hii inaweza ikawastua wengi, lakini ukweli ni kuwa watu wengi sana hawayajui maneno ya wimbo wa taifa, hasa watoto wetu waliosoma baada ya trade liberalization, ambapo mambo ya chipukizi, halaiki na hata JKT ilisimama kwa muda. Kosa la kawaida ni kuchanganya maneno ya ubeti wa pili na wa kwanza. Sitashangaa kabisa kama vijana wa miaka ishirini mpaka ishirini na tano hivi hawajui maneno ya wimbo huu.
Natafuta nafasi nizipate nyimbo zote patriotic tusipoangalia tutazipoteza. Natafuta kuwasha mwenge, tazama ramani, na Tanzania tanzania nakupenda kwa moyo wote. Yes Nilalapo naiota Tanzania ( whats wrong with that?) Nafikiria tulikotoka tulipo sasa hivi na tuendako. Niamkapo ni heri kwa sababu mambo yalivyo sasa ndoto nyingi ni nightmare.
Nadhani saa nyingi maneno yanatuumiza kwa sababu tunayatafsiri kutokana na uelewa wetu wa mambo.
Mungu Ibariki Tanzania. I will love Tanzania forever despite being discouraged by mafisadi.