Wizi kupitia mitandao ya simu

Tamaa zetu ndio sababu ya kuumizwa
Hapana mkuu sio tamaa sema ukiangalia unafanyaga miamala mingi so kwanini usipokee zawadi????

Neno zawadi au "bonus" halijawahi acha mtu salama.

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Tusambaze ujumbe mkuu ili watu wafahamu at least tutapunguza

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
-------___________________________------------
 
Mkuu mazoba mjini hawatakaa waishe kuna mpango wangu wa kando niliufungulia kibanda cha m-pesa juzi kapigwa za uso mpaka nimeshindwa kumuhurumia
HHahahaaaa....mchepuko alianzaje kukusimulia asee cpati picha jicho ulomwangalia

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Mkuu mazoba mjini hawatakaa waishe kuna mpango wangu wa kando niliufungulia kibanda cha m-pesa juzi kapigwa za uso mpaka nimeshindwa kumuhurumia
Alipigwa sh ngap

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Mpuuzi na mpumbavu ndio anaweza kuibiwa namna hiyo
Hahahahaa...ngoja yamkute ndugu ako ndo utajua kama mpumbavu au mpuuzi. Mjini ujanja ujanja

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Hao matapeli wanashirikiana na baadhi ya staff wa mitandao husika. Ndio maana wanaweza kuwa na details zako zote hasa transaction zako zote.
Kuna jamaa namjua ndio michezo yake hiyo. Na wanashirikiana na mtu m1 yuko customer care.
 
Mtaje mwanangu, maana nnahasira nao kinoma

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Mbona maelezo yooote hayo ni ya kuibiwa tuu inakuwaje mtu hashtuki? Daaa wajinga ndio waliwao!
 
Hao matapeli wanashirikiana na baadhi ya staff wa mitandao husika. Ndio maana wanaweza kuwa na details zako zote hasa transaction zako zote.
Kuna jamaa namjua ndio michezo yake hiyo. Na wanashirikiana na mtu m1 yuko customer care.

Ndio maana hawawapigii watu wasiokuwa na salio la pesa nyingi kwenye simu. Maana wana taarifa kwamba fulani ana hela. Lazma wanashirikiana na watu ndani ya mtandao wa simu husika.
 
Asante sanaaa mkuu na huu wizi hufanywa hasaa kwenye tigo pesa na m pesaa wanacheza sanaa ba akili za watu na details zote huwa zinatoka kwa hao jamaa wa IT kutoka mitandao nimetaja hapo juu....
Kwa wizi huu hakuna detail wanazopata kutoka kwa maservice provider bali ni ujanja wakubahatisha namba wanafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wahusika ndani kwani wanaweza block number yako na kutumia number yako kwa text message kumtumia ndugu au rafiki wakitaka hela asipokuwa mjanja anaetumiwa sms imekula kwake
 
Sehemu ya pili.

Habari wadau ...! juzi kati nilipost juu ya wizi unaoliza ndugu zetu kila kukicha kupitia mitandao ya simu.
Pitia hapa kwa sehemu ya kwanza

Wizi kupitia mitandao ya simu

Sehemu hii ntaonyesha ni jinsi gani wezi hutumia akili ama mteja huibiwa kijinga kwa kutokujua kupitia mawakala wausajiri (freelancer) fake au wasio waaminifu.

Ipo hivi upo nyumbani kwako umetulia sebureni ukipiga stor na wife au kucheki kideo mda si punde wanapita mawakala wa mtandao wowote(tigo,voda,aitel n.k n.k) wakijifanya wanasajiri laini,kusajiri huduma za nivushe,m-pawa, timiza au kukamilisha sajiri za laini ya mitandao husika, ukiwa mmoja wa wanaohitaji huduma kati ya hizo unawaita na kuwaeleza shida yako na wao watakuomba utoe laini yako uwape ili waweke kwenye simu yao kwa kuwa lazima watumie simu yao ya kazi ili kukuhudumia. Tuchukulie mfano. Mteja anahitaji kusajiliwa m-pawa ya vodacom, msajiri huchukua laini ya mteja na kuiweka kwenye simu yake ya usajiri na kujifanya anasajiri. Itafika kipindi atakupa simu uweke namba ya siri ili kukamilisha usajiri wako. Pasipo kujua kama wakala usajiri ameingia katika menu ya m-pesa na kufuata hatua zote za kutuma pesa na kinachosubiriwa ni namba ya siri ili kuruhusu muamala. Mteja ataingiza namba ya siri na kumrudishia wakala usajiri aendelee na zoezi kumbuka ukiweka neno siri namba hubakia zilivyo (hazifichiki). My friend kama una laki tano au milioni zote zitahamishwa na sms zote zitafutwa muda huo huo ili kuficha ushahidi, kumbuka huwa wanauliza salio la mpesa ili kukuhakikishia huduma ya m-pawa kukamilika. Wakala huenda mbali zaidi na kubadili namba ya siri ya mteja kisha kumwambia kuwa zoezi limekamilika baada ya saa 24 m-pawa itakuwa active ili mteja aendelee kutumia. Mwisho huomba malipo ya huduma na kutokomea. Mteja akija kushtuka ni pale anapo fanya muamala na majibu huambiwa namba ya siri sio sahihi Akipiga simu huduma kwa wateja atapewa taarifa ya fedha zake kuhamishwa na upande wa pili umeshatoa hizo pesa. Kinachofuatia ni kilio kwa uchungu sababu ya kutokujua au uzembe

My take: tuwakumbushe watumiaji wa mitandao hii kuwa makini kwa kuwa kila kukicha mbinu zina badilika na wizi unashamili kila iitwapo leo. Next time ntaweka sehemu ya tatu kuhusu mawakala wa tigopesa, airtel money au m-pesa wanavyolizwa na kupoteza mitaji yao .

Asante

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Shukrani mkuu.

Hayo masuala ya sijui niunge mpawa, mara 4G, sijui nini yataendelea kuishia masikioni tu.
 
Shukrani mkuu.

Hayo masuala ya sijui niunge mpawa, mara 4G, sijui nini yataendelea kuishia masikioni tu.
Pamoja sana chief.

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Huwa nipo makini sana akisema weka namba ya siri napiga OK hapohapo kwa kuwa ni SIRI haitakiwi aijue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…