Mwezi uliopita tulisimama pale Comfort hotel na gari ndogo ili kupata chakula. Mara mhudumu mmoja wa kike 'aliokota' laptop imewekwa kwenye mfuko wa Rambo, akaulizia lakini haikuwa ya mmoja wetu.
Ndipo ikatoka stori kwamba abiria mmoja aliyekuwemo katika basi moja linalokwenda Songea (nimesahau ni lipi) alitoa tangazo laptop yake imeibiwa, wakasachi ndani ya basi haikupatikana na wakaondoka kwenda kuripoti kituo cha Ilula kwa sachi zaidi.
Nadhani jamaa alivyoona dili limetimuka akaamua kuachana nayo pale pale hoteli. Au walikuwa na makubaliano na mmoja wa wale wahudumu lakini bahati mbaya ule mfuko aliuona mwengine na akadhania kuwa mmoja wa abiria amesahau mzigo wake.
Bado ule msemo wa Abiria chunga mzigo wako unafanya kazi.