Yako Wapi Majina ya Watumishi Hewa?!

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,271
1,119
Habari zenu wana JF

Binafsi napongeza hatua ya utumbuaji inayofanywa na Serikali ya Rais JPM. Niweke wazi kuwa namuunga mkono na nashangazwa sana na wale wanaobeza zoezi hili. Japo naheshimu mawazo yao lakini kwakweli nchi yetu ilipokuwa imefika ni dhahiri kwamba JPM anapaswa ku triple his actions. Aongeze kasi ya kuwafichua na kuwawajibisha wale wote waliowaumiza watanzania kwa namna yoyote ile. Awatumbue popote pale hata wakiwa bafuni na kwenye majakuzi.

Zoezi la kukagua orodha ya watumishi hewa linaendelea japo mpaka sasa imebainika kuwepo kwa zaidi ya watumishi hewa 7,500. Hii ni hatari kwa Taifa dogo kiuchumi Kama TZ. Ni hatari pia kwa nchi zinazoendelea hasa kwa bara la Africa. Nina hakika ndani ya Africa endapo patafanyika ufwatiliaji Kama wa hapa TZ basi kuna uwezekano wa robo ya watumishi wote kwenye sector za uma ni hewa. Napenda kupongeza tena juhudi za Serikali ya JPM.

Bado tunahitaji sasa kwenda hatua moja mbele. Kuanika majina yote ya watumishi hewa waliobanika kwenye zoezi hili. Kila wilaya, halmashauri, wizara na idara zake wawasilishe majina ya hao watu hewa na kuwekwa wazi. Kuchapishwa kwenye tovuti ya serikali, magazeti na hata humu JF tuyapate. Hili linawezekana tena hata ndani ya siku mbili tu. Kama tuliweza kuchapisha majina ya wapiga kura na tukabandika vituo vyote vya uchaguzi, ninaamini hili halishindikani.

Natambua wapo husika na watendaji wa Serikali ndani ya JF. Na ambao huenda wapeta time ya kusoma uzi huu...naomba twende mbele hatua moja ya kuanika majina ya watumishi hewa hadharani.

Zoezi hili litasaidia kuibeba nguzo ya msingi ya good governance (utawala bora) ambayo ni Transparency (uwazi). Lakini itasidia kuwafumbua macho wananchi na kuwajua zaidi watendaji wao ambao wanapaswa wote kuwajibishwa kwa kuihujumu nchi yetu.

Hatua ya pili ya msingi baada ya kuanika majina ni kuwawajibisha wale wote waliokula jasho la watanzania kwa kujilipa mishahara hewa. Kuanzia kwa wakurugenzi (DED), wahasibu (DT), maafisa elimu (DEO) na watumishi wa hazina (treasures) ambao wamekuwa na connection ya wizi huo na watumishi wa halmashauri na wizara husika.

Hivyo tunaomba majina ya watumishi hewa kwenye notes boards za magazeti, blogs, serikalini na social medias. Ninaamini hii itakuwa na positive impact kwa watendaji wetu na Taifa kwa ujumla.

Kwa kumaliza, baada ya zoezi la kuhakiki vyeti feki linaloendelea kwa sasa kwenye idara mbalimbali, tunatizamia pia kupata majina hadharani ya watumishi walioghushi vyeti. Tumekuwa na Taifa la wazembe, watu wasiokuwa wabunifu ndani ya serikali kwakuwa wengi wao waliingia kwa mgongo wa vyeti feki uliosukumwa na kujuana na undugu. Vijana wengi wa kimaskini na wenye uwezo wamenyimwa haki ya kuzitumikia taaluma zao kutoka na genge la 'feki'.

Wote hawa majina yao yawekwe hadharani.

Asanteni na Mungu awabariki nyote

Goodluck Mshana
 
Tena ukute kuna watu mnafanya intervw kumbe mlisha ajiriwa zamaani. Majina yenu yanaonekana tu huko wakubwa wanakula mishahara
 
Kwakuwa baadhi ya watendaji wengi serikalini wanasubiri kuagizwa basi mkuu wa nchi waagize wakurugenzi wote waweke hadharani majina ya watumishi hewa.

Hapo ndipo mchezo utashika kasi kwani wapo hewa wengine bali watu hawajajua kama wametajwa ama la.

Kwakuwa hata watendaji wakuu wanaohusika hawawezi kutoa maelekezo hayo kwenye taasisi na idara mbalimbali basi mh.

Rais tumia mamlaka yako kuwaagiza watafanya hivyo maana hata wewe unajua watatekeleza japo hawapendezewi na kasi yako.
 
Wazo lako ni zuri sana sana la kutoa hadharani orodha ya majina ya watumishi hewa.Hata mini nilishawahi kutoa ushauri au maoni ya jinsi hii lakini wahusiki labda hawakuona maoni hayo.Tatizo la nchi yetu tabia ya wakubwa kupuuza maoni ya watu wadogo au wasiokuwa maarufu.Ushauri huu ni mzuri sana lakini kama ungekuwa umetolewa na wakubwa kama akina Makonda,Nape,Kinanana kesho yake majina yote hewa yangeorodheshwa na kubandikwa mpaka kwenye kuta za madaraja ya baravarani.Kutoa hadharani majina ya watumishi hewa kutabainisha viroja vingine kama kukuta jina la mtumishi moja kuonekana pia kwenye mikoa mingine.Wapo watumishi wengi waliowahi kuhamishwa kutoka mkoa moja hadi mwingine hata zaidi ya mikoa nne au zaidi.Mimi binafsi nimetumikia mikoa mitatu kwa hiyo unaweza kukuta jina langu linalipwa kwenye mikoa yote hiyo niliofanyia kazi baada ya kuwa nimeacha kazi.Orodha ya watumishi hewa pamoja vyeti bandia vyote viwe hadharani.Kila jina lionyesha cheo alichokuwa anakitumikia na kituo chake cha kazi.Vyeti bandia navyo vivo hivyo,vionyeshe jina, cheo ,na kituo alichokuwa anakitumikia.
 
He! hilo la ukaguzi wa vyeti bandia ndio nalisoma kwako leo.Je linafanyika vipi mkuu?
 
Back
Top Bottom