Yafahamika: Meli iliyobeba sukari haikuzama kama ilivyodaiwa, shehena imeibiwa na kuuzwa Kenya

Hii ishu inanikumbusha namna Ethiopian Airline ilivyotua ghafla KIA ili wanaume washushe "mizigo" yao...

Watu wakadhani ni "emergency landing"...

Kaka tafadhali tuelezee yan ilikuaje mana sote twaamini ilikua emergency
 

Watu watokao Kanda ya Ziwa, hasa wanaojishughulisha na masuala ya majini kwa maana ya usafirishaji na uvuvi, hususan maeneo ya Visiwa vya Kome, Zilagula na vingine ndani ya Ziwa Victoria ukiwaambia au kuwatajia jina la Kitana, kisha ukaongezea Matata na wengine, kisha ukasema kuna serikali iko madarakani inatawala, wanaweza kukuona unahitaji kuwa 'screwed' ili uweze kufikiri sawa sawa kujua maana ya serikali hasa yenye mamlaka...

Ni kweli Kitana ni nomaa, pale Nyamango kuna kisiwa kidogo anakimiliki. Kama siyo mvuvi wake hakuna kukanyaga hapo.
 
Ndiyo maana mimi majuzijuzi nilishangaa sana, yaani kila nikinywa maji ya ziwa victoria yanakuwa matamu kama vile yametiwa asali ya nyuki wadogo.
 
Sitaki kusikia majina ya hawa watu... Nimefilisika na kuhama MWANZA kwa unyama wa watu hawa!

Hivi kwanini watu wa Mwanza hupenda sana kuchagua majambazi? kumbuka hata yule mzee wa uporaji ardhi mpaka wananchi walikuja mtwanga na mawe. Anyway viongozi wengi wa ccm wana tabia hiyo na hapo utaona dana dana za policcm. mara utasikia uchunguzi unaendelea, tumeunda tume au tunatoa donge nono kwa mwenye taarifa. Hivi hiyo intelijensia ya polis haikunasa hili mapema? Au ni kwenye mikutano ya CDM tu?
 
Masikini watanzania wengi ni mapungufu tu,majanga. Hivi hapa mnajadili nini hasa. Great mind discuss great issue
 
Ton 280 za sukari zina thamani kubwa kuliko hiyo boat?

Kiongozi ni hivi, boat ina bima na imechoka hivyo unapakia mzigo wa maana then mbeleni unapakuliwa, meli inatobolewa inazama na inawekwa mifuko iliyofunikwa vizuri kuonesha sukari iliyeyuka mifuko ikaelea. Mzigo utauzwa na atalipwa pesa ya kujenga boat mpya.
Hii ni kama stori ya kituo flani cha redio dar kiliunguza ofisi makusudi na kulipwa pesa ya kujenga na kununua vifaa vipya vya kisasa. Ni michezo tu hata wa mabasi wanafanya
 
hao hawajui wanachokisema....hiyo meli ni zaidi ya bilion mbili...wao wanaropoka tu
 
Ile meli iliyotangazwa imezama katika ziwa Victoria na tani 280 ya sukari siyo kweli. Haikuzama ila umefanyika wizi na mmiliki wa meli hiyo Kitana Chacha wa Mwanza ambaye ikiwa njiani zilikuja boti kadha kutoka Kenya na sukari ikapakuliwa na kuingizwa kwenye hizo boti, na baada ya hapo meli ikazamishwa kwa kutobolewa chini ingawa haikuzama yote.

Inafaa vyombo husika vichunguze issue hii kwa kina na huyo Kitana na wafanyakazi wale wa meli wahojiwe kueleza ukweli.

Huyu Kitana ni swahiba wa Matata yule Meya wa Ilemela na wawili hao wamekuwa wakishiriki sana katika vitendo vya ujambazi katika Ziwa Victoria.

Kitana Chacha tena, nilidhani ameacha?

Alikuwa akiogopewa sana enzi hizo kisha akatulia, ameanza tena?

Ama kweli maji hata uyachemshe namna gani hayasahau ubaridi!!!


Mkuu Ritz nadhani unamfahamu huyu jamaa manake nawe huenda uliwahi kuwepo kule kwenye visiwa vya Juma na Lyakanyasi

 
Last edited by a moderator:
Kiongozi ni hivi, boat ina bima na imechoka hivyo unapakia mzigo wa maana then mbeleni unapakuliwa, meli inatobolewa inazama na inawekwa mifuko iliyofunikwa vizuri kuonesha sukari iliyeyuka mifuko ikaelea. Mzigo utauzwa na atalipwa pesa ya kujenga boat mpya.
Hii ni kama stori ya kituo flani cha redio dar kiliunguza ofisi makusudi na kulipwa pesa ya kujenga na kununua vifaa vipya vya kisasa. Ni michezo tu hata wa mabasi wanafanya

Mkuu hapo pameniacha hoi!! Kumbe kale ka pale Kitega Uchumi ilikuwa mchezo uliotupeleka Mikocheni!!!!
 
Boti ilibinuliwa kiufundi mkuu. Sasa hivi imeshavutwa ipo ufukweni Mwaloni 'Safe and sound'




Kwaiyo wameondoka na kitita cha pesa haram za kitanzania 560, 000, 000, wanasemaga tumejaribu tumeweza na sasa tunasonga mbele
 
Mkuu ni true story.. Iwapo watu waadilifu wataingia madarakani nikiwa hai nitatoa ushahidi.. Ningeendelea kubaki Mwanza hivi sasa ningekuwa nimeuawa!.
Mwaga data humu utapata japo ushauri nasaha kusubiri waadilifu nchii hii its a dreaming for imposible
 
Back
Top Bottom