Wimbo na Matukio

kimadui

Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
32
Reaction score
46
Natumai mpo good Wana JF, na tunaendelea na kazi na shughuli zetu mbali mbali Ili kulijenga Taifa letu.

Turudi kwenye mada tajwa.
Hivi ulishawahi kua unafanya kazi fulani ama tendo lolote, ila kipindi unafanya hio kazi ama tendo ukawa unasikiliza redio, mara unasikia nyimbo ambayo ndo mara ya kwanza kuisikia na kilichoimbwa au kijisehemu Cha nyimbo kikaongelea kitu unachokifanya kwa muda huo?

Mimi nakumbuka ilikua 2003 kama sio 2004 nlienda kumsalimia bro wangu alikua akiishi gheto na mshikaji wake mmoja hivi, basi baada ya kufika bro sikumkuta, nikamkuta mshikaji wake ambae pia nlikua nikimuita bro akiwa anakorofisha kitu cha ubwabwa nyama.

Baada ya msosi kuiva ukatengwa tukawa tunakula mdogo mdogo huku tunaskiliza redio nakumbuka ilikua kipindi Cha showtime enzi hizo redio free Africa RFA inabamba balaa.
Sasa bana ikapigwa ngoma ilikua ndo mara ya kwanza kuisikia ilikua ni ya Juma nature - Mzee wa busara. Si mnajua enzi hizo ukiwa unakula na mkubwa tena hasa nyama ama samaki lazima uvizie vizie mpaka mkubwa aanze kwanza ndo na wewe ufatishe.

Sasa na mimi ni Kawa nategea bro aanze kuchukua jipande la nyama naona kama na yeye anategea tu nikaona isiwe tabu nikaingia front nikajichikulia jipande la nyama ile naweka tu mdomoni nikasikia mstari Katika ule wimbo unasema nanukuu.

" Tukiwa tuna kula na mtoto wa mzee wa busara yeye ndo wa kwanza kuchukua nyama ukimkataza ma maaa! anaenda kusema"

Aisee stimu yote ilikata kabisa. Hii nyimbo ya mzee busara mpaka leo nikiisikia huwa nakumbuka hili tukio.

Je wewe ilishawahi kukutana na tukio kama hilo??

Mtanisamehe ndugu zangu mimi sio mwandishi mzuri.
 
mimi kila nikitoka kazini halafu nipitemaeneo ya Bar huu wimbo unanijia kichwani mwangu

enjoy life is too short
kamata kamata kamata, kamata
aaah shii
kamata kamata kamata, kamata
eti babe wangu anivuruge ubongo
hata kazini kwangu wanichanganye kichwa,
mmmh
wee sio kweli
wee beer tamu
aaah, asikwambia mtu tutu, beer tamu
beer beer mitungi beer tamu
aghii beer tamu
asikwambie mtu tutu, beer tamu
beer beer mitungi beer tamu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…