Wivu na hasira zako vina chanzo na kwa jinsi ulivyoandika, kuna uwezekano unasumbuliwa na kati ya mambo haya; Huridhiki na mwonekano wako, huridhiki na hali ya kiuchumi uliyonayo wakati unajiona unastahili kuwa na hali ya juu zaidi usiyoifikia pamoja na jitihada nyingi unazozifanya, Umezungukwa na watu waliokuzidi uwezo na huna la kufanya. Angalia pia mambo mengine ambayo yanakufanya usijiamini uyarekebishe kwani wivu na hasira mara nyingi huwa yanaletwa na kutojiamini ingawa kwa upande wa hasira inaweza kuletwa na factors nyingine nyingi pia.
Mfano, unaweza kuwa mbishi, mgumu wa kusikiliza wengine na usieshaurika, watu watadhani wewe ni mkali na mkorofi wakati kumbe kinachokusumbua ni hofu ya kudharaulika inayosababishwa na kutojiamini kutokana na kudhani kuwa watu wanakudharau kwa ufupi wa kimo chako, rangi ya ngozi, sura mbaya n.k na hivyo unakuwa mtu wa kujihami kwa kutanguliza hasira.
Si lazima uangukie katika hayo niliyotaja kwani kuna sababu nyingi nyingine zinaweza kusababisha hilo na anaezifahamu vyema ni wewe.
So jiulize ni kipi kinachokutia wasiwasi na kutojiamini ukirekebishe.