Wito wa kuishitaki Kenya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa kwenye Ekolojia ya Serengeti Masai MARA

Alice Gisa

Senior Member
Sep 6, 2014
172
417
Mwaka 2007-2013 wanaharakati wa Kenya kwa masaada wa wanaharati wasiowazalendo wa Tanzania walianzisha kampeni na kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kupinga ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mugumu wilayani Serengeti.

Hoja ikiwa barabara ya lami na uwanja huo wa kimataifa wa ndege utabughudhi uhifadhi wa mfumo wa maisha ya Wanyamapori.

Leo mwaka 2021 Wakenya wale wale waliofadhiri harakati hizo wanajenga uwanja wa kimataifa ndani kwenye hifadhi ya Masai Mara. Kama ilivyotangaza na Waziri wao wa usafirishaji na uchukuzi bw Solomon Kitungu tarehe 11.08.2021 na kunukuliwa na gazeti la the Standards pita link Tourists to jet directly to Maasai Mara once airstrip is expanded

Nikujuze, Masai Mara ni sehemu ya ekolojia kubwa ya Serengeti Masai Mara. Ekolojia hii hujumuisha hifadhi tatu kubwa.... Serengeti, Ngorongoro zilizoko Tanzania na Masai Mara iliyoko Kenya.
Aidha kuna hifadhi ambatano ndogo katika ekolojia hii.

Wakenya walilalamika kua, ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege Tanzania utadhuru Serengeti. Makelele ya ndege na kadhia za barabara zitaudhi wanyama na kuharibu ekolojia nzima. Hivyo kuathiri pia hifadhi yao ya Masai Mara.

Hivyo imetolewa wito wa kufungua kesi katika mahakama ya East Africa Court of Justice EACJ.
Kesi hii ombi lake, mosi ni kupinga ujenzi wa Uwanja huo wa Masai Mara.
Pili kama uwepo wa Uwanja wa ndege hauna madhara , basi Tanzania ilipwe harasa iliyopatikana kwa kutokuwepo uwanja wa kimataifa Mugumu Serengeti. Kwani ujenzi wake itakua ukizuiliwa kwa hila.
Tatu ni kuweka wito uwanja wa ndege Serengeti wa kimataifa ujengwe haraka.

Wito na.
Bunda Mara Tanzania
Email Kubwerafrank@gmail.com
Simu 0764363651
 
Mwaka 2007-2013 wanaharakati wa Kenya kwa masaada wa wanaharati wasiowazalendo wa Tanzania walianzisha kampeni na kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kupinga ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mugumu wilayani Serengeti...
Una hoja nzuri lakini nia ya kufungua kesi ndiyo imekuangusha. Wewe unasema kesi ifunguliwe kwa sababu wakenya nao walitufanyia roho mbaya! Mimi naona sababu iwe ni kulinda mazingira na siyo kukomoana.

Kama nitavyopinga uharibifu wa mazingira nchini kwangu Tanzania, hivyo hivyo nitapinga nchini Kenya na duniani kote. Ukishasema sababu ni kulipapiza kisasi basi hoja yako inakuwa haina maana.
 
Una hoja nzuri lakini nia ya kufungua kesi ndiyo imekuangusha. Wewe unasema kesi ifunguliwe kwa sababu wakenya nao walitufanyia roho mbaya! Mimi naona sababu iwe ni kulinda mazingira na siyo kukomoana. Kama nitavyopinga uharibifu wa mazingira nchini kwangu Tanzania, hivyo hivyo nitapinga nchini Kenya na duniani kote. Ukishasema sababu ni kulipapiza kisasi basi hoja yako inakuwa haina maana.
Mtazamo wa mwandishi ni uwanja wa Mugumu ulizuiliwa kwa hila. Mazingira na Ekolojia ilikua Sanaa tu hoja ni kukwamisha watalii kufikia Serengeti kwa wepesi.
 
Una hoja nzuri lakini nia ya kufungua kesi ndiyo imekuangusha. Wewe unasema kesi ifunguliwe kwa sababu wakenya nao walitufanyia roho mbaya! Mimi naona sababu iwe ni kulinda mazingira na siyo kukomoana. Kama nitavyopinga uharibifu wa mazingira nchini kwangu Tanzania, hivyo hivyo nitapinga nchini Kenya na duniani kote. Ukishasema sababu ni kulipapiza kisasi basi hoja yako inakuwa haina maana.
Issue ya mazingira hata mimi naunga mkono ila kwenye suala la nchi kuzuiwa kufanya jambo la maendeleo kwa mustakabali wa nchi nyingine kupinga sikubaliani nalo.

Kenya walipinga si kwa sababu ya ekolojia ila walitumia hicho kama kigezo, now wametafuta pesa na kuamua kutu_time kwa haraka.

Hizi mambo zilitaka watu kama kina late Magufuri, akisema NO ni NO kweli kweli.
 
Back
Top Bottom