Ralphryder
JF-Expert Member
- Nov 16, 2011
- 5,599
- 1,798
Yaani aibu tupu, pamoja na chopa bado waliojitokeza ni wahuni wachache hata akina mama ni wa kuhesabu! source ITV.
wananchi wa kalenga ni mabogasi!
Ushabiki ni ugonjwa wa hatari sana. Kalenga watafanya makosa makubwa sana kuchagua CCM kwa mantiki tu kwamba Ubunge sio rambirambi au kifuta machozi. Ubunge ni kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi kazi ambayo inahitaji elimu, uzoefu wa uongozi katika utumishi wa umma na weledi vitu ambavyo Godfrey hana na hajapimwa kama anavyo. Mara mia wangempendekeza Abbas Kandoro ambaye kwa maoni yangu alikuwa anafaa kuliko hata William kutokana na vigezo hapo Juu. Isitoshe Msimamo wa William pale hazina uliwakera sana kiasi cha Kinana kumuita ni mzigo, iwaje leo CCM hao hao waanze kumsifia Godfrey kuwa ni Chaguo zuri. Chaguo la Godfrey ni kutaka kumbabaisha ili asijue chanzo cha baba yake kupelekwa Afrika Kusini na kumsaidia mama yake. Ni muda tu dogo atajua watakapomtosa 2015.Yaani aibu tupu, pamoja na chopa bado waliojitokeza ni wahuni wachache hata akina mama ni wa kuhesabu! source ITV.