Yaliyojiri katika Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM Songea Mkoani Mkoani Ruvuma

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Shirika la utangazaji nchini TBC itarusha live maadhimisho ya miaka 38 ya chama cha mapinduzi ccm yatakayofanyika mkoani Ruvuma kesho February mosi.

==============

Updates:

attachment.php
attachment.php

Rais Kikwete akionesha alama ya Jembe na Nyundo

- TBC1 pamoja na Startv wanaonesha mojakwa moja maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM.

- Sasa hivi vijana wa halaiki ndo wanaonyesha ukakamavu wao.

- Sherehe zinaonyeshwa moja kwa moja kutoka uwanja wa Majimaji Songea.

- Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine wa juu wa CCM wapo uwanjani tayari, wakiwemo Katibu muenezi wa CCM Nape Nnauye , Makamu M/kiti wa CCM Philip Mangula, Waziri Mkuu Mhe. Pinda, Katibu Mkuu wa CCM Abdularahman Kinana, na wengineo wengi.

- Muda huu wimbo wa Taifa unaimbwa na kikundi maalum cha vijana wa umri chini ya miaka 18 huku ukisindikizwa na wageni wote waliopo uwanjani
.
attachment.php

- Kikosi maalum cha Halaiki-Makomandoo wenye umri mdogo, kikiwa kimebeba silaha za SMG kinapita mbele ya Mwenyekiti wa CCM, kumuonesha umahiri wao.

- Baada ya maonyesho hayo ya 'Makomandoo', hivi sasa ni zamu ya Brass Band kutoka Zanzibar kutoa burudani ya kwaya fupi.

- Wakati huu, Katibu wa CCM, Mkoa wa Ruvuma, anakaribishwa kutoa hotuba fupi ya ukaribisho. Na anamkaribisha Mhe. Nape Nnauye atoe utambulisho wa viongozi mbalimbali waliopo uwanjani pamoja na wageni.

- Nape anasema kutokana na ufinyu wa muda, atatoa utambulisho wa wageni kutoka Uganda huku akisema wengine wote wanafahamika. Ila kwa sasa anamkaribisha Mbunge wa Ruvuma, Mhe. Emmanuel Nchimbi; ambaye kwenye hafla hii, ndiye Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi.

Anatoa hotuba;

Emmanuel Nchimbi: Ndugu Mwenyekiti, uliagiza ujenzi wa barabara ya Manispaa, bado haujatekelezwa, pia uliagiza wakulima wadogo wadogo wapewe kipaumbele kisha mawakala na ulitoa pesa takribani bilioni 7.7, tunakushukuru sana.

Mhe Rais, Wananchi wa Songea wanapenda sana mpira, na wana timu yao ya majimaji, nimepata mdau kutoka marekani aliyetuchangia Milioni 150, hivyo kwako rais hatutaki chochote zaidi ya Dua tu. (makofi).

- Mhe. Nchimbi amemaliza kuzungumza.

- Na sasa anakaribishwa M/kiti wa CCM mkoa wa Ruvuma kuzungumza;

M/kiti (CCM - Ruvuma): Tunakushukuru Mheshimiwa JK, kwa kutuletea sherehe hizi Ruvuma, wananchi wa Ruvuma wanawakaribisha sana.

CCM inajivunia wingi wa wanachama laki 257 456. Hakuna mbunge wa upinzani mkoa wa Ruvuma.

Tunakuhakikishia sisi wanaCCM na wananchi kwa umoja wetu CCM itashinda kwenye uchaguzi mkuu 2015. Kwa ushahidi, tumeshinda kwa asilimia zaidi ya 90 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa huku!

- Anaendelea kutoa takwimu za shughuli za maendeleo zilizofanywa na serikali ya CCM katika mkoa wa Ruvuma.

- Anamalizia kwa kumtakia Rais mwisho mwema wa uongozi wake utakapofika (Makofi kwa wingi)!

- Naam, Ndugu Kapteni Komba anaitwa kutumbuiza kidogo ili kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Ndg Jakaya Kikwete kuzungumza, Kisha baada ya hapo, atafuatia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutoa burudani.

- Komba amemaliza kutumbuiza, na sasa Katibu mkuu wa CCM, Ndugu Kinana anaitwa kumkaribisha M/kiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete.

Kinana: CCM oyeee! Nani kama CCM? Nani kama Kikwete?

Ndg, M/Kiti kabla sijakukaribisha, nachukua nafasi hii kuwashukuru wana-Ruvuma kwa maandalizi, na kuwakaribisha wageni kutoka chama cha National Resistance Movement (NRM) kutoka Uganda.

- Katibu mkuu NRM, Jestine Lumumba anatoa neno la shukrani. (Anashangiliwa).

- Sasa Kinana anawatambulisha zaidi wajumbe kutoka Uganda, Rose Nyamayanja, John kiangi na wengineo.

- Katibu wa CCM, sasa anamkaribisha makamu M/kiti wa chama cha NRM kusema machache.

Makamu M/kiti wa NRM: CCM oyee, CCM itaendelea kutawala (Makofi na vifijo kwa wingi).. Tunafurahi sana kuwepo ndani ya nchi ya Tanzania. Vijana mpo? CCM juu..

M/kiti, sisi tumetoka Uganda kuungana na CCM kama NRM tuko mutu moja (pamoja). Ndugu M/kiti, mnamo miaka ya 1970's, Nyerere alisema kwamba 'Watanzania, adui imetuingilia, na sisi watanzania, hatuna chochote cha kufanya, kilichobaki ni kumpiga nyoka. Sababu tunayo, uwezo tunao na nia ya kumpiga nyoka tunayo''.

Nataka kusema kwamba, siku hiyo ndiyo sisi tuliamua kuungana na Tanzania. Tunakumbuka ukombozi wa Uganda. Leo tumesimama imara kama nchi na Tanzania imetusaidia sana.

Rais Museven na familia yake ilikuwa Tanzania, mfumo wa uongozi tumekopi Tanzania, ukombozi wa South Afrika, Zimbabwe, Angola, Namibia ulianzia Tanzania.

Tunakumbuka sana, mzigo Tanzania ilioubeba ilitokea ndani ya chama cha CCM.

Mwisho, muungano wa Afrika Mashariki ulianzia hapa Tanzania. Niseme kwamba, Muungano wa A/Mashariki udumu! Tutahakikisha nchi zote za A/Mashiriki tutakuwa nchi moja. Nasema asante sana Tanzania, Hongera CCM kuongoza miaka 38.

Mungu Ibariki Tanzania. Tuko pamoja. Rais Kikwete Juu, Rais Museven juu.. (Makofii).

- Amemaliza!

- Na sasa, M/kiti anajongea kuanza kutoa hotuba (anashangiliwa sana).

JK: Mheshimiwa Makamu m/kiti wa CCM Philip Mangula, M/kiti wa NRM. Huyu ni rafiki yangu mkubwa, ni rubani pia. Alishawahi kunisafirisha na ndege akiwa kama rubani.

- Sasa anashukuru wahusika wote na waheshimiwa mbalimbali .

- Anammwagia sifa Mhe. Nchimbi kwa maandalizi mazuri na kuwashukuru viongozi mbalimbali wa CCM kwa kazi nzuri, akiwemo Katibu mkuu, AbdulRahman Kinana.

JK: Nchi yetu imepiga hatua, kuna amani, utulivu na maendeleo yanayoonekana. CCM imeendelea kuaminiwa katika awamu zote. Hata mwaka huu itakuwa hivyo hivyo. Nalisema hil bila wasiwasi kabisa, roho baridiiiii.

Dalili ya mvua ni mawingu, ushindi tulioupata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Oktoba 2014 ni ushahidi tosha, ndugu zetu wapinzani hawana chao.

Tusikate tamaa, tunaweza kuwa na changamoto nyingi mwaka huu, ila tunapaswa kuwa na ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Lazima tuhakikishe tuwe wamoja. Umoja ni ushindi.

- Anaendelea..

JK: Komba nakushukuru sana kwa wimbo mzuri, huishiwi nyimbo (vichekooo).

Huu ni mwaka ambao tunapaswa kuwa na rasilimali za kutosha kuweza kuwapatia ushindi wagombea wetu, ni mwaka wa kuhakikisha tunafanikisha kwa kiwango kikubwa.

Nafurahishwa na wale waliofanya kazi kubwa. Nawapongeza sana!

Nasikitishwa na viongozi wetu ambao hawajafanya kazi ipasavyo, hawa wanavunja moyo, wanazorotesha chama chetu. Kuna msemo unasema ''Jasho jingi wakati wa amani, damu kidogo wakati wa vita''.

Maana yake maandalizi yakiwa ya kutosha, kazi inakuwa rahisi, kinyume chake unapunguza nguvu ya ushindi. Naomba kila mmoja ajipime yupo fungu gani.

JK: Kila wilaya na mkoa kiwe na mfuko wa uchaguzi, na wakati ndio huu mfuko unatakiwa kufanya kazi. Sina budi kuwatahadharisha, msichukue fedha ambazo zitaleta matatizo!

JK: Lazima tujiandae kama chama na kuwa na nyenzo zote kwa ajili ya kukiwezesha chama na wagombea wetu kushinda.

Katika jitihada za kutafuta pesa za
kutunisha mifuko ya uchaguzi, Msichukue tu kila pesa, nyingine moto. Mi ushauri wangu ni huo tu!

Huu ni mwaka wa kutambua ahadi, zipi zimetimizwa na zipi bado. zipo ahadi za rais na za chama kuanzia mkoa, wilaya na kata. Mwaka wa kuulizwa ndio huu!

Waswahili husema, ''mla kunde husahau, mtupa maganda hasahau''. Kwahiyo watupiwa maganda hawajasahau. Lazima tuwe makini.

JK: Sio tukiulizwa, tuanze kuwanyooshea vidole na ni kuwaita wapinzani. Kwahiyo nasisitiza kila mmoja akumbuke ahadi zake. Mimi nayakumbuka maana naandika, na wasaidizi wangu hunisaidia kunikumbusha, ila kusema kweli mengi tumetekeleza sana. Japo yapo machache bado.

Huu ni mwaka wa kuulizwa, si vizuri tuumalize mwaka huu huku tunaenda na madeni lukuki ya ahadi. Kushinda tutashinda, ila yatatupunguzia. Huu ni mwaka wa kuongeza jeshi letu la ushindi, nalo ni wanachama wapya.

JK: Jambo lingine kubwa na la muhimu ni kuwatembelea wanachama na wananchi kuzungumza nao. Jambo hili huwa hatulifanyi vizuri sana. Kila nikipata taarifa, nna watu wengi wa kunipa taarifa, wengine hamuwajui nawajua mie.

Wananiambia, 'Chama chako hakifanyi mikutano mingi kama wapinzani'. Japo ukiwauliza watajitetea. Ndugu zangu, hili ni jambo kubwa, huwezi kupata ushindi kwa watu wasio kujua.

JK: Tuache kukaa ofisini, tutoke tuwashawishi watu wajiunge na ccm. Kila ofisi ya mkoa na wilaya inayo gari. La kuwawezesha kufanya kazi hiyo lakini hamtembei. Tulipokuwa hatujawapa magari, ajenda ilikuwa ni magari. Mpaka mzee Mkapa akawa anakasirika. Sasa tumewapa hayatumiwi inavyotakiwa.

Jambo la msingi ni kuwapata wapiga kura ili tushinde. Chama chetu kama vilivyo vyama vingine kinapaswa kuhimiza wananchi wajitokeze kwa wingi kujitokeza kupiga kura.

Asiyekuwa na kadi mpya ya kupiga kura, hatoruhusiwa kupiga kura, unaanza utaratibu mpya wa BVR, kadi za zamani hazitotumika.

Tume ikitangaza, nenda, usije ukasema unacho chako, we nenda kwa kuwa hicho cha zamani hakitotumika.

Asiyejiandikisha hatopata fursa ya kupiga kura ya maoni na ya uchaguzi mkuu. Hakuna kujiandikisha tena, hii ndio ya mwisho! Asiyejiandikisha kala hasara.

Nawasihi wanachama wetu ambao ni zaidi ya milioni 8 wajiandikishe, ikiwa wote hawa watajiandikisha na kupiga kura, tutapata ushindi kwa kishindo!

JK: Ndugu wananchi, tunajua jambo kubwa ni kura ya maoni ya Katiba pendekezwa ya hapo machi, uandikishaji wa kupiga kura ndio lipo mbioni. Lingine ni uchapishaji na usambazaji wa katiba pendekezwa ili wananchi waisome.

Tuwasaidie wananchi kuwapatia elimu kuhusu katiba inayopendekezwa na kuhamasisha wananchi wapige kura ya ndio. Wenzetu watatoa elimu hasi, sisi tutoe chanya. Wao watahimiza isipite, sisi tuhimize ipite..

JK: Katiba iliyopendekezwa imebeba maslahi mapana ya nchi yetu, nadiriki kusema hakuna katiba bora kama hii ya sasa. Inatambua maslahi ya makundi maalum na namna ya kuyatimiza. Wakulima, wafugaji, wasanii, wanawake na mengine mengi.

Katiba imeshughulikia kero za muungani vizuri. Yale mambo yaliyokuwa yanaukwaza muungano, yamepatiwa suluhisho. Sioni sababu ya kukataa katiba inayopendekezwa.

Niwakumbushe, tukiikataa hii, maana yake iliyopo itaendelea kutumika, maana hakuna nyingine. Na itakuja kuchukua miaka mingi ijayo. Labda rais ajaye apate hamu. Maana mimi nilipata hamu!

Wapinzani wamesikika wakisema hawatoshiriki na kuwataka wananchi wasishiriki. Hii imenisikitisha. Mimi nawasishi washiriki, na nawasihi wananchi washiriki, wao wakitaka kususia wasusie, ila nyie pigeni kura.

JK: Nawasihi, msiache kupiga kura eti kisa tu serikali 3 haimo, maana hawana hoja nyingine. Sasa hivi bado hawa watu hawana muamko nalo, ila muda ukifika muamko utakuja. Serikali tatu haina muhemko kwa sasa.

Lakini jambo ni moja tu, kama kweli wananchi wanataka serikali tatu, na humu haimo, itathibitika kwenye kura. Wasiposhiriki tutashiriki sisi na tutashinda.

Msibabaishwe na wala msirudishwe nyuma.

JK: Wananchi, Mwezi Oktoba tutafanya uchaguzi mkuu. Utakuwa wa kihistoria kwani tunachagua Rais wa awamu ya tano. Mimi mwakani nitakuwa nafanya 'handover' tu, lakini pembeni yangu atakaa MKUU WA NCHI. Mimi nataka rais ajae awe ni wa CCM.

Maelezo ni rais, Namnukuu Mwalimu aliwahi kusema, 'Rais wa nchi yetu anaweza kutoka chama chochote, lakini rais bora atatoka CCM'. Tuuenzi wosia huu mzuri.

JK: Mgombea ambaye wananchi wakisikia jina lake tutakapomtangaza katika ukumbi wetu, wananchi watanzania waseme, 'hapo barabara'.

JK: Kushinda chaguzi za dola, ndiyo madhumuni makuu ya chama cha mapinduzi.

Tusipoipigia CCM, tutakuwa tumemuangusha muasisi wetu. Aliwahi kusema bila CCM imara, nchi itayumba. Tuhakikishe tusifanye vitendo vitakavyokiuka, laana na hasara kwa taifa ni kubwa, na ni msiba mkubwa kwa CCM na nchi itayumba! Lazima tuhakikishe hatufiki huko. Watu wazuri wapo CCM wa kutosha, naamini mnawajua.

Mnaowaona wanafaa, washawishini wachukue fomu, sio dhambi, hata mimi nilishawishiwa.

Ngoja nitoe siri moja, japo sio nyeti. Kinana aliniulizaga kipindi hicho 'umemuona mzee fulani'? Nikamjibu 'sijamwona', akaniambia ''uwe umemwona au hujamwona, we zingatia''.

Kwahiyo, Sio dhambi, mnayemuona anafaa, mpendekezeni, hata kama anasita sita na kusema hajajiandaa kisaikolojia, mwambieni 'wewe ndie unayetufaa'.

Nina imani tunao watu wazuri sana ambao watatuvusha (Makofiii).

Msanii wetu Diamond yuko hapa, atatumbuiza, ni msanii bora Afrika nzima na dunia, anapendwa sana. Ile nyimbo yake ya My Number One ikipigwa ile, hata mimi nishawahi kuiimba kidogo. (Vicheko).

JK: Nikizungumzia kwa Mkoa wa Ruvuma, hali si mbaya sana. Maana kwa takwimu za ushindi wa kura za serikali za mtaa mwaka huu, ni ushindi mzito. Tuimarishe zaidi. Kuhusu maendeleo yaa Ruvuma, yanaridhisha japo kasi zaidi inahitajika.

Kwa ufupi, Ruvuma ya miaka 10 iliyopita, si sawa na ya leo. Mwenye macho haambiwi tazama.

JK: Jambo la mwisho nitazungumzia kuhusu mazao ya wakulima. Niliwahi kuelezea kutofurahishwa kwangu na deni lisilolipwa. Nimeagiza walipwe kwanza wakulima wale wadogo, nasikia wanatangulia kulipwa mawakala halafu wakulima wanacheleweshewa. Hili liangaliwe, na walipwe kwanza wakulima wadogo.

Hivi karibuni tutapata pesa nyingi, bilioni 36, waziri mkuu anasema bilioni zaidi ya 10 zishaletwa, zipo, tutawapa. Safari hii Hatutopenda kusikia tena malalamiko.

Sasa hebu tuanze safari, wizara ya kilimo na na wizara ya viwanda na biashara washirikiane na mikoa ya kilimo kama hii.

Namalizia, Mafanikio ya kuongoza miaka 38 isitufanye tubweteke. Tuzidi kuongoza juhudi. Tuwe tayari kubadilika na kwenda na wakati. Itawezekana ikiwa tutaendelea kukuza demokrasia ndani ya chama. Na tukoseane bila chuki ndani ya chama.

Hatuna budi kuondoa utegemezi wa kifedha, kutegemea misaada, na hata ruzuku na michango ya wafanyabiashara. Ipo siku watoa misaada, na wafanyabiashara watapungua.

Tuwekeza nguvu zaidi kwenye kuzalisha kwa kutumia vizuri rasilimali zetu, lazima tuwe wabunifu. Hii yote ni ili kuwezesha chama chetu kijitegemee.

Nihitimishe kwa kusema leo ni siku ya furaha kwetu wote. Tuwakumbuke waasis japo wawili, Mwalimu Julius K. Nyerere na Aboud Jumbe, kwani kwa busara zao, wao ndio walioanzisha chama cha CCM.

Kidumu chama cha mapinduzi.

- M/kiti wa CCM Taifa, ndugu JK Kikwete ameshamaliza kutoa hotuba yake. Na sasa ratiba nyingine za sherehe zinaendelea.

MC: Kabla m/kiti hajaondoka, nimpandishe msanii Diamond.

JK: Mi bado nipo (vicheko)

MC: Hahaha, naona mheshimiwa bado yupo nasi.

- Hotuba ya rais imeisha, na Msanii Diamond anatoa burudani sasa.. (Anashangiliwa sana).
 

Attachments

  • ccm1.jpg
    ccm1.jpg
    58.8 KB · Views: 9,797
  • ccm2.jpg
    ccm2.jpg
    46.6 KB · Views: 7,487
  • songea.jpg
    songea.jpg
    75.7 KB · Views: 2,896
wamkumbuka kuwa waangaliafu na yale masifa yao ya REA?Kinana anaweza fanya stunts na maigizo yake ..sijui atawaamuru kuleta umeme kijiji gani.Wazungu wamegoma kujazia,wananchi walichokiweka CCM wamekitamani.CCM ni km Scavenger wa asili.Hata uwatunze vipi siku unawapa mkono wanakula.
 
Nawatakia sherehe njema za kuzaliwa kwa CCM muendelee kuwa mabalozi wa amani yetu ndani na nje ya mipaka yetu!
 
Star tv wanarusha live sherehe za miaka 38 za Chama cha Mapinduzi(CCM).

Tutarajie hotuba ya kujikosha kwa wananchi kutoka kwa Kikwete kama mwenyekiti wa CCM Taifa na zaidi atatumia nafasi ya leo kuipa chapuo katiba pendekezwa.

Hatakuwa na jipya zaidi ya kuwafariji wenzake kuwa watashinda uchaguzi mkuu baada ya kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa ingawa ukweli ni kuwa wameshindwa vibaya.

TBC1 na ITV pia wamejiunga na star tv kuonyesha sherehe hizo.
 
Na ITV wako live na washukuru sana! Sasa bora leo Mengi kaonesha uzalendo kwa chama chake!

Namsubiri komba atuburudishe.
 
Niache kuangalia Australian open Men's Final niangalie upuuzi wa CCM
 
Ni siku ya kuadhimisha miaka 38 ya ccm tangu kuzaliwa kwake mwaka 1977 mambo yako hivi sasa.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    469.1 KB · Views: 775
Kila siku napata sababu mpya ya kuendelea kuipenda CCM, Asanteni wana-Songea kwa kuwaonyesha Watanzania kuwa CCM haina mbadala Tanzania.
 
Back
Top Bottom