Tatizo la “Windows can’t be installed on this device” mara nyingi halimaanishi kwamba kompyuta yako haiwezi kabisa kusupport Windows, bali linaashiria kuwa kuna ukinzani kati ya mfumo wa sasa na installer uliyojaribu kutumia.
Mara nyingi hii hutokea kwa sababu umeboot moja kwa moja kupitia flash/USB, jambo ambalo kwa kawaida hujaribu kufanya clean install (kufuta kila kitu na kuset Windows upya). Katika hali hiyo, Windows hukagua mfumo wa disk na BIOS mode, na ikibaini havilingani na installer uliyochagua, hutoa kosa.
Moja ya visababishi vikuu ni tofauti kati ya MBR na GPT. Kama hard disk yako imewekwa katika mfumo wa MBR (ambao ni wa zamani) wakati installer inahitaji GPT (wa kisasa unaotumika kwenye UEFI BIOS), basi Windows hukataa kuendelea. Sababu nyingine inayojitokeza mara nyingi ni wakati BIOS imewekwa kwenye mode isiyo sahihi (mfano, Legacy badala ya UEFI). Hizi zote husababisha installer kushindwa kukubali kuendelea na usakinishaji.
Njia rahisi zaidi ya kuzuia kupoteza data ni kutofanya installation kwa njia ya boot kupitia flash. Badala yake, fungua kompyuta yako kwa kawaida na uingie kwenye Windows uliyonayo sasa.
Ukishafungua flash yenye Windows, tafuta faili linaloitwa setup.exe na lifungue kwa kubofya mara mbili.
Hapo utapata chaguo la Upgrade this PC, na katika hatua ya “What to keep” hakikisha umechagua Keep personal files and apps. Njia hii itafanya Windows ibadilishe system files pekee huku data zako zikibaki salama.
Faili sahihi la Windows 10 unaweza kulipakua moja kwa moja kupitia tovuti ya Microsoft:
Download Windows 10 Disc Image (ISO File).
Hakikisha unaendesha setup ukiwa ndani ya Windows uliyonayo badala ya kuanza installation kwa ku-boot kutoka USB. Njia hii ndiyo rahisi zaidi na salama kwa watumiaji wengi.