Wizi wa laptops kwenye mabasi

mabegi ambayo yana vifaa maalumu ni bora kukaa nalo kuliko kuweka juu siti.na kila mda unaitoa watu wakajua kunalaptop au vifaa muhimu.
 
Siachi negi ndani ya basi, kwanza unaambiwa kabisa mzigo wa ndani siyo dhamana Yao, unaachaje?!
 
Vifaa vya muhimu km ivyo unatakiwa ukishuka kwenda msalani au kupata chakula, we shuka tu na begi lako. Dunia ya ss hakuna kumuamini mtu. Na ndiyo maana huwa wanasema kabisa mzigo wa ndani ulinzi ni juu yako abiria.
 
Mimi ni muhanga wa haya matukio. Huu wizi umekithiri na inaonekana kuna uswahiba kati ya wezi na wafanyakazi wa mabasi.
 
Ukiwa na Laptop kwenye basi, pakata begi lako mpaka ukifika. Wezi wengi sana kwenye mabasi
 
Ukiweka begi lako juu, linasukumwa taratibu mpaka linasogea then linaondoka.
Pia wanapuliza dawa au kunusishwa kitu, then unasinzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…