MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kutokana na mabadiliko ya kidunia hasa kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia, kuna mabadiliko makubwa sana kwenye mfumo wa maisha ya mwanadamu katika nyanja zote kuanzia kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na hata kijamii. Ni too local kuendelea kung'ang'ania analogy wakati tuna digital tayari, ni aibu kugangamala na chama toekea enzi za ukombozi yaani mbadala wa TANU mpaka leo, hata jina lenyewe tu "Chama cha mapinduzi" ni jina lililozeeka tayari, kuna mapinduzi ya nini hivi sasa? Lazima tuende na wakati sasa.
Vijana ndio nguvu mpya na ndio taifa letu la kesho, kuendelea kuwapika katika chungu kilichochoka ni kuwadumaza kifikra. Wanatakiwa kuiva katika jiko la Umeme au gesi na sio mafiga waliyoyatumia mababu zetu kina hayati Mwalimu Nyerere na kina Mzee Sijaona. Vijana wajiunge na upinzani ambavyo ndio vyenye nguvu na shauku ya kuingia Ikulu na sio
Chama ambacho kwa sasa kazi yake ni kujilinda kisiondoke madarakani, muda wote kinajihami hakina raha kabisa,muda wowote kinaweza kudondoka.
Kuna vijana ambao wengi wao wanakimbilia CCM kwa maslahi na wanaishi kwa tahadhali kwamba pakiharibika tu wanakimbilia upinzani, hawa ni opportunity seekers, hawana nia njema na taifa wala jamii yao. Kwanza itakua ni kuchelewesha muda maana huko ambako mtu anategemea kukimbilia baadae nako tayari kuna wajenzi ambapo ndio wanaojiunga hivi sasa.
Duniani kote vijana wasomi na wenye akili, wenye kutaka mabadiliko katika mifumo ya utawala ndani ya nchi zao hujiunga na vyama vya upinzani, ni Tanzania pekee ambapo utakuta kuna kijana msomi mwenye Shahada za chuo kikuu zaidi ya moja anakimbilia chama cha ukombozi eti ana ndoto za kuwa kiongozi wa baadae! Kwa mtazamo huo ni bora tu kijana huyo atambue kua ni ngumu sana ndoto zake kutimia kupitia Chama kilichopitwa na wakati ambacho kinaishi kwa kujihami tu maana hakiwezi kua kipya tena zaidi ya kufanya repairing.
Wanafalsafa wanasema gari ambalo lilitengenezwa miaka mingi iliyopita hata muda wake wa kulitumia ulikwishapita, hata ukibadilisha spare zake kiasi gani bado halitokufikisha kokote zaidi zinaweza kukusababishia ajali. Naifananisha CCM na gari ambalo limeshapitwa na muda wake, kilichobaki ni kubadili spares tu kama mjamaa moja alivyodai kua alikitoa shimoni maana kilikua kinaenda kudumbukia na kupotea kabisa.
Sidhani kama kijana ukiwa na mawazo yako na mtazamo wenye mvuto kwenye jamii unaweza kukosa fursa ya kujiwekea hazina yako ya kisiasa kupitia vyama vya upinzani, vyama hivi vinaendeshwa na wabobezi katika siasa za ulimwengu wa leo, ni vyama vilivyosheheni vijana huru wenye mitazamo mbali mbali na sio wale waliofungwa kuusema ukweli kwa sababu watanyimwa kula.
Nimalize tu kwa kutoa wito kwa vijana kuitumia fursa hii, kwani ndiko zinakochipukia fikra mpya badala ya zile za kukaririshwa "Ahadi kumi za Mwanatanu" waliokwishaimba sababu zetu.