Kati ya kero zangu kubwa ni huduma za NHIF. Unaenda hospitali unahudumiwa kama muhaini!!! Yaani kama kinyaa vile ukitoa CARD ya NHIF kwa wauguzi na madaktari. Why? Fedha mfano ninayolipia mie ni sawa na ama inazidi mchangiaji wa STRATEGIS ama TANESCO health fund, lakini kwa nini huduma nisipate hospital kama AGHA KHAN ya Dar es Salaam (Mwanza naambiwa AGHA KHAN wanaendelea kuwahudumia wanachama wa NHIF na hii yawezeekana kwa sababu ya uchache wa wanachama wenye GREEN CARD-na-assume hivyo) ama BOSCHI ya Kimara??? Regency, kwa wale tulio Dar es Salaam, ndipo palikuwa kimbilio letu, lakini hospital imezidiwa sana na sasa CARD ya NHIF inaonekana ni UCHURO!!!
Tunahitaji kufanya marekebisho ya sheria ili huu mfuko kma ilivyo mifuko mingine ya kijamii, mwanachama awe na uhuru wa kuamua ajiunge wapi. Wafanyakazi wa TANESCO ni watumishi wa UMMA lakini wana mfuko wao, similary watu wa BOT wanahudumiwa na STRATEGIS (niliwahi ona hili kwa mtumishi mmoja wa BOT) na wao pia ni watumishi wa UMMA. Kwa nini kwa watumishi wengine iwe LAZIMA ukiajiriwa tu, mkataba unasema utajiunga na NHIF??? Hili ni JIPU kubwa mno.
Wanachama wa NHIF kwa kweli hatupendezwi na huduma za mfuko katika kutupatia huduma za kiafya zenye staha na heshima. Mgonjwa hupona kutokana na tiba na huduma nzuri. Siyo karaha za manesi kisa tu kuwa mwanachama wa NHIF. Hatulazimishi sisis kuwa katika mfuko huu hivyo tusihukumiwe kwa kulazimishwa kwetu kuwa wanachama.
La mwisho ni kuwa ni kwa nini kuwa mwanachama wa mifuko miwili ya jamii kama mtumishi wa umma??? NSSF wanatoa fao la matibabu kwa wanachama wao mfano. Na huyo mwanachama anaweza kuwa ni mtumishi ambaye bado anachangia NHIF. Je, hakuna haja ya kuwa mwanachama wa mfuko mmoja tu wa jamii ambao utatakiwa kutoa fao la afya kwa wanachama wake maana kwa watumishi tunachangia kote kote mpaka kustaafu.
Hili liangaliwe jamani. Tunaumia na pia tunanyanyaswa na uanachama wa NHIF.