GE2025 Wilson Mahera: Samia ametimiza maono ya Mwalimu Nyerere, Butiama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea wa nafasi ya Ubunge kwenye Jimbo la Butiama Mkoani Mara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Wilson Mahera amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ndoto na maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kujenga Chuo cha Kilimo Butiama Mkoani Mara ambapo takribani shilingi Bilioni 102.5 zinatekeleza mradi huo mkubwa.

Dkt. Mahera amebainisha hayo leo Ijumaa Oktoba 10, 2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Butiama, waliokusanyika kwenye Viwanja vya Mwenge, Butiama kwenye Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema tayari jengo la ghorofa 16 limeanza kujengwa na majengo mengine yakijengwa Tabora.

Dkt. Mahera kadhalika katika salamu zake ameeleza kuwa wananchi wa Butiama hawamdai Dkt. Samia kwani zaidi ya Bilioni 345 zimetolewa na serikali yake katika kipindi cha miaka minne ya serikali yake, fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Wilaya hiyo.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule 9 mpya za Sekondari, 8 za Msingi pamoja na mabweni 18 ya sekondari na 3 ya Shule za msingi, ujenzi wa shule ya amani Butiama iliyogharimu takribani shilingi Bilioni 1.6 sambamba na kuweka historia ya kufanikisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa mara ya kwanza kwani tangu kuanzishwa kwake, Wilaya hiyo haikuwahi kuwa na Hospitali yake.

Mahera amemshukuru Dkt. Samia pia kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya Bilioni 70, akisema kukamilika kwake kutaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Wilaya hiyo yenye historia kubwa na Tanzania.

Pia Soma: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kipindi cha Magufuli, Dr. Wilson Mahera Charles anagombea Ubunge wa CCM
Your browser is not able to display this video.
 
Mgombea wa nafasi ya Ubunge kwenye Jimbo la Butiama Mkoani Mara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Wilson Mahera amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ndoto na maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kujenga Chuo cha Kilimo Butiama Mkoani Mara ambapo takribani shilingi Bilioni 102.5 zinatekeleza mradi huo mkubwa.

Dkt. Mahera amebainisha hayo leo Ijumaa Oktoba 10, 2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Butiama, waliokusanyika kwenye Viwanja vya Mwenge, Butiama kwenye Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema tayari jengo la ghorofa 16 limeanza kujengwa na majengo mengine yakijengwa Tabora.

Dkt. Mahera kadhalika katika salamu zake ameeleza kuwa wananchi wa Butiama hawamdai Dkt. Samia kwani zaidi ya Bilioni 345 zimetolewa na serikali yake katika kipindi cha miaka minne ya serikali yake, fedha ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Wilaya hiyo.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule 9 mpya za Sekondari, 8 za Msingi pamoja na mabweni 18 ya sekondari na 3 ya Shule za msingi, ujenzi wa shule ya amani Butiama iliyogharimu takribani shilingi Bilioni 1.6 sambamba na kuweka historia ya kufanikisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa mara ya kwanza kwani tangu kuanzishwa kwake, Wilaya hiyo haikuwahi kuwa na Hospitali yake.

Mahera amemshukuru Dkt. Samia pia kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya Bilioni 70, akisema kukamilika kwake kutaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Wilaya hiyo yenye historia kubwa na Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…