Mimi nimeisoma vizuri ripoti ya richmond na ukweli ni kwamba hakukuwa na kamati ya tanesco bali kulikuwa na kamati kuu ambayo mlikuwa na wajumbe toka tanesco, wizara ya nishati, mwanasheria mkuu, wataalam wa uchumi na pia kulikuwa na kamati ndogo ndogo ambazo zilikuwa ni za ufundi, sheria nk. kamati kuu ambayo ilikuwa chini ya waziri mkuu ndiyo iliyotoa mapendekezo ya majumuisho ambayo waziri mkuu ndiyo aliyoyawasilisha kwenye baraza la mawaziri. Hata baada ya serikali kuridhia hilo [baraza la mawaziri] wakati wa utekelezaji wa mradi huo kuna mapungufu yaliibuka ambayo yalimshtua WM na alimuarifu mkuu wa kambi juu ya anavyoona na hatua ambazo alitaka kuchukua dhidi ya mapungufu hayo. Kwa vile mkuu wa kambi alikuwa nje ya nchi, WM aliombwa avute subira hadi atakaporejea ili suala hili lijadiliwe kwenye baraza na ndipo hapo mandumila kuwili walipo leak mambo hayo na kufanywa kama kashfa inayomhusu WM.
unahangaika NDO MAANA yeye akuridhishwa na kampuni iyo kumbuka waziri hasaini mkataba ,waziri mkuu haingii kwenye gorvement negotiating team ..hawa ndo ushauri wao ulisikilizwa... yeye mpaka mwisho alianza kuitilia mashaka iyo kampuni hata membe unalijui vizuri hili swala.... sasa yeye hataki kuligawa taifa wala chama chake
Uongo mwengine huu,membe hakuwa foreign affairs 2006 wakati Lowassa anaboronga.
Lowassaalimshinikiza msabaha kukiuka taratibu ili Richmond wapewe mkataba.ilipokuja kuthibitika ni kampuni ya mfukoni,Lowassa huyu huyu akamtumia rafiki yake Karamagi kusaini mkataba wa Dowans hotelini London.sasa Karamagi ni mfadhili mkuu na mpambe mkuu wa Lowassa.
Unadhani watanzania wapuuzi kumuita huyu bwana mwizi ba fisadi?hakuna njia nyengine.
Amepata nafasi zaifi ya 1000 kuitetea kakaa kimya kwa kuwa ni mkosefu.
Anajidai nitasena ukweli mkinichagua,ili aje kuwaruka.mtu mwenyewe graduate wa sanaa huyu.
Membe ameingiaje hapa? Hebu fungua ubongo wako. Membe na yeye tutamchambua hapa hapa. Kwasasa anaye hatarisha usalama na Ustawi wa Tanzania kwa miaka 10 ijayo ni Lowassa. Na kwa kuwa Magazeti yamenunuliwa na hayafanyi uchambuzi yakinifu, tutasema tu Ukweli.
Uongo mwengine huu,membe hakuwa foreign affairs 2006 wakati Lowassa anaboronga.
Lowassaalimshinikiza msabaha kukiuka taratibu ili Richmond wapewe mkataba.ilipokuja kuthibitika ni kampuni ya mfukoni,Lowassa huyu huyu akamtumia rafiki yake Karamagi kusaini mkataba wa Dowans hotelini London.sasa Karamagi ni mfadhili mkuu na mpambe mkuu wa Lowassa.
Unadhani watanzania wapuuzi kumuita huyu bwana mwizi ba fisadi?hakuna njia nyengine.
Amepata nafasi zaifi ya 1000 kuitetea kakaa kimya kwa kuwa ni mkosefu.
mkuu kimweri acha kukuRUPUKA kujua kitu sio lazima awe waziri wa mambo ya nje kwa kipindi icho.....
pia walioshauri wapewe mkataba ni gorvement negotiating team acha uongo na waziri mkuu hakuingia kwenye gorvement negotiating t... pia njo na video na huo mkataba aliosaini karamagi tukujue kweli kama wewe ni mkweli .. otherwise unakua mwongo mwongo
UONGO.
Lowassa alishiriki kusaini mkataba wa Richmond wakati Raisi hayupo nchini,msipitoshe mambo.ripoti ya Richmond iko wazi na tuliijadili kwa mapana n marefu humu 2008.
Sababu kubwa ya Richmond kumuangukia Lowassa ni yeye kulazimisha msabaha,waziri mhusika kukiuka taratibu za mkataba kusimamiwa na katibu mkuu wa wizara.msabaha alitamka wazi yeye alitolewa kafara na Lowassa.
Danganya hao waliokuja JF mwezi mei.
Utakatifu gani unaouamini wewe? au ndio kukopi semi na kuzileta humu.Watanzania gani hatutaki pamoja kundi lake ikulu nu mahali patakatifu
"kipi ambacho nilichofanya bila kukutaarifu mwenyekiti wangu?.......mbona munawaacha hawa vijana wadogo wanaendelea kunichafua majukwaani na hii habari ya richmond".........ndipo rais mstaafu benja akaingilia kati na kumwomba mzee el atulie na hiyo hoja iachwe.....
Ni maelezo gani ya Mwakyembe mnayoyasema juu ya Lowassa tofauti na haya hapa chini? nadhani Mwakyembe mwenyewe alikuwa wazi juu ya hili na next time usitufanye waTanzania wote wapumbavu, leteni huo ushahidi tutawaelewa.
Kutoka kwenye Hansard za Bunge, hii ni sehemu ya hotuba ya MHE. DR. HARRISON G. MWAKYEMBE MWENYEKITI WA KAMATI TEULE YA RICHMOND kwenye MKUTANO WA KUMI - KIKAO CHA KUMI NA MOJA - TAREHE 15 FEBRUARI, 2008.