Xmass ni sherehe za kidini au kibiashara zaidi?

Annina

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Posts
437
Reaction score
59
Wapendwa wakati tunaelekea kusheherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo si vibaya tukatafakari lengo la sherehe hizi. Binafsi nimekuwa nikijiuliza kama sherehe hizi zimebaki kuwa za kiimani zaidi hasa kwa wakristo au zimekuzwa na wafanyabiashara kwa malengo ya kuvuna pesa?

kwa kifupi hiki ni kipindi cha mauzo makubwa ya nguo, maua, cards, CD's, vyakula, vimiminika (hasa aina ya lager!) na kila aina ya bidhaa na huduma kwa kisingizio cha kukumbuka kuzaliwa kwa Mesiah! Nisingekuwa na tatizo kama vitendo hivi vingeenda sambamba na utekelezaji wa mafundisho ya Yesu wa Nazareti, lakini kwa maoni yangu nguvu kubwa imeelekezwa kwenye kusheherekea katika namna ya kuwanufaisha wafanyabiashara na sio katika kutafakari ujio wa Mwana wa Mungu.

Tujadili
 
I do make a lot money this time of the year...more spending from folks good news for my pocket...as for religion I don't care..
 
I do make a lot money this time of the year...more spending from folks good news for my pocket...as for religion I don't care..

Tumaini,
Nimeipenda hii, umekuwa mkweli maana wengine wangeanza na visingizio kibao kwamba wanafanya yote hayo ili kumtukuza Mungu! Mfanyabiashara yeyote makini sasa hivi soko lake lipo kwa Yesu! Music wa Yesu, hospitali za Yesu, shule lazima ziwe ni St... nk nk tutashuhudia mengi kizazi hiki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…