Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 23,905
- 31,686
Hatimaye zimebaki siku chache tuweze kushuhudia mpambano wa marudiano kati ya Deontay Wilder (Bronze Bomber) na Tyson Furry (Gypsy King).
Katika pambano lao la kwanza lililofanyika mwaka 2018 Dec 08 , matokeo yalikuwa ni sare (Split Draw) ila Wilder alimkalisha mara mbili Tyson japo Tyson alifanikiwa kunyanyuka na kuendelea na mchezo na kufanikiwa kumaliza raundi zote 12.
Katika pambano lao la kwanza ubishi mkubwa uliibuka huku pande zote mbili zilionesha kutokubaliana na matokeo ,kwa upande wa Wilder walidai mwamuzi alimbeba Tyson kwa kutumia muda mwingi kumuhesabia kuliko kawaida (15 seconds), upande wa Tyson ulidai Tyson ali dominate raundi nyingi sana hivyo kutoa matokeo ya sare ni kuwaonea upande wao.
Pambano la marudiano litafanyika 22 Feb 2020 katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena .
Mpaka sasa Deontay amepambana jumla ya mapambano 43, 42 ameshinda na moja ametoa sare dhidi ya Tyson, kwenye mapambano hayo 42,41 ameshinda kwa Knockouts na 1 ameshinda kwa Uninamous Decision(UD) .
Tyson amepambana mapambano 30, ameshinda 29 ,20 kwa Knockouts na moja ametoa sare dhidi ya Deontay Wilder.
Aina ya upiganaji ,wote ni orthodox ,japo kwa skills Tyson ni mzuri zaidi kuliko Wilder ila hana nguvu,Wilder sio mzuri sana kwenye boxing skills ila ana nguvu sana.
Hivyo kama watafanikiwa kumaliza raundi 12 ni rahisi sana kwa Tyson kuibuka na ushindi kinyume na hapo tungojee knockout nyingine ya Deontay Wilder ,na bahati nzuri Wilder huwa anazungumza mara kwa mara kwamba kama unahitaji kumpiga basi utahitaji upate raundi 12 za kusimama naye ulingoni ila yeye atahitaji sekunde mbili tu ili kukukalisha hivyo ukipigana naye usifumbe macho hata kwa sekunde moja maana atakumaliza.
Wilder ametoa ahadi kwamba atahakikisha safari hii Tyson haamki ,huku Tyson amejisifu kwamba amefanya mazoezi ya kutosha kuweza kumkabili Wilder pia amedai kuwa Wilder hana nguvu kiasi hicho kama anavyozushiwa ,bali Wladmir Klitschko ndiye bondia mwenye nguvu zaidi.