Yaliyonikuta Leo

NATA

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2007
Posts
4,492
Reaction score
1,313
Nikiwa naendesha kariakoo kaja mwanaume wa makamo hivi namuona makusudi anajigongesha kwenye kioo cha gari cha pembeni.

Mie nikasimama mara anadai nimpeleke hospital kaumia nikamwambia umeumia wapi na gari haikuwa kasi sanasana umegusa kioo .
Kashupaa nimpeleke hospital au nimpe pesa akatibiwe.

Nikampa 10,000.00 ili yaishe bwana wee nimeenda kupaki nazunguka kariakoo na kutana naye anadunda swafi kabisa!

Jamani hali ya uchumi hii itatupeleka pabaya mtu mzima kama yeye nimesikitika sana.
so ukiwa kariakoo uwe mwangalifu sana.
Watu wanabuni njia mbalimbali za kujipatia pesa kiurahisi.
 
hahaha pole mkuu. Kuna signature ya mdau flani ni one of my Fev inasema hivi "MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO" uwezo wa kubuni njia za kutuingizia kipato ni mdogo sana....
 
Duhhhhh
Pole sana
Laakini ulifanya la maana sana...
Tenda wema lakini papo hapo
Usizidi uwezo.
 
hahaha pole mkuu .... Kuna signature ya mdau flani ni one of my Fev inasema hivi "MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO" uwezo wa kubuni njia za kutuingizia kipato ni mdogo sana....
Ni ya mkulima mmojaanaitwa Nyani Ngabu
 
Hahahaha...,pole!Hesabu kama sadaka tu!!
 
Haaaaaaa!!!! Jamani tunaelekea wapi!! Pole sana rafiki yangu hiyo ndo bongo ye2.
 
...ehhh, ndio yamekuwa hayo siku hizi? ama njaa ni wendawazimu! Tshs 10,000/= nyingi...! Kwa mtaji huo utakuta mtu ndio ajira yake hiyo, udhalimu tu. Ungemkomalia na kumtishia mpaka polisi waje, lakini Mob Justice za Bongo aaarrggghh!
 
una bahat hajajifanya kafa!

Hapa ningetoa zaidi maana polisi wangeingilia kati na raia wema wangegawana gari langu vipande vipande na kuvipeleka mtaa wa lindi.
Na ratiba yangu ya kariakoo ingeishia pale.

Nashukuru sana yu mzima!
 
...ehhh, ndio yamekuwa hayo siku hizi? ama njaa ni wendawazimu! Tshs 10,000/= nyingi...!
Kwa mtaji huo utakuta mtu ndio ajira yake hiyo, udhalimu tu!....
Ungemkomalia na kumtishia mpaka polisi waje, lakini Mob Justice za Bongo aaarrggghh!

Kwanza niliingiwa na woga sikutaka kubishana naye sana kwani watu walishaanza kunizunguka
Huwezi jua inawezekana wana kundi lao.
Mtu mwenye njaa wakuu si wakucheza naye yuko tayari kufanya chochote.
 
kweli maisha magumu...lakini si ni bora angeomba?
pole mkuu
 
Duh pole sana,haya matapeli siyapendi yanarudisha maendeleo nyuma.
 
Hapa ningetoa zaidi maana polisi wangeingilia kati na raia wema wangegawana gari langu vipande vipande na kuvipeleka mtaa wa lindi.Na ratiba yangu ya kariakoo ingeishia pale.Nashukuru sana yu mzima!
Mi ningemshukia na bonge la panga' kudadeki angenitambua.
 
Hiyo ni sadaka/malipo?Usingempa ingekuaje kama ndio kumfidia hayo maumivu yake?
 
Haha!! Mbona hii tayari ilishaigizwa na ze comedi? Next time nafikiri akishakukomalia umpeleke hospitali unampakia kwenye gari halafu unampeleka polisi.

Ilimradi unauhakika kwamba amejigongesha mwenyewe na hajaumia. Mimi ilinitokea Tandika, jamaa akajigongesha kwenye side mirror na akajifanya ameanguka.

Halafu jamaa wengine wakaanza kuja mbele ya gari ili kunizuia nisiondoke, nilichofanya ni kukanyaga mafuta wenyewe wakanipisha barabarani.
 
Pole sana,hawa kina joti kwa upande mwengine wanatufundisha kuwa yapo nayatendeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…