Nakumbuka miaka ya 1990 nikiwa ndio naingia Dar baada ya kupata kazi shirika moja kubwa hapa mjini. Nilikuwa nimepanga vyumba vitatu pale Magomeni Kagera. Katika nyumba hiyo kuna vyumba sita, mimi nilichukua vitatu upande mmoja na nilikuwa Bachelor, mkabala na mimi kuna jamaa nilimkuta alichukua vyumba viwili na alikuwa anakaa na dada mmoja pamoja na mtoto wao mmoja na chumba kingine alikaa mzee mmoja (sasa ni marehemu). Mimi nilikuwa na pikipiki ya Ofisi zile Honda 110. Nilikuwa nimezoeana sana na wapangaji wote hadi wa vyumba vya uani, utani kama kawa.
Nyumba yetu haikuwa na maji hivyo ilibidi kuchota maji bomba la jarani. Siku moja nilikuwa nimetoka job, nikaenda kuchota maji ili nioge ghafla akatokea jamaa yangu tuliyesoma naye (sasa ni marehemu) alikuwa anafanya kazi tume ya Jiji (siku hizi Manispaa), akaniambia pikipiki nzimaa, nikamawambia ndio akasema unaenda wapi mbona una bukta? nikamjibu naenda kuoga, akasema usioge kwanza nikimbize Mwananyamala, kuna hela ya mgao jamaa anayo na nikumwachia mpaka kesho sinta ipata tena, tumuwahi yuko Bar fulani kule anakunywa kama hana akili nzuri, tumuwahi tupate hela ya kutesa weekend yote. Nika ahirisha kuoga nikavaa Trucksuit tukaondoka. Wakati huo ndoo ya maji ya kuoga niliacha uani karibu na bafu.
Kumbe huku nyuma yule demu wa jirani yangu alirudi toka matembezi yake akataka kuoga, akaangalia kwenye corridor tulipokuwa tunaweka ndoo zetu yangu hakuiona ili aazime akatumie, hata hivyo akaamua kwenda uani msalani, kufika akakuta ile ndoo yangu ina maji karibu na bafu, alipouliza akaambiwa ni mimi ndie nimeweka hayo maji hapo, akaulizia nilipo akaambiwa katoka na rafiki yake mmoja, akaamua kuchukua yale maji akaoga ili akimaliza akateke mengine aniwekee palepale nikija niendelee.
Baada ya kuoga akaenda kuvaa sasa kabla hajateka maji mengine, bwana wake akarudi, katika pilikapilika za kumpokea mzee, akasahau kwennda kuteka maji na akaanza kupika, ghafla akasikia pikipiki ninarudi, bila kumuaga bwana wake akatoka nduki akaenda akateka maji akaweka pale karibu na bafu, kumbe mzee anacheki picha yote. Mimi bila kujua nilifika na kwenda moja kwa moja kuoga nimuwahi jamaa pale bar nilikomshusha Lango la jiji, nikavaa na kuondoka, huku nyuma kimbembe kilianza Bwanake akamwambia kumbe siku hizi jamaa unamchotea maji ya kuoga na unajua ratiba yake ya saa ya kurudi. Ugomvi ukawa mkubwa ila mimi na jamaa wengine hatukujua kinachoendelea, hadi baada ya miezi minne.
Siku hiyo nilikuwa pale Lango la Jiji na jamaa yangu mwingine tunanyonya Konyagi, nikamwona shemeji anapita ghafla aliponiona akasema shemeji tuko ngomani hapo mtaa wa Ifunda ninunulie kinywaji na mdogo wangu huyu, nikawaagizia stella mbilimbili, hamadi Bwanake huyu akaanza kufoka nilijua tu mko pamoja ndio maana umetoroka ngomani na hata siku ile nilipokufuma unamchotea maji ya kuoga ulibisha lakini ilikuwa ni kweli huyu ni Bwanaako, Bwanaee niliamua kuvunja Ujirani na Usheji pale pale.
Kurudi home kesho yake nikamuuliza mama mmmoja ambae ni mpangaji humo ndani, akasema unakumbuka siku moja uliweka maji ya kuoga ukaondoka? nikamjibu naam, basi Mama Doto (sio jina lake) aliyaoga na akarudisha aliposikia pikipiki inakuja na mumwe alimuona songombingo kati yao lilianzia hapo ila wewe hakuwahi kukuuliza. Kwa kifupi ni hayo ingawa yalltokea mengine makubwa zaidi ambayo yalisababisha wao kuachana ila sio kwangu ni kwa rafiki yake mkubwa huyo jamaa kwani mimi nilishajiweka mbali nao.