavyoongea kuna kikao kati yavijiji nlivyotaja. kujadili atima yao. tarehe 29. mwezi huu ndo wanakja kuonshewa mipika na kupewa notice. ni mchakato wa muda miezi kadhaa.
 
Mkuu sie wa huku mjini tunaiona bahari ile na hakuna makazi yeyote, lakini atuwezi jiamulia kwenda kuangusha vibanda vyetu usiku tulale na upepo mwanana. Maana kuna utaratibu wa kuzingatia sheria za ardhi na nchi.

Sasa kama wewe unalima na huna hati ya kumiliki hiyo ardhi kama sheria inavyotaka ujue anytime unaweza amishwa hata kama umekaa miaka 100 sheria ndio hipo hivyo, hiyo ardhi unayotumia bado ni mali ya serikali mpaka njia sahihi zipitiwe ya wewe kupewa hati miliki (hapo tena huwezi amishwa bila ya mpango).

Hila ni muda muafaka sasa wa serikali kupeleka elimu ya uraia vijijini, maana kuna watu wamezoea tamaduni za kumiliki au kutumia resources bila ya kujua sheria za nchi zikoje kwakuwa sehemu zilikuwa zimesahaulika au hazikuwa na sababu ya serikali kuzuia.

Nachokubaliana na wewe ni kwamba serikali pia lazima itenge makazi na kugawa kwa wanavijiji as part of permanent settlement kabla haya madhara hayajazidi, baadae na wanavijiji waanze kujifunza utamaduni wa kuelewa kwamba sisi wa mjini kujenga mpaka tununue viwanja kutoka kwa wamiliki binafsi au kupitia serikali za mtaa, utaratibu wa sheria ndio huo hata vijijini.
 
hata hao wana kijiji wanapewa maeneo ya kuishi na serikali za vijiji husika, hati ya kumiliki maeneo yao. hizo hati zinapatikana halimashauri ya wilaya. mara nyingine kila kijiji inapewa mipaka. sasa swala linakuja watu mnaambiwa hayo hayatambuliki. ndo maana kwenye hoja yangu nimesema wamekua wakihudumiwa na serikali halali ya vijiji kata na hata tarafa na wilaya. ishu imekuja pale maliasili wao wanakomaa kwamba wanatoa notice ya kuhama hawatambui chochote na hawahitaji mjadala.
 
Nadhani hilo ni swala la mahakama, maana ya hati ni nini sasa kama aieshimiki na taratibu za sheria za umiliki zimefuatwa. Watu hawawezi kujiwekea mipaka mipya bila ya kujua utaratibu wa kuwatoa wenye vibali utafanyikaje na fidia inapatikana vipi (hata mimi mshale ningerusha, that is immoral).
 
ha ha ha nikweli rafiki yangu... sasa mwekezaji ameshapatikana na hela yake imeshaliwa ni dhahiri wananchi ndo watashindwa kwani serikali itatumia kila njia kuwakandamiza ili adhama yake ipite.
 
Well kama serikali itaendelea na utaratibu huo, nadhani yaliyotokea Singida majuzi wayategemee kila mahala maana naona na Mbeya kuna kesi kama hii.

Ndio maana kuna umuhimu sana wakuwa na utaratibu wa kuwa na sehemu tatu za checks ambazo azi ingiliani na mara nyingi upande wa serikali (watendaji) wamekuwa wakijiamulia bila wahusika kuadhibiwa na mahakama zipo na ushahidi hupo.

Poleni.
 
Ahsante kwa pole ndugu yangu... labda katiba mpya inaweza kutoa mwafaka wa migogoro zugu kama haya. watu kada Fulani mfano wafugaji, wakulima, wawekezaji wa kigeni wakibainishiwa haki na maeneo yao ya kudumu nafikiri ndo tutaishi bila mizuguano ya mara kwa mara.
 
Katiba (kama sheria mama pekee) sidhani kama itakua suluhisho la kudumu, tatizo la msingi lipo kwenye missing link kwenye utaratibu wa kutunga sheria au sera kwasasa na implemention zake. Kuna sehemu nne muhimu zinapwaya
1.....Ufahamuji wa sheria kwa wananchi and their binding obligations (hili swala watunga sera lazima wajue, huko vijijini somo la nguvu linatakiwa kupelekwa).

2.....Consistence, watu hawawezi kurekebisha rekebisha mipaka kila kukicha, lazima watenge sehemu za kutosha kwa wananchi hata kama bado hawajifika hili kuwe na sehemu za kutoa jinsi idadi inavyoongezeka na lazima kuwe na zones ambazo za misitu/akina simba na wawekezaji. Sio utaratibu wa sasa mwekezaji anakuja inabidi wanakijiji wampishe au watu kesho wanaamka jamani pale tufanye hifadhi ya taifa hilo ndio linaleta matatizo ya sehemu ya 3.

3.....Uwezekanaji wa sheria kueshimiwa, kama nilivyosema sehemu ya pili sasa wewe watu wameshajenga makazi miaka arobaini leo unasema sehemu ya msitu. Obviously ukuzingatia hayo kwenye sehemu ya pili wakati wa utungaji wako wa sera/sheria ndio maana leo watu wenye haki miliki unataka kuwaletea ubabe. Halafu jamaa wakileta ubishi uwapige useme wavamiaji haramu, that is unacceptable.

4.....Sheria/sera inalindwa vipi na nani, na hili ndio tatizo kubwa sana kwa sasa hawa madiwani, viongozi wa serikali za vijiji na wilaya. Wanahusika sana kwenye kugawa ardhi mara mbili au kutoa ardhi kwa wawekezaji ambayo ina overlap mpaka kwenye mipaka ya kijiji na hili ndio linachangia sana serikali kuu kujikuta inapokea lawama, sasa kama waziri anakwambia na yeye mpaka arudi kwa raisi na mahakama zipo. Hizo sheria zipo kwanini kama wavunjaji wakuu can not face the consequences of breaking them or causing social misunderstanding.

Siasa zetu bado, asubuhi njema, me out for now.
 
thank you for your school... I get u clearly ma friend... ngoja tusubiri nini kitatokea baada ya muda maana hawa wenye nchi lazima watatumia nguvu kuwaondoa hawa wananchi wakiwaita wavamizi.
 
mleta mada asome sheria no 5 ya vijiji ya mwaka 1999 na kama kijiji kilianzishwa kwenye eneo la misitu kijiji hicho ni batili kwani itaonekana ni wavamizi wa maeneo ni kupe mfano mdogo huko Serengeti kuna eneo kijiji cha Kenyana kitongoji cha mochuri mwaka 1991 kuna mzungu alipewa ardhi hekta 2030 na kumilikishwa kwa muda wa miaka 99 bahati mbaya mzungu huyo alifariki na kuacha mitambo yake huko , baadhi ya wananchi mwaka 2000 wamevamia eneo hilo na sasa wamejenga shule kwenye eneo hilo. Je mwenye eneo akijitokeza si yatatokea malalamiko kama hayo ya kwenu hebu tujaribu kufuaata taaratibu na sheria ya nchi hii
 
Back
Top Bottom