Tafakuru nakupa pole sana kwa masahibu ya kupotelewa na mizigo yako maya unapo tuma Dar kwa basi. Mimi naamini kwa mtu kuwa na biashara kubwa na yenye heshma kama Abood, hawezi kuwa tayari kuona jina la biashara yake linaharibika kwa sababu ya mtu/watu ambao hawana sifa za kufanya kazi kwenye biashara yake. Anacho hitaji kwetu ni taarifa za ukweli na zenye ushahidi ili aweze kuchukua hatua sahihi na za haki.
Kwa mtazamo wangu, nafikiri ungesaidika kama ungejumuisha mambo yafuatayo;
1. Ni mara ngapi umetuma mizigo ikawa inapotea?
2. Wakati wa kutuma mizigo yako huwa unailipia na kupewa risiti?
3. Wakati wa kutuma mizigo huwa unawaambia waandike (kwenye risit) kitu halisi unachotuma?
4. Unazo risiti zozote za Abood zinazo onesha ulituma mzigo (jina la bidhaa) na haikufika Dar
4. Una ushahidi wowote kuwa uliyemtuhumu hapo juu anahusika na wizi wa mizigo? na kama unao ni ushahidi gani?
Naamini ukitoa hayo majibu yakujitosheleza, wanaohusika wataona kama kuna ukweli wa kisheria na hivyo kuchukua hatua za kinidhamu na za haraka ili kuwapa wateja amani.