Yani hawa ndio usiseme kabisa mkuu. Mimi leo nimekwenda kwao,nilihitaji huduma ya nduki.Jibu nililopata,kama isingekuwa mvua imenyesha,ningekaa chini nikachekaaa mpaka basi. Dada niliyemkuta mapokezi,mbali na kuniambia kwamba ile huduma ni kwa wale wenye simu za mezani tu,lakini alinishauri nisitumie huduma hiyo. Amesema mwanzo ilikuwa iko fresh,lakini kwa sasa wateja wengi wanalalamika sana kutokana na speed kudrop kwa kasi ya ajabu.
Mimi nipo Moshi nimeishaachana na huduma yao,coz saa inaisha sijadownload hata 100MB,huu si wizi kabisa! Wanasema malipo kwa saa halafu wanabana speed,mi hata sitaki kuwasikia kabisa. Labda nyie mlio mikoa mingine mnapata speed nzuri,ila huku nilipo ni michosho tu.