Wito wangu kwa Viongozi

ofisa

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2011
Posts
4,374
Reaction score
4,114
Nimesikitika kuona bei ya samaki wa baharini ikipanda sana mpaka kufikia shs 8500 kwa kilo moja wakati mwaka 2017 nilikuwa nanunua samaki shs 4500 wale wa wachina.tukasikia wamesimamishwa ili kazi tuifanye wenyewe baada ya hapo ni kuongezeka kwa bei mpaka leo. Nashauri wachina warudi na huo blue economy ya Dr Mwinyi ipiganiwe na huku bara uanze ni aibu kwa kweli.

Maji ya bowser -Morogori,miaka 2 nyuma kwa sisi wakazi wa kitungwa na kingolwira hatukuwa na shida ya maji mpaka kuagiza bowser, leo hii baada ya JPM kuondoka tunaona kama ndio imekuwa biashara,kamati ya maji maeneo husika na MORUWASA hawaelewani kutuhudumia wananchi.la kujiuliza jeshi na Magereza wao maji hayakatiki.maana yake sisi tu wakazi ndio tunaoumia na tunatumika kama wateja wakubwa wa bowser.

Kwa muda mrefu kuna mradi unatajwa ule wa mindu kuzungukia Tubuyu na Tungi,mradi ambao wananchi status yake ni kitendawili.
kwanza mradi hauwezi tena kukatiza kwenye mradi wa mwendo kasi.

Pili tuliona kusainiwa kwa mkataba wa 33 bil ,baadae tuliona mtendaji mkuu akitenguliwa kwa kusaini mkataba bila idhini ya wizara. Hatujui nini kimeendelea kwenye huo ufadhili. Kama maji yaliwezekana kupatikana huko nyuma iweje kipindi hiki.? Kama jeshini wanapata iweje kwetu utaiani?

Na kama maji yanapatikana hadi stesheni yakiwa na presha nzuri kwa nini hayafiki mtaa wa mahakamani, shule na bomba la mafuta?
Hoja ya tatu tofauti ni kuhusu vipimo,ukienda sokoni wanatumia kopo la lts 1 kuuzia njegere,hivi wenye wizara husika za kuwalinda wakulima msisisitize itumike mizani rasmi ili tusiwalangue wakulima?

Mawazo yangu.
 
Ukali wa maisha ndio kipimo cha akili

Tunalazimishwa kuwa na mashamba madogodogo na bustani majumbani ili tulime ufuge kwa ajili ya chakula; Samaki kidogo, kuku kidogo, mbuzi kidogo, ng'ombe wa maziwa, mchicha, nyanya, vitunguu na viazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…