Thanks kwa kina Eliekeem, Tuma, Wacha, JK, na Rufiji and all others of our type. These ones we even share a bottle. Ngoja nihamie kwenye thread ile wanayosema Kikwete knows very well Kenya will momopolise EA?TZ.. Sasa Smatta, mwanzoni ilikuwa ni mapambano yangu na wewe, sasa umeona wenye nchi wamekuja. Hapa ni nguvu ya hoja. Mbona sijaona ndugu yako nomasana anaandika hata Kiswahili kidogo, yeye ni kizungu tu. Ndiyo, Eliekeem, hata policy ya bretton institutions ni kuona tunakuwa soko moja ili wauze vizuri, wakati wao wanalinda masoko yao na kwa vile walishajiandaa. Wanateka multilateral trading system kuwa ya kwao. Ninachoona, interests zao zinamatch na za Kenya, Kenya wao wakitaka sehemu ya ku-off load their army of unemployed na ardhi yetu nzuri. Sasa wanaokula hasara ni sisi, maana even our only bargaining chip (ardhi na raslimali zetu) vitapokwa. Smatta, mwende mmwagilie kule Narok na Turkana, you can do it, si mmesoma? Technology si mnayo?
Hata hivyo hatua inayofuata ya integration it's an uphill task itself. Kuna convergence criteria ambazo kwa maoni yangu hatikuja kufikiwa hata siku moja, mpaka Yesu arudi.
Nchi zote tano zinatakiwa kuwa na inflation rate 5% or less (Matajiri kina Smatta wana 29.7%, Uganda kuni ma kitu, sisi 9.7%), rwanda na Burundi sijafuatilia. Ni mwaka gani zitafikia hiyo five, naomba nisaidiwe. Foreign reserve coverage ni six months, nchi zinazojitahidi zina 4 months. Kuna one off cost za adjustment, hiyo nayo ni kasheshe. Kuna budgte deficit rate ambayo hutakiwa kui-run kwenye bajeti yako, nayo ngumu. Economic growth rate, nayo ngumu. Sasa kwa nini tusifanyie hayo kwanza kabla ya kuanza mambo ya sarafu moja huku tukijua kwamba vigezo hatuna. Pia Kenya wanaweza kuwa wameahidiwa misaada ili wapush hii federation, they have been in wrangle with DP's kwa muda mrefu, wanataka watokee hapo.
Kwa suala la ajira, bado suala la work permit liko pale pale (Smatta hapendi hili), cha muhimu ni immigration kuzibana au kutotoa kabisa, ni uzalendo unatakiwa, sasa vijana wetu watakula wapi? Halafu suala la kusema watanzania are lazy dogs, mtu ajiseme mwenyewe, kama ni kilaza hayo ni ya kwake. Mi nimeishi na wakenya na waganda na wanyarwanda na kufanya kazi nao, hamna chochote, if anything utamaduni ni ule le wa kiafrika. Kama ni attitude towards work, waafrika tuko sawa, ingawa mi nina my school of thought kwa hili. Smatta, kwani kuishi nje ya nchi inaichukuliaje? Mimi sihitaji kutangaza, nilisoma
www.laroche.edu na nikafanya kazi
www.northsidebank.com na nikaamua kurudi kwenye nchi yangu ya asali na maziwa, na nina raha sana na ninakula kuku kwa mrija. Si hapo tu, nimefanya mashirika ya kimataifa na kitaifa, but so what. Hoja ni fast tracking ya federation, tunapelekwa kasi mpaka tunashituka, ni kwa faida ya nani? Ni mkono wa nani, kama mjumbe mmoja anavyosema, media na watu wa nje hawajalishtukia hili, ingawa huko nyuma msimamo wao ni kwamba watZ wengi hawataki, iwe media au wanchi wenyewe. Smatta, you seem to envy this romantic country, wewe ishi, hata wachina na wahindi wanaishi, but at the end wenye nchi lazima tujue and one we will take stock. Ukisema wewe unatengeneza hela kwa mgongo wetu, wachina na wahindi watasemaje.? U r the same. Magogo yetu yetu yote mmemaliza, na kufyeka misitu yetu, wageni mmeshatufanya uchochoro, madini, pembe za ndovu na vitu kibao mnasomba, lakini watu makini watakuja. Hatuna viongozi, mafisadi hawawezi kukamata wezi wenzao hata kama ni wa nje, wanajuana, wanawagawia kile wanachopora. Nchi hii inaongozwa na mafisadi, sishangai yanayotendeka, uzuri hata Sophia Simba alishatuthibitishia, tena rasmi kuwa yeye na mabosi wake ni mafisadi nyangumi. Kwa hiyo suala si biashara tu, ni biashara ipi unafanya na unaifanyaje, that's what counts Smatta.