Wimbo wa Papii Kocha umenitoa machozi

Ana tamani kulia??? Anyoroshe maneno labda anawalilia wamfanye kama walivyowafanya vile vitoto na kutiwa hatiani na mahakama
 
Punguza mihemko wewe...

Kwanza bado wana kesi ya kujibu hawa.
Na video haihusiani na kinachoimbwa.
Yaani hata sielewi kwa nini watu wanakuwa na vimuhemuhe na miamko ya ajabu ajabu kiasi hiki.
 
Daaah huyu jamaa niliwahi kusema akirudi kuimba Tena Dunia itasimama.

Yasome mashairi yake hapa.

Verse 1.

Dunia inazama, naangalia,
Sina cha kufanya,moyoni naumia.
Mawazo yangu oh, naangamia
Uko wapi Mungu wangu we,hunioni nalia

*Kumbe ulikua unanisikia , unaniangalia.....weweeee
Likapotea,tumaini langu ila imani ikaingiaa....×2

Chorus

Waambie, uliniona,nilipokuomba uliskia,na ukaitika.
Mungu wambie,uliposema uwaja, wala hukukosea njia, na ulifika.
Mungu wambieee, niwewew tuuu, niwewee tuuu, wuwuwu.
Mungu wambie eeh, niwewe tuu uliesababisha leo imefika.

Verse 2.
Wambie, kila siku ni zawadi, hakuna heshima inayozidi uhai.
Ni Nineema na Rehema, wawe ha hekima unazitimiza ahadi,
Ooh ooh wambie, hawapaswi kukata tamaa, sababu daima haupo mbali.
Ukipotea mwanga, gizani ndo nyota hunga'aa mwanga mkali.

Wambie,
Wasiache tumaini ndo imaniiii iii
Wasiache kukuamini ndo amanii ii iii

Chorus

Waambie, uliniona,nilipokuomba uliskia,na ukaitika.
Mungu wambie,uliposema uwaja, wala hukukosea njia, na ulifika.
Mungu wambieee, niwewew tuuu, niwewee tuuu, wuwuwu.
Mungu wambie eeh, niwewe tuu uliesababisha leo imefika. ×2

Link hii kuitazama video yake

Wabakaaaaaaaaaaaaaaaji walawiii8iiii8iiti
 
Kama ushawahi kukupatwa na matatizo mazito wimbo wowote wenye huzuni utakumwaga chozi,lakini kama hujawahi kupitia vigingi vigumu huu wimbo utaona kama ngororo,m huu wimbo unahudhunisha.
 
Back
Top Bottom