Yaliyojiri Uwanja wa Taifa: Yanga FC 2 - 1 Mbeya City

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Match loaalding
Yanga fc vs Mbeya City
Uwanja:Mkapa Stadium
Time:10:00pm
Joto:25c
Humidity:normal
Rainfall:no,70%
Nakuletea updates LiVe
Kiingilio:
Mabanda umiza: 500Tsh
Bar:Soda au any drinks
Kikosi cha 1
1. Beno David
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Nadir Ally
5. Vicent Bossou
6. Thabani kamusoko
7. Saimon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Obrey Chirwa
10. Donald Ngoma
11. Geoffrey Mwashuiya
Kikosi cha akiba.
Deogratius Munishi, Vicent Andrew, Hassan kessy, Oscar Joshua, Said Makapu, Emmanuel martin, Juma mahadhi, Matheo Anthony, Amiss Tambwe na Malimi Busungu..
Head Coach : GEORGE LWANDAMINA
Assistant Coach : JUMA MWAMBUS

Kikosi Cha Mbeya City kitakachoanza leo dhidi ya Yanga Sc SAA 10:00

KIKOSI KAMILI
Owen Chaima
Haruna Shante
Hassan Mwasapile
Tumba Lui
Sankani Mkandawile
Ditramu Nchimbi
Majaliwa Shabani
Kanny Ally (C)
Zahoro Pazi
Raphael Daudi
Rajabu Isihaka

KIKOSI CHA AKIBA
Fikirini
Kabanda
Ngassa
Bryson
Omarry
Danny
Elyud

=====

UPDATES:

Yanga 1-0 Mbeya City | GOAL amefunga Simon Msuva 7' (YANGA)

Dakika ya 57: Haruna Shamte anaisawazishia Mbeya City bao, anafunga baada ya walinzi wa Yanga kuachwa kisha kupata mpira akiwa yeye na kipa, akapiga shuti likajaa wavuni na kufanya matokeo kuwa
Yanga 1-1Mbeya C

Dakika ya 64: Baada ya kazi nzuri iliyosababisha kona, Chirwa anaipatia Yanga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.

Yanga 2 - 1 Mbeya

Yanga (Simon Msuva 7', Obrey Chirwa 64') 2-1 (Haruna Shamte 57') Mbeya City

FULL TIME

=======

Dakika ya 94: Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga wanaibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Dakika ya 92: Mchezo unaendelea huku kukiwa na presha kubwa kwa pande zote.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.

Dakika ya 89: Mbeya City wanaendelea kutengeneza mashambulizi lakini Yanga wapo makini.

Dakika ya 88: Ngassa anamiliki mpira lakini anashindwa kuwatoka mabeki wa Mbeya City.

Dakika ya 85: Bossou anautoa mpira inakuwa kona. Inapigwa inaokolewa.

Dakika ya 82: Yanga wanapata faulo karibu na kona, inapigwa inaokolewa

Dakika ya 80: Mchezo unaendelea, Mbeya City wanapata kona, inapigwa Yanga wanaokoa.

Dakika ya 79: Raphael Daudi anapatra nafasi akibaki yeye na kipa baada ya kuwatoka walinzi wa Yanga, anapiga shuti linazuiliwa na Beno, inakuwa kona.

Dakika ya 76: Mchezo umesimama kwa muda, Chirwa yupo chini anapatiwa matibabu, aliumia baada ya kugongana na mchezaji wa Mbeya City.

Dakika ya 75: Kasi ya mchezo imeongezeka timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 73: Mbeya City wanapata faulo nje kidogo ya eneo la 18 la Yanga, Haruna Shamte anapiga mpira unapita juu ya lango.

Dakika ya 71: Tambwe anapiga kichwa kizuri, mpira unagonga nguzo ya juu ya lango la Mbeya City na kurejea uwanjani, beki wa Mbeya City anaokoa.

Dakika ya 68: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Nadir Haroub 'Cnnavaro' anaingia Kelvin Yondani.

Dakika 67: Kuna vurugu zinatokea kwenye moja ya jukwaa, mashabiki wanapigana, haijajulikana sababu, ila mchezo unaendelea.

Baada ya kazi nzuri iliyosababisha kona, Chirwa anaipatia Yanga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.

Chirwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 64: Chirwa anaingia na moira, anawatoka walinzi wawili lakini wa tatu anautoa nje moira inakuwa kona.

Dakika ya 62: Mchezo umechangamka, Mbeya City wanafika langoni kwa Yanga, Yanga nao wameamka. Ngassa anatoa pasi nzuri lakini mpira unatoka.

Dakika ya 60: Mbeya City wanafanya mabadiliko, Rajab Isihaka anatoka, anaingia Mrisho Ngassa.

Dakika ya 57: Haruna Shamte anaisawazishia Mbeya City bao, anafunga baada ya walinzi wa Yanga kuachwa kisha kupata mpira akiwa yeye na kipa, akapiga shuti likajaa wavuni na kufanya matokeo kuwa 1-1.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 54: Kessy anatoka nje, nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martine. Mashabiki wao wa Yanga wanapiga kelele za kushangilia mabadiliko hayo.

Dakika ya 51: Kessy anafika katika lango la Mbeya City lakini anashindwa kuitumia nafasi anayopata, kipa anauwahi mpira anadaka.

Dakika ya 50: Mwashiuya anaingia na mpira kwa kasi lakini anamsukuma beki wa Mbeya City inakuwa faulo kuelekea kwa Yanga.

Dakika ya 48: Niyonzima anapiga krosi nzuri, Tambwe anapiga kichwa kinapaa juu ya lango

Dakika ya : 46: Yanga wanafika langoni mwa Mbeya City lakini Tambwe anacheza faulo.

Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia uwanjani kutoka vyumbani.


MAPUMZIKO

Dakika ya 48: Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza. Timu zote zinaingia vyumbani kupumzika, Yanga inaongoza kwa bao 1-0.

Dakika ya 46: Yanga wanapata kona. Inapigwa na Mwashiuya inatolewa inakuwa kona tena, inapigwa lakini kipa anadaka.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 43: Mwashiuya anapiga shuti lakini linakuwa na nguvu ndogo linadakwa

Dakika ya 42: Yanga wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Mbeya City baada ya Amiss Tambwe kuchezewa vibaya.

Dakika ya 41: Zahoro Pazi anagongana na Bossou ndani ya eneo la 18 la Yanga, Pazi analalamika kuwa amechezewa vibaya.

Dakika ya 40: Kessy anapiga krosi lakini beki anazuia mpira unatoka inakuwa kona.

Dakika ya 38: Haruna Niyonzima anampa pasi Juma Abdul katikati ya uwanja lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 36: Kessy amejaribu mara kadhaa kupiga krosi lakini imeshindikana na mpira kutoka.

Dakika ya 35: Mwamuzi Andrew Shamba anazungumza na wachezaji wa Mbeya City, mchezo unaendelea.

Dakika ya 34: Yanga wanafanya shambulizi la kushtukiza, Kessy anakimbia na mpira unaingia lakini unatoka nje.

Dakika ya 30: Inapigwa kona lakini Yanga wanatoa tena inakuwa kona. Inapigwa Beno anaupangua mpira na kuelekea katikati ya uwanja.

Dakika ya 29: Yanga wanashambuliwa, Kessy anaupiga mpira unatoka nje inakuwa kona.

Dakika ya 28: Mbeya City wanapata kona, wanapiga lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 27: Mbeya City sasa wanajipanga na kutengeneza mipango ya kushambulia.

Dakika ya 25: Mbeya City wamefika langoni kwa Yanga mara mbili na kufanya mashambulizi lakini wameshindwa kutumia nafasi walizopata baada ya kipa Beno kufanya kazi nzuri.

Dakika ya 20: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.


Dakika ya 16: Kwa mara nyingine Yanga wanapata kona, wanapiga kipa anudaka mpira

Dakika ya 15: Yanga wanapata kona, anapiga Mwashiuya, mabeki wa Mbaya City wanaokoa.

Dakika ya 10: Msuva anashindwa kurejea uwanjani kutokana na kuumia kichwani, nafasi yake inachukuliwa na Juma Abdul

Wakati Msuva amevunga bao aligongana kichwani na beki wa Mbeya City, ameshindwa kushangilia, watu wa huduma ya kwanza wameingia kumchukua na kumtoa nje, bado anapatiwa matibabu

Dakika ya 8: Yanga wanapata bao la kwanza, krosi nzuri ya Hassana Kessy inatua kichwani mwa Msuva ambaye anapiga kichwa na kufunga.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!! MSUVAAAAAAAA

Dakika ya 6: Mchezo umeanza kwa kasi na inavyoonekana timu zote zinataka kupata bao la mapema, Yanga ndiyo ambao wamemiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 4: Yanga wanafanya shambulizi kali, Niyonzima anaingia na mpira anapiga krosi lakini inakosa mtu wa kumalizia, mpira unatoka nje

Dakika ya 2: Yanga nao wanajibu mapigo kwa kufika langoni mwa Mbeya City baada ya mabeki wa Mbeya kujichanganya lakini mapira unatoka inakuwa kona.

Dakika ya 1: Mbeya City wanafika langoni mwa Yanga lakini kipa wa Yanga anauwahi mpira.

Mwamuzi anaanzisha mchezo:

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa.

Mpira umeisha Yanga fc wanajianda kuchukua Kombe kwa .Mara ya Tatu jumanne mbele ya wadogo zao Toto Afrika
Simba wao bado wanaandika barua ya kwenda FiFa kudai point Tatu
 
sawa mkuu..unaweza kuweka msimamo wa top 4 hapa
Huo
126d86eaad8cb9e345facafe60d2cfad.jpg
 
Bila shaka umeweka mbeya city 2 sasa mimi nakubaliana na wewe kuwa mbeya city 2 yanga 4.
 
Match loaalding
Yanga fc vs Mbeya City
Uwanja:Mkapa Stadium
Time:10:00pm
Joto:25c
Humidity:normal
Rainfall:no,70%
Nakuletea updates LiVe
Kiingilio:
Mabanda umiza: 500Tsh
Bar:Soda au any drinks
Kikosi cha 1
1. Beno David
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Nadir Ally
5. Vicent Bossou
6. Thabani kamusoko
7. Saimon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Obrey Chirwa
10. Donald Ngoma
11. Geoffrey Mwashuiya
Kikosi cha akiba.
Deogratius Munishi, Vicent Andrew, Hassan kessy, Oscar Joshua, Said Makapu, Emmanuel martin, Juma mahadhi, Matheo Anthony, Amiss Tambwe na Malimi Busungu..
Head Coach : GEORGE LWANDAMINA
Assistant Coach : JUMA MWAMBUS
Mkuu mbona umetaja kikosi kimoja tu hujataja kikosi cha mbeya city
 
Tuko pamoja naona timu ndio zinaingia uwanjani, Yanga mbele daima nyuma mwiko....

Najua leo wachawi wapo wengi lakini ndio hivyo tutapambana
 
Back
Top Bottom