Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, kodi ya nyumba ya mwaka inatuumiza

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,121
Niliwahi kuleta uzi hapa siku za nyuma ukiwa na kichwa "barua ya wazi na pongezi kwa mh Lukuvi" Ilikuwa ni barua ya kumpongeza kwa kuaminiwa katika wizara hii ngumu iliyokuwa imejaaa urasimu.

Binafsi nimefanikiwa kuishi nchi kadhaa barani Afrika, kodi zote za nyumba zinalipwa on monthly basis Tanzania nashangaa kodi ni kwa miezi sita ama mwaka wengine ndio wanadiriki kutoza hata kwa fedha za kigeni, usisahau hapo pia kuna hela ya dalali ambao hawalipi kodi.

Kama ninalipwa mshahara kwa mwezi unategemea kodi ya mwaka ntapata wapi kama sio wizi makazini rushwa na mikopo kwenye mabenki yenye riba maradufu.

Mbona mnatuumiza Serikali jamani tulie kilio gani mtusikie.

Mh Lukuvi shikamoo.
 
usilaumu wenye nyumba tu ht sirekali yetu haijajipanga.
mtu ana uhuru wa kujipangia kodi ya nyumba yake coz alitaabika ktk kuijenga.
mf shirika la nyumba linalalamika kuwa serikali haitoi kipaumbele ktk miradi ya nyumba hivyo mzigo wa kodi ktk vifaa unabebwa na shirika.
 
Kwa mtazamo wangu.. ukilipa kwa miezi mingi ni nafuu zaidi.. kwa sababu miezi mingine unafanya mambo mengine..
 
Kwa mtazamo wangu.. ukilipa kwa miezi mingi ni nafuu zaidi.. kwa sababu miezi mingine unafanya mambo mengine..
mkuu unapata wapi hela ya kulipa kodi ya mkupuo.......wewe ni mtumishi ama mfanya biashara, unakaa peke yako au unafamilia....mi nazungumzia watumishi wenye mishahara ya tgs mtumishi mwenye watoto watatu wa jinsia tofauti ambapo inabidi awe na nyumba yenye vyumba vitatu si chini ya laki tatu unamwambia alipe kodi ya mwaka.
 
Mkuu nyumba ya room 3 which means plus seating room is not less than 700,000/month na sio laki 3 labda Mbagala au gongo la mboto . Sinza/mwenge two bedroom house is from 350,000/month and above.

Kwa kweli Kwa mtumishi kulipa Kwa mwaka na vimshahara vya 400k ni wizi tu au hiyo mikopo yakuja kubebewa/kunyanganwa kitanda na tv
 
usilaumu wenye nyumba tu ht sirekali yetu haijajipanga.
mtu ana uhuru wa kujipangia kodi ya nyumba yake coz alitaabika ktk kuijenga.
mf shirika la nyumba linalalamika kuwa serikali haitoi kipaumbele ktk miradi ya nyumba hivyo mzigo wa kodi ktk vifaa unabebwa na shirika.
mbona kwenye nauli sivyo hivyo hata ununue gari china japan uingereza, liwe na ac liwe na wifi lakini kuna bei elekezi huwezi kujipangia nauli.....
 
Nyumba ni Biashara na huko unakosema wengi wamejenga mfumo wa Apartments
Sasa unakuta kama mtu ana apartmens 10 inakuwa inamlipa vizuri
Huwezi kukusema kwamba unilipe Sh 10,000 kila mwezi,hii ni ngum sana

Nyumba ni Biashara nyumba ni mtaji,sasa lazima mmiliki apate pesa nzuri ili atimize malengo yake na sio kumpangia kwamba asuburi hiyi elf 10 yako mpaka itimie miezi sita ndio atimize malengo yake.
Kuna mikoa humu Kodi ya Nyumba elf 4,lakini kulipa ni mbinde,sasa hata ikiletwa ya mwezi bado ni janga vilevile

Mfano UK,ni kwamba wapangaji wote kodi zao zinapitia makato ya mishara yao,na kodi ya nyumba pia inakatwa kodi ya Serikali,sasa wafanyakazi na wapangaji wote wanajulikana walipo na kazi wanazofanya.
Sasa hapa kwetu watu wanavyoishi kiujanja ujanja bado ni ngum sana
 
mkuu unapata wapi hela ya kulipa kodi ya mkupuo.......wewe ni mtumishi ama mfanya biashara, unakaa peke yako au unafamilia....mi nazungumzia watumishi wenye mishahara ya tgs mtumishi mwenye watoto watatu wa jinsia tofauti ambapo inabidi awe na nyumba yenye vyumba vitatu si chini ya laki tatu unamwambia alipe kodi ya mwaka.
Kuna watumishi wanaolipiwa kodi na mwajiri usidhani kila mtumishi ni hohehahe
 
Kwa mtazamo wangu.. ukilipa kwa miezi mingi ni nafuu zaidi.. kwa sababu miezi mingine unafanya mambo mengine..
Mkuu unapotoa hoja ijengee maelezo ya ushawishi mm Nita kuuliza swali: ww unafanya kazi inayokulipa kwa mwezi mwezi na isitoshe kipato chako ni kidogo sasa unapata wapi pesa ya kulia Mil. 3 ya kodi kwa mwaka? Kama sio wizi? Kuna utaratibu ambao tulikuwa tunautumia wa Tanzania ambao ulibebwa na mfumo mbaya wa wizi ambao ndio Mh. Ana deal nao kwa sasa kuweka sawa mm naimani hata hili la nyumba za kupanga atatutatulia.tu anapenda wanyonge na masikini wafaidike huyu ni tofauti na wengine.
 
Poleni sana......!! Kweli Magufuli kabana kila kona hili suala ndio linaonekana sasa hivi huko nyuma ilikuwa sio tatizo maana mishahara ilikuwa haiguswi vikao vilikuwa vingi sana wakati sasa hivi hata hela ya kuendeshea ofisi ni tatizo.
 
we unayetupa pole ni nani?
 
Nashukuru Tanzania nchi yangu sasa ina Rais ambaye amekaza center bolt ya uchumi naona kila kitu kimebanwa sawa hamna mtikisiko.

Sasa aje kwenye suala la kuthibiti mifumuko ya bei maana huku ndiko kunafanya watu wawe mafisadi na wala rushwa.

Mf.sina hela ya kodi Halafu kuna rushwa naiona ambayo itatosha kodi inabidi ulazimike kuilamba.

"Kazi Tu"
 
Kwanza wewe jina lako,tu,unapaswa ulipe kodo kubwa sana,(jokes) ila ungejua nyumba zinavyosumbua? Waliojenga wamejinyima sanaaaaaa! Wacha wapange bei wanayotaka sisi tutalipa tu,siku ukijenga utaelewa,
mfano mdogo,kitasa cha mlangoni kizuri 70000,mlango 250000,bawab 3 ni 12000,
kama vipi muamkie mwenye nyumba si mchezo,.hasa hapa dar,weka mbali na mwenye gari kabisa.
 
nina jumba sio nyumba mkuu nawaongelea wadogo zangu.
 
Back
Top Bottom