`Yaliyomkuta Ngeleja iwe mwanzo na mwisho,kumbuka cheo ni dhamana Mh Steven Maselle | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

`Yaliyomkuta Ngeleja iwe mwanzo na mwisho,kumbuka cheo ni dhamana Mh Steven Maselle

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, May 5, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Chonde chonde mh.Maselle,wadhifa ulioupata kama kijana toka kwenye mikoba iliyoachwa na vijana wenzako ni changamoto kubwa sana katika zama hizi za ufisadi uliotamalaki.Nakumbuka mh.Shibuda aliwahi kumsihi sana Ngeleja alipoteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo ulioynayo,naomba ule ushauri aliopewa Ngeleja nawe hufanyie kazi ili kulinda heshima ya vijana nchini.Kuanguka kwako ni anguko la vijana kwasababu vijana ndo tunaoamini kuwa chachu ya mabadiliko popote pale duniani.Cheo nidhamana,jaribu kurudia ahadi za TANU hatakama ahadi hizo zilikwenda na mwalimu JK Nyerere.
   
 2. P

  Pilitoni JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 1,001
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Mbona unaongelea mawazi wasukuma tu?ktk baraza,kijana ni masele tu?hapa kuna harufu ya ukabila na chuki dhidi ya wasukuma na huu ni ujinga ambao haukubalik. Ukiwa na akili iliyochanganyikana na makamasi aghalabu utashikia bango mambo ya kijinga kama haya.Kama kila kabila litadai liwe na mawaziri wengi tz hatufiki na watu wa aina ya kwako ndio mtakaoipeleka tz iwe kama Rwanda 1994,angalia sana.
   
 3. b

  bmosses Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabla ya yote na declare interest,mh. Maselle ni mbunge wa jimbo langu,pili nimezungumzia vijana na si kabila.Labda cha msingi kwa kukusaidia kwa faida yako,jaribu kusoma kwa kina na kutafakari kabla ya kuandika ili mradi uonekane umeandika.Ukabila unaojaribu kuuleta ulikwisha malizwa toka zama za ujima.Tatu si busara kusoma thread za humu ndani kama umelewa,hapa si FB!
   
 4. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza,mh. Maselle ni mbunge wa kitaifa pia ni naibu waziri katika nchi yetu,kinyume kabisa na fikra zako kuwa huu ni utawala wa kichifu.Lazima apambane na changamoto ambazo ndizo zilizo wadondosha waliomtangulia.Hapa hatupiki majungu hapa ni think tank ndo maana vichwa panzi hawana nafasi ndani ya JF.Pia kilichozungumzwa si ukabila,ikitokea watu kama wewe mnazungumzia ukabila katika karne hii ni lazima tuwaogope kama ukoma.
   
Loading...