Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,717
- 2,594
Kama ilivyo ada JF ni paa la bati, juzi ilitolewa taarifa katika radio za mtwara kwamba gari semi trailer mbili zimepotea katika mazingira ya kutatanisha na kufikisha idadi ya magari matatu ndani ya siku mbili.
Korosho imekuwa dhahabu na kwa lugha ya kitaa gunia tatu ni zaidi ya milioni. Yaani lorry moja lina zaidi ya gunia mia 500. Manake wahuni ndani ya siku mbili wamepiga nusu bilioni bila bunduki kulia na hajaumizwa mtu.
Miezi michache iliyopita wahuni walipita na lorry la cement kitoka Dangote likakamatiwa Mtwara town na watu wakimalizia kushusha mifuko ya mwisho tena baada ya kuzinguana wenyewe.
Inawezekana vipi kuiba lorry zima zima pamoja na ulinzi mkali wa korosho mtwara, wengine tuliwahi sema kuhusu barriers barabarani lakini uwezi amini watu wametusua.
Za kijiweni zinasema gari zinaenda kuchukua mzigo na namba za pikipiki bush wakifika town wanaweka namba halisi na wanasepa na korosho. Tunaandika sababu mwisho wa siku msiseme mkulima ndio kapoteza wakati alishakabidhi korosho ghalani.
Mwisho jamani wahusika wakumbusheni matumizi sahihi ya pesa, wiki iliyopita kuna mzee kavuta baada ya kupatamstuko wa pesa nyingi alizolipwa zaidi ya 30M ghafla na vijana wanahasira na boda boda. Wakumbuke na kuna watu wananyatia pesa zao.