Kwa muda mrefu sasa watu mbalimbali nchini wakiwemo wazazi,viongozi wa serikali,wanasiasa,wanaharakati na wadau wengine wamekuwa wakilalamika juu ya matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka 2013 ,ambayo kwa miaka mingi hayajawahi kutokea. Katika matokeo yale,wapo waoilaumu serikali,wengine wanawalaumu walimu na baadhi wanazilaumu pande zote yaani wanafunzi wenyewe kwa tabia yao yakutopenda kujisomea,wazazi kutopenda kufuatilia mienendo ya watoto wao kitaaluma na jukumu hillo kuwaachia walimu pekee,serikali kwa kutokuwa na mfumo bora wa elimu na wengine wanaliona suala hili linatokana na walimu kutofundisha kutokana na kuwa na mgogoro wa muda mrefu na serikali kuhusu maslahi yao mbalimbali kama vile mishahara isiyokidhi,stahiki mbalimbali kama vile masomo,likizo,matibabu,posho ya mazingira magumu nk.,huku wengine wakiangushia lawama zao moja kwa moja kwa baraza la mitihani. Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dr. Shukuru Kawambwa wakati akitangaza matokeo haya alitoa sababu mbalimbali ambazo zimechangia ufaulu huo mdogo wa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule nyingi nchini hasa zile za serikali kuwa pamoja na sababu nyingine, upungufu wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia ni moja ya tatizo. Mengine ni upungufu wa walimu katika shule za kata na ukosefu wa hosteli jambo ambalo linaathiri elimu kwa wasichana ikiwa pamoja na kupewa kazi nyingi na wazazi wao wawapo nyumbani na kulubuniwa na wanaume njiani wakiwa wanakwenda shule au kurudi nyumbani. Kwa maoni yangu,naona sababu hizi ni za kweli lakini siyo sababu kuu,ila ni sababu zinazochangia tatizo kutokana na ukweli kwamba ufaulu umekuwa mdogo hata shule zile zenye hosteli,bweni hata zile za wavulana peke yake ambao hawalubuniwi na mtu waendapo au wawapo mazingira ya shule. Pili, shule hizo hizo na katika mazingira hayo hayo kwa kipindi cha nyuma ziliweza kufanya vizuri na baadhi ya wanafunzi kutoka shule za kata waliweza kufanya vizuri na kuendelea na kidato cha tano ambako pia ilipofika mitihani ya kidato cha sita walifanya vizuri na wale walioongoza kitaifa,walikwenda kupongezwa bungeni. Tatu,baadhi ya masomo kama vile uraia ,historia,Kiswahili,kiingereza wanafunzi wamefanya vibaya licha ya kwamba haya hitaji maabara,labda maktaba. Katika kuliangalia tatizo hili,kwa mtazamo wangu ningependa watanzania washawishike na waungane nami kuwa sababu zilizo changia kufeli kwa wanafunzi wengi kidato cha nne kuwa ni mfumo mbaya wa masomo shuleni, tatizo la mitaala, mgomo wa walimu,ukosefu wa chakula shuleni kwa shule za kutwa,umbali kutoka nyumbani kwa wanafunzi hadi shuleni kwa shule za kutwa,utandawazi,ushiriano mdogo kati ya wazazi na walimu,likizo ya muda mrefu(kwa mwakajana tu),kupuuzwa kwa mitihani ya kidato cha pili na darasa la nne,upungufu wa maabara na maktaba,kutofuatilia matokeo ya ya tafiti mbalimbali za kielimu za huko nyuma ,uwekezaji mdogo katika elimu na ukubwa wa wizara yenyewe,uwezo mdogo wa wa baadhi ya wanafunzi kumudu masomo ya sekondari. Hivyo nitagawa matatizo haya katika makundi mawili. Kundi la kwanza,ni sababu zinazohusika na matokeo ya mwaka 2013 pekee na kundi la pili ni lile lenye sababu za kupromoka kwa kiwango cha elimu siku hadi siku.
A:UFAULU MBAYA WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2013
Kundi hili lina sababu zifuatazo,mgomo wa walimu na likizo ndefu ya sensa.
Mgomo wa walimu:
Kwa muda mrefu walimu walikuwa na mgogoro na serikali wakidai nyongeza ya mishahara,stahihiki zao mbalimbali kama vile posho ya mazingira magumu, malimbikizo ya mishara,pesa za kujikimu nk,lakini serikali ilishindwa kutimiza madai hayo jambo ambalo lili sababisha walimu kukata tama,hasa baada ya mahakama kuu kitengo cha kazi kuamuru walimu waachane na mgomo na badala yake warudi kazini wakaendelee na shughuli za ufundishaji. Jambo la mahakama kuamuru walimu warudi mdarasani kufundisha halikuwa baya,ila walimu walikuja kutambua kuwa serikali haikuwa na nia ya dhati ya kuumaliza mgogoro ule na walimu kwa kukaa pamoja nakupata suluhu baada ya mahakama kuwa tayari imezuia mgomo. Baadhi ya walimu waliona kama serikali imewapuuza na kuamua kuwa komoa hasa baadhi ya halmashauri kuamua hata kuwaengua katika zoezi la sensa,eti watahiribu. Swali la kujiuliza ni hivi ,kazi ya kufundisha siyo ya serikali ambayo inaweza pia kuharibiwa na walimu wenye hasira? Lakini ukweli ulikuja gundulika kuwa wapo maofisa wa serikali waliamua kujenga ile hoja kwa namna ile na kuiaminisha serikali na umma,kumbe nafasi zile walitaka kuziuza na kuwapa jamaa zao. Lipo pia swali juu ya mgomo wa walimu kuwa siyo sahihi kwa kisingizio eti mbona shule za binafsi zikiwemo za seminari nazo zimefelisha,hivyo sababu ya mgomo wa walimu haina ukweli,lakini lazima watu watambue kuwa ongezeko la mshahara serikalini linafanya pia mshahara uongezeke katika shule za watu binafsi zikiwemo seminari, hivyo mgomo ule ulikuwa wa walimu wote bila kujali wapo serikalini au laa.
Likizo ndefu ya sensa: Kulingana na watoto wetu wa siku hizi ambao wengi wao wameathirika na utandawazi,hawatakiwi kukaa muda mrefu bila kuwa na mwalimu ambaye anawahimiza kujisomea au kufundishwa. Kwakuwa serikali haikuwachukua walimu wengi kwenye zoezi la sensa kwa madai kuwa watahujumu kutokana na mgomo wao,walipaswa kuamuru shule zifunguliwe ili walimu waendelee na ufundishaji,lakini pamoja na wazo hili kutolewa na chama cha walimu Tanzania (CWT) kwa serikali lakini bado serikali ilipuuzia ikaendelea kizifunga shule. Baadhi ya shule hazikutoa mwalimu hata mmoja kwenda kwenye zoezi la sensa,je,kulikuwa kuna haja gani kwa shule kama hizo kufunga? ,kadhalika shule zilizotoa mwalimu mmoja,wawili,watatu,au hata watano wasingesababisha shule zifunge . Wanafunzi nao hawakuchukua tahadhari juu athari hii na ile ya mgomo,wakasahau kujisomea wakiwasubiri walimu,wakashitukia mtihani umefika ,wakashindwa kuandika wakaishia kuandika matusi,kuandika mashairi ya nyimbo na kuchora vibonzo.
B: SABABU ZA KUSHUKA KWA UFAULU SIKU HADI SIKU
Kundi hili linasababu zinazochangia kuporomoka kwa matokeo ya mitihani kwa kidato kwa ngazi zote za elimu pamoja na mchango wa baadhi ya sababu hizo katika matokeo ya kidato cha nne 2013. Baadhi ya sababu hizo ni:
Mgawanyo mbaya wa masomo mashuleni:
Miaka ya nyuma kabla ya miaka ya 2000s,wanafunzi mashuleni walijifunza masomo kama vile kilimo,sanaa na ufundi,uchoraji,muziki,sayansi kimu,uchapaji,upishi,biashara, na msomo ya kawaida kama vile hisabati,Kiswahili, kiingreza nk. Masomo haya yaliwafanya watoto kujielekeza katika michepuo wanayo iweza,kwa mfano,asiyeweza kuchora,alisoma masomo ya sayansi au biashara,wakati wengine wakijikita katika ufundi,uchapaji nk.lakini masomo haya hayana msisitizo tena mashuleni na wala vyuo vya ualimu kwa kiwango kikubwa haviandai tena walimu wa masomo haya ya muziki,uchoraji,upishi nk.,jambo ambalo linawafanya watoto wasome masomo yanayofanana,yaani hisabati,biolojia,kemia,kiingereza,Kiswahili,Fizikia,uraia na jiografia bila kujali uwezo wao wa kitaluma na vipaji vyao. Jambo ambalo situ linawathiri wanafunzi wenye uwezo mdogo, bali hata soko la ajira kwa baadae,kwani ni vigumu kuwaajiri watu watu wenye ujuzi unaofanana. Mwanafunzi Yule aliyechora kibonzo cha ZOMBI KASAHAU KUVAA VIATU, na wale walioandika nyimbo kama yangeachwa masomo haya wasingepata sifuri.
Tatizo la mitaala:
Kubadlikabadilika kwa mitaala ni tatizo pia la kufeli wanafunzi .Mitaala inapobadilika walimu huwa hawahusishwi katika utengenezaji wa mitaala hiyo. Aidha ,hata mbinu mpya za kufundishishia ambazo zimependekezwa katika mihustasari walimu huwa hawapewi semina,bila kujali wao ndiyo ni watekelezaji wa mitaala hiyo na mihuhtasari.
Walimu hukosa mafunzo kazini:
Tukichukulia kwa mfano,wapo wale walimu wa shule za msingi ambao walipata mafunzo ya mwaka mmoja na wale wa sekondari waliopata mafunzo ya mwezi mmoja kwa makubaliano kwamba maada ya miaka miwili ikipita wajiendeleze ili wawe walimu kamili(kwa wale wa sekondari)lakini serikali ni kwa kiwango gani imefuatilia utekelezaji wake?baadhi ya walimu walishindwa kwenda kujiendeleza kutokana na uhaba wa walimu katika shule zao.Je,mafunzo gani walimu hawa walipewa kuboresha utendaji wao? Nini hatima yao kiutumishi?
Kukosekana kwa chakula shuleni:
Shule nyingi za kutwa hasa za kata hazina utaratibu wa kutoa chakula cha mchana shuleni ,kutokana na ukweli kwamba michango ya chakula hugharimiwa na wazazi ambao wengi wao uwezo wao ni mdogo na baadhi ya wazazi kutokuona kama jukumu hilo ni la serikali,au serikakali za mitaa kutowashauri vema. Hivyo kutokana na tatizo hilo,watoto wengi wanashindwa kuhimilili masomo na hivyo hutoroka vipindi kabla ya muda. Kama vile haitoshi,umbali huwaathiri wanafunzi kimasomo.Kwamfano mwanafunzi atoke mbagala anatakiwa kwenda kusoma bunju na prukshani zote za usafiri,je mwanafunzi atakuwa na ari ya kusoma?
Wazazi kutosimamia mwenendo wa watoto wao kitaaluma:
Wazazi wengi huwa wanajishughulisha na matokeo badala ya mchakato. Hapa nina maana kuwa,ni vema mzazi kufuatilia maendeleo ya mtoto wake akiwa katika kila ngazi ya mafunzo,mfano kidato cha kwanza,pili,tatu mpaka cha nne,badala ya kumwachia mwalimu jukumu hilo na mzazi kusubiria aje asikie matokeo tu mwaka wa mwisho.
Kupuuzia ripoti mbalimbali zinazohusiana na matatizo ya elimu:
Kama tume mbalimbali zinazohusu matatizo mbalambali ya elimu zilizopita kama ziliweza kutoa masuluhisho ni tatizo. Katika ripoti zile huenda kuna baadhi ya masuluhisho na mapendekezo yametolewa ambayo yangeweza kushughulikiwa kidogokidogo mpaka yangepungua au kwisha kabisa.
Wizaara ya elimu ni pana mno kwa waziri mmoja kuimudu:
Wizara ya elimu kwa sasa ni kubwa mno kiasi cha kuwa ni vigumu kwa waziri mmoja kushughulikia matatizo yaliyo katika shule za chekechea,msingi,sekondari,vyuo vya ufundi na ualimu paja na vyuo vikuu ambapo kwa sasa shule za msingi ni nyigi,sekondari hadi vyuo vikuu ambavyo navyo ni vingi .Ni vigumu kwa waziri hata kama angekuwa mahiri kiasi gani kuimudu wizara kubwa kama hii tena yenye changamoto nyingi kama hizi. Matatizo ni mengi ambayo naweza kuyaelza hapa lakini naona kwa leo niishie hapa.
MAPENDKEZO
1.Nivema kila changamoto inapojitokeza kama vile matatizo yanayo husu walimu madai yao yaka chunguzwa uhalali wake na hatua stahiki ziwe zinachukuliwa kwa wakati muafaka kupitia vikao mbalimbali vikiwa vinahusisha wadau wote.Napale inapotokea kutoafikiana basi tahadhari ichukuliwe kuangalia namna ya kumaliza mgogoro pasipo kuathiri upande wa pili.
2.Wizara ya elimu kama inawezekana igawanywe kuwa mbili au tatu ili kurahisiha utendaji kuliko ilivyosasa na wizara ambazo hazina changamoto kubwa ziunganishwe ilikupunguza uwingi wa wizara.
3.Serikali iweke utaratibu utakaowezesha kila mwanafunzi aweze kupata chakula shuleni ili kupunguza utoro wa rejareja hali ambayo hupunguza ufanisi kitaaluma kutokana na ukweli kwamba hakuna mwanafunzi ambaye anaweza kuhimili masaa zaidi ya nane bila kula na akasikiliza vipindi kwa uhakika.Tatizo hili ni kubwa katika shule za kutwa hasa zile za kata.Madiwani,watendaji kata,mitaa watumika kuhamasisha watu wao/wananchi kuchangia chakula shuleni. 4.Shule nyingi za kata hazijakamilika kimiundombinu kama vile madarasa,maabara,makitaba na hosteli.Kwakuwa madiwani na watendaji kata kwasasa hawa himizi tena juu ya kujitolea kukamilsha ujenzi huo,basi wafungwa watumike kukamilisha kuandaa matofali,kujenga,kupaua na kusakafia huku,serikali na wananchi wakichangia vifaa muhimu kama vile bati,nondo,saruji nk.Lengo vyumba view vingi ili kupunguza msongamano madarsani na wanafunzi wengi waweze kukaa hosteli au bwenini.
5.Wazazi wanawajibu kufuatilia mwenendo wa watoto wao ili kuhakisha watoto wao wanasoma kwa kiwango kinacho kidhi haja ikiwa pamoja nakuwapa mahitaji muhimu kama vile vitabu,madaftari,kushauriana na walimu juu ya matatizo ya watoto hao,kudhibiti nidhamu na mwenendo bora kuliko jukumu hilo kuachia walimu.
6.Yarudishwe masomo ya muziki,uchoraji,upishi,ushonaji,biashara na kilimo ilikwezesha watoto kujitegemea. Baadhi ya wanafunzi hufikia hatua ya kujiua baada ya kufeli mtihani kwani anaona kuwa hana namana tena ya kuishi,uwepo wa masomo haya ungewezeshha wanafunzi hawa kujiajiri. Vilevile,manafunzi aliyechora vibonzo au mchezaji wa mpira(MESI) Kama somo la uchoraji lingekuwepo basi huyo angepata alama A au B,sifuri zingepungua.Na Yule aliyeandika mashairi ya muziki,naye pia angefaulu kama somo la muziki lingekuwepo.
7.Mafunzo kazini ni muhimu tena ya mara kwa kwa mara,kwani huongeza maarifa,ujuzi,mbinu mpya,ujasiri na ari ya kazi.Walimu wanakaa muda mrefu bila semina,kwenye masomo yao huku mitaala ikiwa ina badilika mara kwa mara,mihutsari mipya ikiandikwa.Hili pia litapunguza tatizo.
8.Mitaala inapobadilika basi kwa kiwango kikubwa walimu ndiyo wahusike.
9.Wapo wanafunzi wengi wenye uwezo wa kusoma nakuandika lakini uwezo wao wa kumudu masomo ya sekondari ni mdogo kutokana na ukweli kwamba wanafunzi wengi wanamaliza darasa la saba wakiwa na uelwa mdogo.Niliwahi kumwuliza mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne katika shule moja,kama anaweza kuniambia kama anafahamu ni wapi wanyama aina ya NYATI wanapatikana nchini Tanzania na umuhimu wake,alijibu kuwa wanapatikana KISUTU Dar es Salaam,na wanaumuhimu wa kuzalisha maziwa.Halikadhalika,kama ukifuatilia kipindi cha SKONGA (EATV) utaweza kuona jinsi watoto wanavyoshindwa kujibu maswali rahisi ya sekondari.
10.Wapo watu ambao wanalitupia lawama baraza la mitihani kuwa ndilo lina husika na kufeli kwa wanafunzi hawa eti mtihani haukusahhihishwa kwa makini,mtihani ulikuwa mgumu,matokeo batili nk.,lakini mimi naomba nipingane nao kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kwamba kazi ile wakati inafanyika,usalama wa taifa wanakuwepo.JE,inamaana walishindwa kuzuia hujuma hizo? Baraza la mitihani lina ruhusu kukata rufaa kwa mtu asiyerdhika na matokeo ili mtihani huo usahihishwe upya,kwanini asiyeridhika na matokeo asifanye hivyo?, baraza la mitihani linakawaida ya kuhifadhi karatasi za majibu ya watahiniwa kwa kipindi kirefu,je, kwaninitume isiundwe kwenda kuchunguza karatasi zile kama hazikusahihishwa kwa makini? Je,mwanafunzi aliyeshindwa swali siangepaswa kuacha karatasi wazi bila kuandika chochote au kuandika jibu lolote?sasa kama mtihani ukarudiwa kusahihishwa inamaana Yule aliyeandika matusi,nyimbo vibonzo apate alama hata kama swali la aina hiyo halikwepo? Mtihani kama ulikuwa siyo standadi ya walengwa mbona walimu hwa kulalamika kama umetungwa bila kuzingatia ngazi yao? Kwanini tume itayoundwa na mheshimiwa waziri mkuu isichunguze uhalali wa mtihani huo na badala yake watu wanataka serikali iangalie namna ya kuwasaidia,mara katibu mtendaji wa NECTA ajihuzuru kwa lipi? Kama matokeo yaliyopatikana yalikuwa ni hayo,je, yeye angefanyaje?inamaana alitakiwa kuachana na hayo tangaze yak wake? Angeyatoa wapi? Lamsingi ni kuchunguza kiini cha tatizo ili kuiwezesha serikali kutafuta mbinu ya kutatua.Wanafunzi wajenge tabia ya kujali mitihani na kusoma kwa bidii ilikuweza kukabiliana nayo barabara na hatimaye kufaulu,haiwezekan mtoto anakwenda shuleni akiwa amebeba daftari moja kaikunja na kuiweka katika mfuko wa ---- wa suruali na akafaulu na huku masomo shuleni yakiwa zaidi ya saba.Haiwezekani mtoto akapoteza muada kukariri mashaili ya bongo fleva akaacha kukariri what is biology,effects of mamaji war nk halafu akafaulu. Haiwezekani wazazi wakaacha watoto wakachati na facebook,luninga bila kikomo,simu bila udhibiti maalumu na akafaulu mitihani. M itihani inahitaji nidhamu ya hali ya juu. Nimeeleza machache ili kuwapa nafasi na wenzangu wachangie.
Aksante,
mamboleongoroto@yahoo.com :high5::high5::high5:
QUOTE=prince nadheem;5816986]Habari za ijumaa wanajamvi?? nawasilisha masahibu yangu na kama ikitokea kuna ushauri wowote tafadhali nauhitaji than anything else.
Ni hivi; mke wangu ni muhitimu wa shahada ya kwanza ya elimu, na wakati huo mimi ni muajiriwa wa Serikalini mwaka wa tano sasa hapa Dar . Ishu inakuja pale wakati hizi posti mpya za ajira zimetoka. maana yeye kapangiwa sehemu ambayo hata hatujawahiota!! Ni mkoa wa kagera wilaya ya M......i yaani sitaki hata kuamini hili jambo.
Tukakata shauri twende wizara ya elimu kuangalia taratibu za uhamisho kabla ya kuingia kwenye payroll, hiyo ilikuwa ni last week jumanne. tumeenda na vithibitisho vyote vya kuomba uhamisho (cheti cha ndoa,nakala ya barua yangu ya ajira pamoja na document nyingine nyingi tu) sasa baada ya kuangalia hivyo vitu wale watu wa elimu wakasema kuwa kweli tunahitaji huo uhamisho na hilo jambo lipo within their control. It was a hope for us. Ila leo tumeenda wife hajabadilishiwa mkoa wala nini na pia wahusika wa vitengo vya elimu au niseme ngazi za juu zote hawataki kuonana na watu wenye kesi kama hii yetu yaani unaanzia kamishna wa elimu,mkurugenzi wa elimu sekondari hadi katibu. sasa mi najiuliza swali kuwa hawa watu wanawasikiliza kina nani??wapo kwajili ya nani??
Upande wapili wa shilingi we are so confused so jamani kama kuna mtu yeyote anaejua how to deal with these kind of situations please give me your positive advise. Please kama hauna cha kuchangia pita tu kuliko kuleta kebehi, it is a serious matter.[/QUOTE]