YAH: Rais Dr. Magufuli nahitaji msaada wako kama kweli wewe ni mzalendo

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,184
11,201
Ndugu watanzania, serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imepata kiongoz shupavu na mwenye akili nyingi yakuliongoza taifa hili ktk kipindi hiki kigumu.

Rais wetu mpendwa amedhamiria miaka mitano ijayo tanzania iwe taifa lamfano ktk bara la afrika ktk kila nyanja ya uchumi, kuanzia ngaz ya kijiji, mpaka taifa.

Ndio hili linawezekana, ikiwa wewe kama mtanzania mwenye mapenzi mema na taifa lako utajitokeza mbele na kumuunga mkono mh Rais. Shughuli alio kwisha ifanya mpaka sasa hakuna mtanzania hajala tunda lake ila Rais angependa kuona utumbuaji majipu ukianzia ngazi ya familia mpaka kitaifa.

Yani kila unalo lifanya jiulize lina ongeza thaman kias gani kwenye taifa? Wewe kama baba ktk taifa lako umeongeza nin ktk familia yako? Wewe kama kiongoz umeleta ubunifu wa aina gani ktk taifa lako na watu wako?

Mh Rais anaitaji watu wachapa kazi na wenye ubunifu bila kusahau uzalendo wa kwel wenye kupinga unyonyaji na ufisadi. Mh Rais anaitaji msaada wako kama mtanzania kuonyesha njia ktk jamii yako na serikal yake nin kifanyike na nin kisifanyike. Ubunifu wako ni wamuhim sana ktk serikali hii.

Manazuoni huu ndio wakati wakuleta mabadiliko maana Mh Rais anaitaji mawazo yenu kulijenga taifa hili. Mh Rais anataka kufumua kila mianya ya wiz ktk serikali nakuleta mabadiliko makubwa sasa ila ktk njia yakisasa zaidi.

Uzalendo ndio sifa namba moja kumsaidia Rais. Kama Rais ameonyesha njia sasa nawewe mtanzania jitokeze kumsaidia Mh Rais ili taifa hili lisonge mbele.
 
Lugumi lugumu! Aanzena Kuleta Katiba ya wananchi. Imeweka MFUMO wa kufanya kazi. Asifanye/asiamue ATAKAVYO. Aweke msingi wake na watakaomfuta.....
 
Sidhani kama kuna lisilojulikana kuhusiana na Tanzania, anatakiwa yeye aanze kwanza kuuthibitisha uzalendo wake na uaminifu wake uozo anaufahamu, akitaka kumuua nyani asimuangalie usoni na asitofautishe nyani.
 
Nchi inaongozwa na watu lakini watu hao wanaongozwa na katiba na sheria, kwa hiyo tunataka katiba ya warioba ikamilishwe, asiongoze nchi kwa akili yake
 
Naami ata yeye mwenyewe anajua kuwa ni kipi na ni nini akiweza kukifanya wala hatahitaji ata hayo maombi yako! Kwani uzalendo si ushabiki bali uzalendo ni imani iliyondani ya nafsi ya mtu.
 
"LAITI KAMA NINGELIJUA KWAMBA KAZI YA URAIS NI NGUMU HIVI, BASI NISINGELIGOMBEA"
Kwa Mujibu Wa Kardinali Pengo, Hiyo Ni Kauli Ya Mhe. Magufuli Alipokuwa Mapumzikoni Chato, Na Kwa Kauli Kama Hiyo Nadhani Si Vema Kujivika Kiremba Cha Ukoka Kumshauri Mtu Afanye Mambo Ambayo Ugumu Wake Siujui Kiundani.
Jambo La Msingi Atekeleze Ahadi Zake Zote
 
kwa sasa Magufuli acha ayatumbue majipu yaliyoshindikana,tatizo la katiba utekelezaji wake una siasa nyingi kiasi kwamba majipu mengine hayataguswa kwa kutetewa na wanamtandao walioko kwenye maamuzi..
 
Tupo pamoja sana na JPM ila cha msingi asichague majipu ya kutumbua asizame kwa wafanyakazi wa umma tu hapan aingie mpaka kwenye viongozi wakuu wa siasa asiangalie wadhifa wa mtu .la mwisho lazima arudishe katiba ya warioba asitumie sana akili sana maana najua hataongoza milele muda utafika atamwachia mwingine ambae hatujui ni nani kwa bila katiba sahihi atakuwa ametwanga maji kwenye kinu tutarudi kule kule msoga .
 
kwa sasa Magufuli acha ayatumbue majipu yaliyoshindikana,tatizo la katiba utekelezaji wake una siasa nyingi kiasi kwamba majipu mengine hayataguswa kwa kutetewa na wanamtandao walioko kwenye maamuzi..
Ni kweli ni bora wakati huu ambao katiba inamruhusu kutumbua majipu ayatumbue kwanza mpaka yapungue au yaishe ndipo arudi kukarabati katiba ya Warioba. Demokrasia nzuri ni pale ambapo mambo yako vizuri kinidhamu. Kwa sasa hakuna nidhamu katika maeneo mengi serikalini.

Wakubwa wasiache kutupa macho na uangalizi wa kutosha katika Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College). Mahali hapo Uongozi wa juu hauna uzalendo kwa Taifa kabisa. Ubinafsi umewazidi na hivyo ufisadi umeshamiri kwa nguvu chuoni.
 
Nchi inaongozwa na watu lakini watu hao wanaongozwa na katiba na sheria, kwa hiyo tunataka katiba ya warioba ikamilishwe, asiongoze nchi kwa akili yake
tunahitaji dikiteta ili nchi iendelee, watz wengi ni wepesi kudanganywa. katiba nzuri mpaka kizizi cha nne. ona kenya katiba inawasaidia nini? mbona wizi ndiyo zaidi?
 
Mh.anaweka standard za kiongozi shupavu. ..aandae kijana mwenye msimamo kama wake ili apokee kijiti 2025
 
kama kweli magu amedhamilia kulibadilisha taifa letu rasimu ya warioba ndo jibu na njia muafaka. mishahara miwilimiwili ni matunda ya katiba ya sasa...
 
Lugumi lugumu! Aanzena Kuleta Katiba ya wananchi. Imeweka MFUMO wa kufanya kazi. Asifanye/asiamue ATAKAVYO. Aweke msingi wake na watakaomfuta.....
Nani alikidanganya katiba inaongoza? Ndiyo ni muongozo lakini Si lazima ufuatwe has a kama nchi ishakuwa corrupt kama hii ya kwetu. Katiba ni utashi wa viongozi na Si zaidi ya hapo. Mbona hiyo hiyo iliyowashinda watangulizi wake kwake unafanya kazi? Ni utashi. Tumuombee na kumsaidia. Uchavuzi ulishaisha ushabiki wa nini?
 
Ndugu watanzania, serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imepata kiongoz shupavu na mwenye akili nyingi yakuliongoza taifa hili ktk kipindi hiki kigumu.

Rais wetu mpendwa amedhamiria miaka mitano ijayo tanzania iwe taifa lamfano ktk bara la afrika ktk kila nyanja ya uchumi, kuanzia ngaz ya kijiji, mpaka taifa.

Ndio hili linawezekana, ikiwa wewe kama mtanzania mwenye mapenzi mema na taifa lako utajitokeza mbele na kumuunga mkono mh Rais. Shughuli alio kwisha ifanya mpaka sasa hakuna mtanzania hajala tunda lake ila Rais angependa kuona utumbuaji majipu ukianzia ngazi ya familia mpaka kitaifa.

Yani kila unalo lifanya jiulize lina ongeza thaman kias gani kwenye taifa? Wewe kama baba ktk taifa lako umeongeza nin ktk familia yako? Wewe kama kiongoz umeleta ubunifu wa aina gani ktk taifa lako na watu wako?

Mh Rais anaitaji watu wachapa kazi na wenye ubunifu bila kusahau uzalendo wa kwel wenye kupinga unyonyaji na ufisadi. Mh Rais anaitaji msaada wako kama mtanzania kuonyesha njia ktk jamii yako na serikal yake nin kifanyike na nin kisifanyike. Ubunifu wako ni wamuhim sana ktk serikali hii.

Manazuoni huu ndio wakati wakuleta mabadiliko maana Mh Rais anaitaji mawazo yenu kulijenga taifa hili. Mh Rais anataka kufumua kila mianya ya wiz ktk serikali nakuleta mabadiliko makubwa sasa ila ktk njia yakisasa zaidi.

Uzalendo ndio sifa namba moja kumsaidia Rais. Kama Rais ameonyesha njia sasa nawewe mtanzania jitokeze kumsaidia Mh Rais ili taifa hili lisonge mbele.
Define kwanza uzalendo ndio watu ambao ni analytical waweze kuchangia.
 
Tumepumbazwa vizuri mno na awamu hii kiasi kwamba tumeacha kabisa kufikiria mwelekeo wa uchumi wetu ambao unakufa siku hadi siku.

Tumekuwa watu wa ajabu kushangilia kila baya linapotokea na kila siku habari nzuri kwetu ni nani katumbuliwa jipu badala ya kufikiria ni viwanda vingapi vinafunguliwa na ajira ngapi zinatengenezwa. Tatizo la ajira kwetu sio tatizo tena, kuyumba kwa elimu kunakosababishwa na mfumo wa elimu bure kwetu sio tatizo tena, kuyumba kwa biashara na kudidimia kwa uchumi sio tatizo tena kwetu, viashiria vingi vinavyoomyesha serikali kukosa pesa za kuendesha shughuli zake za kila siku sio mdajala wakipaumbele kwetu, kususwa kwa uongozi Zanzibar kunakotishia usalama wa muungano wetu sio tatizo linalohitaji kutatuliwa, mfumuko wa bei unaombatana na wananchi kubana matumizi sio tatizo tena kwetu.

Tatizo kwetu sasa ni MAJIPU tu! Kana kwamba kipimo cha uongozi bora kwetu ni idadi ya majipu yaliyopasuliwa. Sijui baba wa Taifa alipasua mangapi hadi akapata sifa alizopata. Tumesahau kabisa kuipima serikali yetu kwa kupima wajibu wake katika kuleta maendeleo ya kweli kwa watu wake.

Uzalendo katika awamu hii ni kumshangilia anayefukuza wafanyakazi ambao hakuwaajiri au kuwateua pasipo kwanza kutafuta mzizi wa ubaya wao na kushughulikia, anayesababisha bandari zikose meli kwa kulazimisha kodi pasipo kujali nafasi ya kodi katika nyendo za biashara na hivyo uchumi, anayehamisha fedha za sikukuu kwenda kujengea pasipo kujali kanuni ya uchumi kwamba matumizi ya sikukuu kama muungano na uhuru nazo ni chachu za shughuli za uchumi (microeconomics) na sio kufuja mali kama anavyotuaminisha!

Kifupi Tz tumepoteza mwelekeo kabisa na hatujachelewa kurekebisha. Tumekuwa mashabiki wa mambo yasiyoleta tija au mchango halisi wa uchumi wetu na kwa bahati mbaya rais wetu anashauriwa na watu wasiomtakia mema! Tuna vijana waliomaliza vyuo bila ajira mitaani, tatizo hili hadi sasa halijaguswa badala yake tunafikiria kupunguza mshahara na huku tukishabikia fukuzafukuza. Tuna tatizo katika mfumo wa elimu bure hili nalo limeachwa! Tuna tatizo kubwa la kushuka kwa shughuli za uchumi za watu wa chini kabisa, tatizo lililosababishwa na kubana matumizi kusikozingatia madhara yake katika uchumi wa watu wakawaida. Hili nalo halijaguswa na badala yake Watanzania wanataka kusikia Lugumi na Kitwangwa wamefukuzwa!!

Naiombea nchi yangu!
 
Back
Top Bottom