wizi wa computer

the great wizard

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2015
Posts
1,482
Reaction score
894
Siku hizi wizi wa vifaa vya kuhifadhia kumbumbu muhimu huwa vinaibiwa sana haswa komputa , komputa nyingi tumeshuhudiwa zikiibiwa na wengine wakitangaza katika mtandao kuhusu hizo computer zao au simu zao wanatowa mpaka serial numbers na vitu vingine .

Mara nyingi vitu wanavyovitaja kama ushahidi kuweza kupatikana vifaa hivyo ni rahisi kubadilishwa , mfano unakuta matu anasema username yake ni anon2232 , au ina winxp , hdd yake sijui iko hivi na vitu kama hivyo .

Nyingi ya hivyo vifaa inakuwa ngumu kupatikana kutokana na hayo maelezo hayajitoshelezi vizuri kuweza kutafuta hata kama mtu alitumia computer hiyo kulogin katika internet au kuitumia katika shuguli zingine .

Mfano ukitaja serial number – zile ni sticker mtu anaweza bandua akabadika ya kwake au akafunika na kitu kingine au akaedit vitu Fulani katika bios , kuhusu os pia mtu anaweza kuifuta na kuweka yake anayojua yeye na maelezo yake .

Tukio hili
Mtu mmoja aliibiwa laptop yake , lakini hakuwa na maelezo yakutosha kuhusu kifaa chake hicho , chakufanya nilimuomba anipe documents zake alizokuwa anaprint kutumia computer ile na vitu vingine alivyotumia kusave file zake .

Maswali yafuatayo ilibidi ajibu

1. Aina ya computer
2. Imetengenezwa na kampuni gani
3. Imetengenezwa mwaka gani , na toleo la ngapi kwa mwaka huo
4. Aina ya Chipset
5. Aina ya Bios , version gani ya mwaka gani
6. Serial Number zake ( kama inazo ) ya monitor , system
7. Aina ya motherboard ( serial numbers zake , imetengenezwa wapi na nani )
8. Aina ya CPU , uwezo wake , Speed yake , imetengenezwa mwaka gani na toleo la ngapi
9. Aina ya network card
10. Aina ya Harddisk Drive , speed yake ,na ukubwa wake
11. Aina ya ram , imetengenezwa na kampuni gani , mwaka gani na speed yake , kama ni ddr aina gani ya ddr , 1 au 2
12. Kama aliitumia katika internet ( watu gani aliwasiliana nao )
13. Kama kuna vifaa vingine vyovyote vimeunganishwa kama kadi
14. Kama kuna alama yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…