Yaliyojiri bungeni Dodoma tarehe 18 May, 2016

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Swali la nyongeza Upandishaji hadhi wa vituo vya afya una urasimu mwingi kwa nini usingepelekwa kwa serikali za mitaa

Majibu: Halifanywi na serikali kuna wataalamu wanaangalia quality control na serikali inaangalia namna ya kufanya ili ku decentralize

Swali: Vituo vya vinavyohudumia wananchi wa mbande serikali itavisaidiaje ili kuviboresha

Majibu: Vituo vya afya na hospitali vipo kwenye halimashauri kwa hiyo mipango ianzie kwenye halmashauri na serikali kwa sasa haina mpango kwa kuwa upungufu ni mkubwa kwa hiyo watafanya kadri halmashauri watakavyoomba

Swali: Mheshimiwa Ng'wani: kwa kuwa fedha zilizotolwa na wahisani ni zaidi ya bilioni 200 ni kiasi gani kilipelekwa Zanzibar na kwa kuwa kuna ufisadi katika hela hizi ni hatua gani serikali inazitumia ili kudhibiti ufsadi huu?
Majibu: Zanzibar imepelekwa bilioni 17 sawa na asilimia 7 kuna miradi mingi kama miradi ya Kilimani na Kisiwapanza watafuatilia kuhusu swala hili la kuwapo kwa ufisadi kwenye miradi chief internal auditaor anafanya kazi na bunge litapata taarifa

WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI
Swali:
Dalali Peter Kafumu: Serikali itawapatia lini wakazi wa Igunga maji ya kutosha?
Majibu: Hali ya huduma ni asilimiaa 60 ya mahitaji yote, serikali imeanza mchakato wa kutoa maji ziwa Victoria na taratibu za kupata wakadarasi ushaanza, mradi huu utaongeza upatikanaji wa maji kufikia asilimia 100

Maswali ya nyongeza: Kutokuwepo kwa umeme wa kutosha imefanya maji kuwa magumu zaidi je serikali ina mpango gani kuhusu kuwapatia Jenereta?

Swali la pili nyongeza: Tatizo la Igunga na Nzega ni sawa lakini Nzega upatikanaji wa maji Nzega ni asilimia 30 tu, jserikali ina mpango gani kununua matenki kabla ya huo mradi wa ziwa Victoria kukamilika
Majibu Swali la kwanza: Waziri wa umeme na ni sahati kunajengwa mradi wa umeme wenye msongo wa Kv 400, mkurugenzi wa halmashauri wa ya igunga anunue jenereta

Swali la pili jibu: Matanki mawili makubwa yanajengwa kupitia mradi wa ziwa Viktoria

Swali: Mheshimiwa Selasini: Miradi ya maji wilaya ya Rombo kuna miradi lakini fedha zinasuasua kwenda ni lini pesa zitaenda?
Majibu: Wameanza programu ya pili wa maendeleo ya sekta ya maji na fedha zinaanza kutolewa

Swali: Mheshimiwa Magreti Sitta: Kwa nini mtanzania akitaka kupata visa ni lazima apitie visa kupitia Kenya na Afrika Kusini, kwa nini utaratibu huo usifanyike hapa nchini ili kuondoa usumbufu?

Majibu: Utaratibu ulihamishiwa Kenya baadaye ukapelekwa Afrika Kusini ili kuleta ufanisi na unafanyika kikanda, nchi za Africa mashariki na kati zote zinafanyiwa Afrika Kusini ila mwombaji sio lazima aende Afrika Kusini, nchi ya kutoa viza yenyewe ndio inaamua yenyewe utaratibu wa kupata visa za kwenda nchini kwao

Swali lanyongeza: Tanzania ilikuwa koloni la Uingereza kwa hiyo zina uhusiano mzuri na Uingereza kwa nini serikali isiishawishi serikali ya Uingereza utaratibu ukaletwa Tanzania?
Majibu: Utaratibu huu ni kwa duniani kote, na utaratibu haujaathiri gharama za kupata visa ila unatakiwa uanze mapema lakini gharama ni zile zile

Swali: Pascal Haonga: Ni lini serikali itapeleka gari na vifaa vya zima moto mpaka wa Tunduma?
Majibu: Kuna kituo kimoja kipo lakini rasilimali fedha itakaporuhusu tutapeleka vifaa na magari mengine

Swali la nyongeza: Kwa nini magari ya washawasha badala ya zima moto?
Majibu: Magari ya washawasha yanaweza pia kutumika kuzimia moto, kwa hiyo tutafanya utaratibu wa gari hizi kutumika kuzimia moto

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Swali: Ester Bulaya: Serikali imejipangaje wananchi kushambuliwa na mamba Bunda?

Majibu: Wizara imepokea taarifa ya wananchi kushambuliwa, sheria inampa mamlaka mkurugenzi kushughulikia masuala hayo, na serikali itafanya tathimini kama kuna mamba wengi kupita viwango, watwindwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari

Swali la nyongeza: Sheria ya kazi namba 6 mtu akifa kazini analipwa fidia milioni 10 sio kifuta jasho cha laki moja ambayo waathirika wa mashambulio haya wamekuwa wakipewa

Majibu: Nchi inaongezwa kwa sheria na kifuta jasho ni sheria kama shaeria hii ya kifuta jashi haifai basi mbunge Bulaya alete mapendekezo yake na yatapitiwa na bunge kuona kama yanafaa,
 
Hivi mhe. BULAYA kila siku anaongea kwa mihemko tu anamgombeza waziri utadhani yeye amewatuma mamba Wang,ate wavuvi.

Ningependa kumpa ushauri nasihi atulie
 
Hivi mhe. BULAYA kila siku anaongea kwa mihemko tu anamgombeza waziri utadhani yeye amewatuma mamba Wang,ate wavuvi.

Ningependa kumpa ushauri nasihi atulie
Nafikiri ni katika ku 'make impression'
 
Hivi mhe. BULAYA kila siku anaongea kwa mihemko tu anamgombeza waziri utadhani yeye amewatuma mamba Wang,ate wavuvi.

Ningependa kumpa ushauri nasihi atulie
Hiyo ni kutafuta kiki,anatengeneza taswira kuwa Seikali ndio imewatuma mamba.
 
Laiti Bulaya angekuwa na elimu mithili ya Tumia Akson angekuwa mwanasiasa bora wa like wa bara la Afrika. Sasa mambo yamekuwa kinyume chake, mwenye elimu Bomu, asiye na elimu ndio super!
 
Laiti Bulaya angekuwa na elimu mithili ya Tumia Akson angekuwa mwanasiasa bora wa like wa bara la Afrika. Sasa mambo yamekuwa kinyume chake, mwenye elimu Bomu, asiye na elimu ndio super!
Kuwa na elimu siyo lazima uwe na akili.Inawezekana ukawa umeondoa hali ya kutokujua kusoma na kuandika.
 
1.JPG


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema Serikali iko katika mchakato wa kuangalia uwezekano wa kubadili matumizi magari ya polisi ya kuzuia ghasia kwa kurusha maji ya kuwasha maarufu washawasha yaweze kutumika kuzima moto.

Kauli hiyo ilitokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliyeuliza ni kwanini Serikali inanunua magari ya washawasha yasiyo na tija ambayo hutumika nyakati za uchaguzi tu badala ya kununua magari ya zimamoto.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Masauni alisema magari ya washawasha bado yana tija kwani Serikali inafanya taratibu ili magari hayo yatumike kuzima moto kwenye majanga na isiwe kwa washawasha pekee na kuwataka wabunge hasa wa upinzani kuondoa fikra za kuyapinga magari ya washawasha kwani sasa itakuwa ni neema kwao badala ya kutumika kwa kudhibiti vurugu pekee.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana Serikali ilinunua magari ya washawasha 777 kwa bei ya kati ya Sh150 milioni na Sh400 milioni, hata hivyo taarifa zingine zilisema magari yaliyotumika wakati wa uchaguzi ni 50.

Awali Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), aliuliza swali la msingi kwamba ni lini Serikali itapeleka huduma ya zimamoto katika mpaka wa Tunduma ili kuokoa mali za wafanyabiashara wanaosubiri kuvuka pindi ajali ya moto inapotokea.

Naibu Waziri Masauni alisema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika halmashauri ya Mji wa Tunduma lina kituo katika eneo la mtaa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Momba katika Mkoa wa Songwe, kinachohudumia wilaya yote ukiwamo mpaka huo.

Alisema kwa sasa kituo hicho kina gari moja ambalo nalo liko kwenye matengenezo mjini Mbeya likiendelea kufanya matengenezo huku askari wakiendelea kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na majanga ya moto.

Masauni alisema ni azma ya Serikali kupeleka huduma ya zimamoto katika maeneo ya nchi ikiwamo Tunduma, mpango huo unategemea upatikanaji wa fedha kwa Serikali.
Kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mbozi, alimuomba mbunge wa eneo husika avute subira ili waweze kuona namna bora ya kufanya kwani bajeti ya Serikali ni ndogo na vituo vinavyotakiwa kujengwa ni vingi.
 
Back
Top Bottom